Mbegu mpya na uhakika wa chakula Sudan Kusini

Kusikiliza /

mbegu mpya Sudan Kusini

Wakulima wa hali ya chini katika Jamhuri ya Sudan Kusini wanapatiwa mbegu bora ili waweza kuzalisha mazao muhimu ikiwa ni sehemu ya kuwainua kimaisha .

Mpango huo ambao unapigwa jeki na serikali ya Ufaransa kwa kushirikiana na shirika la chakula duniani FAO na Wizara ya Kilimo nchini humo unatekelezwa katika majimbo kadhaa na kwa muhula wa kuanzia mwaka mmoja kwenda mbele Taarifa zaidi na George Njogopa:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mradi huo wenye kugharimu kiasi cha dola za kimarekani 612,000 utawasaidia wakulima katika maeneo ya uzalishaji, uhifadhiji wa chakula na kuwa na soko la kuaminika juu ya mbegu. Pia umelenga maeneo ya uvunaji wa mazao kama mahindi, mihogo na jamii ya kunde.

Kuwepo kwa mradi huo kunatarajiwa kusukma mbele ustawi jumla wa wakulima wengi ambao wanatajwa kuwa nimaskini na kiwango chao cha maisha ni cha hali ya chini.

Miongo kadhaa ya mapigano kulikosababisha pia mamia ya watu kwenda kuishi uhamishoni ndiyo sababu kuu iliyofanya wakulima wengi kutojihusisha kikamilifu na shughuli za kilimo na wachache wao waliendelesha kilimo kisichozingatia ubora.

Maeneo hayo pia yamekabiliwa na ukosefu wa dhana za kisasa za kuendeshea shughuli za kilimo na hivyo kusababisha kuporomoka kwa mavuno.

Mkuu wa ofosi fao mjini Juba, Sue Lautze emesema kuwa kuwepo kwa mbegu bora ndiyo mwarobaini hasa wa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula kwenye eneo hilo na kuongeza kuwa pamoja na hali mbaya ya ukosefu wa chakuka inayoshuhudiwa sasa, lakini serikali imehaidi kukabiliana na hali hiyo na imewahakikishia wananchi wengi itafanya kila liwezekanalo kuwapatia chakula.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930