Mazungumzo ya kusaka amani ya Darfur yaanza kupiga hatua

Kusikiliza /

Edmond Mulet

Wakati mazungumzo ya kusaka amani baina ya serikali ya Sudan na kundi moja la waasi kuhusiana na mzozo wa Darfur yanaendelea kupiga hatua huko Doha, Umoja wa Mataifa umeitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuendelea kutupia macho kwa karibu ili kusaidia kutanzua mkwamo huo.

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama kuwa kuna haja kwa jumuiya ya kimataifa kufuatilia kwa karibu pande hizo zinavyoendelea na majadiliano ili kuona kwamba amani ya kudumu inapatikana.

Pande hizo zinazozozana zimekubaliana agenda ya majadiliano baada ya kuvutana kuhusiana na mambo muhimu yanayopaswa kujadiliwa. Maafisa wa serikali na wawakilishi wa kundi la Justice and Equality Movement JEM walikutana huko Doha, Qatar na kukubalina juu ya agenda za majadiliano.

Pande hizo zilitarajiwa kutia saini makubaliano ya awali ambayo ndiyo yanaweka msingi wa kuendelea na majadiliano ya kusaka suluhu ya Darfur.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031