Magonjwa yaliyosahaulika kutokomezwa kabisa: WHO

Kusikiliza /

Shirika la afya duniani, WHO limejivunia maendeleo ya aina yake katika vita dhidi ya magonjwa 17 yaliyosahaulika ambayo yameendelea kuwa mzigo mkubwa kwa nchi maskini duniani. Magonjwa hayo ni kama matende, mabusha, kichocho na usubi.

WHO imesema hatua hiyo imetokana na mkakati wa dunia unaotumia mbinu rahisi ya tiba na kinga na ushirika wa kimataifa na hivyo kuonyesha dalili ya kutokomezwa kabisa kwa magonjwa hayo ifikapo mwaka 2020.

Shirika hilo limezindua mjini Geneva Uswisi ripoti kuhusu magonjwa hayo na awamu mpya ya kupambana hayo ambayo limesema magonjwa kama vile kichocho, usubi na vikope husababisha madhila makubwa kwa nchi maskini lakini mwaka 2010 pekee watu Milioni 711 walipata tiba angalau dhidi ya magonjwa kama matende, kichocho, minyoo na mabusha.

Kouadio Adjoumani ni Balozi wa Kudumu wa Cote D'Ivoire katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

(SAUTI ya Kouadio)

WHO inasema katika miaka mitano ijayo tiba dhidi ya kichocho itafikia watu zaidi ya Milioni 235 na hilo litawezekana kwa kuongeza upatikanaji na usambazaji wa dawa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031