Mafuriko Msumbiji yasababisha wengi kukosa makazi

Kusikiliza /

waathiriwa wa mafuriko Mozambique

Serikali ya Msumbiji kwa kushirikiana na mashirika ya misaada imeanzisha juhudi za kuwanusuru mamia ya wananchi ambao wameathiriwa kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba taifa hilo.

Kiasi cha watu 150,000 wanahitaji msaada wa dharura baada ya makazi yao kuharibiwa na mafuriko yaliyotokea katika jimbo la Gaza, lililoko kusini mwa nchi hiyo.

Mamia ya manusura wa mafuriko hayo walilazimika kukimbia katika maeneo ya mbali na wengi wao walikimbia kwa miguu hadi katika kambi ya moja iliyoko Chiaquelane.

Ili kukabiliana na hali hiyo mbaya serikali na wahisani wake imeanza kusambaza mahema na mahitaji mengine ili kuwasaidia wale walioathirika.

Jumbe Omari Jumbe msemaji wa shirika la kimataifa la wahamiaji, IOM ambalo linahusika katika usaidizi nchini Msumbiji anazungumzia mafuriko kwenye eneo hilo.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031