Lishe bora ya watoto Syria izingatiwe hata wakati huu wa mzozo: UM

Kusikiliza /

kunyonyesha watoto Syria

Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali yametaka wote wanaohusika na usaizidi wa wasyria waliopotea makazi yao na kukimbilia nchi jirani za Jordan, Lebanon, Iraq na Uturuki kuepusha magonjwa na vifo vya watoto visivyo vya lazima vinavyotokana na kuwapatia watoto wachanga lishe mbadala badala ya maziwa ya mama.

Mashirika hayo UNICEF, UNHCR, WHO, WFP na mashirika yasiyo ya kiserikali yamesema takwimu zinaonyesha kuwa katika hali ya dharura zaidi kama ile inayokumba Syria hivi sasa vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ni kubwa kuliko makundi mengine.

Wamesema hiyo inatokana na watoto wachanga kupatiwa maziwa ya kopo ambayo katika mazingira yasiyo salama yanaweza kusababisha kuhara na vifo.

Mashirika hayo yamesema maziwa ya kopo yatafaa tu pale ambapo kuna hakikisho la mazingira safi na si vinginevyo na kwamba kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa misaada ya maziwa ya kopo, chupa za kunyweshea watoto maziwa haipaswi kuwepo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031