Kitabu cha Annan chamulika changamoto na mafanikio

Kusikiliza /

Kitabu cha Kofi Annan

Masuala ya amani, ulinzi, usalama, uongozi bora na misaada na maendeleo ni miongoni mwa mambo yaliyochukua nafasi katika kitabu kilichoandikwa na Katibu Mkuu  mstaafu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, A Life in War and Peace.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kitabu hicho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani hii leo, Bwana Annan amesema alijisikia kuandika kitabu hicho ili kuonyesha changamoto, mafanikio aliyopata wakati akihudumu nafasi ya Katibu Mkuu.

Amesema kupitia kitabu hicho watu wanaweza kufahamu jinsi Umoja wa Mataifa unavyofanya kazi ikiwemo jitihada za Umoja huo kuleta amani.

"Suala nyingine ambalo nimegusa katika kitabu changu ni bara la Afrika na kazi inayofanywa na UM barani humo. Katika kulinda amani, suala la msaada wa kibindamu, utawala wa sheria na changamoto ambazo tumekuwa nazo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Afrika. Nimeandika pia kuhusu athari zitokanazo na mapambano kwa ajili ya uhuru, juu ya utawala wa sheria."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2015
T N T K J M P
« apr    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031