Jimbo la Equateur, DRC lakumbwa na Surua, 11 wafariki dunia: UNICEF

Kusikiliza /

UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Surua kwenye jimbo la Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Limesema ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe Mosi mwezi huu wagonjwa zaidi ya Mia Moja wamebainika ambapo Kumi na Mmoja wamefariki dunia.

UNICEF imesema kwa kushirkiana na shirika la afya duniani WHO wameandaa vikasha 45 vya dharura vya kinga dhidi ya Surua vitakavyosambazwa kwa kanda 32 za afya zilizokumbwa na ugonjwa huo.

Hata hivyo mashirika hayo yamesema kuna changamoto za kusafirisha vikasha hivyo kutokana na barabara mbovu zinazoelekea kwenye maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031