IOM yatoa ripoti kuhusu usafirishaji binadamu

Kusikiliza /

usafirishaji haramu wa watu

Shirika la Wahamiaji Duniani IOM leo limetoa ripoti yake ya kwanza juu ya mwelekeo wa usafirishaji wa binadamu ambapo inaonyesha kuwa nusu ya visa vilivyoletwa mbele ya shirika hilo kwa ajili ya kupata msaada katika mwaka wa 2011 ni kuhusu dhuluma ya kulazimishwa kufanya kazi.

Kabla ya hapo biashara ya kusafirisha binadamu iligusa zaidi usafirishaji wanawake kwa sababu za ngono ndio.

Ripoti inasema katika kipindi hicho IOM imeweza kusaidia watu 3014. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM:

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Ripoti hii inaonyesha wazi wazi kwamba biashara hii inakuwa na ingawaje Umoja wa Mataifa umetia mkataba huu tunaoita protocol ya Palemo mwaka 2000 bado mataifa mengi hayajaweka mikakati mizuri ya kuweza kupunguza biashara hii. Sasa katika ripoti yetu utaona kwamba mataifa haswa ambayo yameathiriwa zaidi na biashara hii utakuta kwamba ni kama vile Urusi, Haiti, Yemen, Thailand na Kazakhstan.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031