IMF yatabiri ukuaji wa uchumi mwaka 2013

Kusikiliza /

Shirika la fedha duniani IMF limesema kuwa kutakuwepo na ukuaji wa uchumi duniani mwaka huu wa 2013 wakati vizingiti kwenye masuala ya uchumi vinaporegea mwaka huu. Lakini hata hivyo IMF inasema kuwa ukuaji huo utakuwa wa mwendo wa kinyonga ikiongeza kuwa sera ambazo zitatumika ni lazimea zihakikishe kuwepo ukuaji.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa sera zilizotumika zilipunguza msuko suko wa kiuchumi ulioshuhudiwa barani Ulaya na Marekani huku mpango wa Japan ukitarajiwa kuikwamua nchi hiyo kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi lakini iliyo ndogo. Inaongeza kuwa sera hizo pia zimechangia kuinuka kwa masoko hasa kwenye mataifa yanayokua kiuchumi ikitarajiwa kuwa iwapo uchumi utazidi kukua huenda ukafikia viwango ambavyo havikutarajiwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29