Idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati yaongezeka: ILO

Kusikiliza /

wafanyakazi wa kipato cha kati

Shirika la kazi duniani, ILO linasema kuwa idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati kwenye nchi zinazoendelea imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita.

Ripoti ya ILO kuhusu mwelekeo wa ajira kwa mwaka 2013 inasema kuwa kitendo hicho kinaweka mazingira yanayohitajika zaidi kwa ukuaji wa uchumi na ongezeko la matumizi kwenye nchi hizo.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 42 ya wafanyakazi katika nchi hizo wana kipato cha dola Nne kwa kila mwanafamilia kwa siku, zikitaja zaidi maeneo husika kuwa ni nchi za Asia Mashariki.

ILO inakadiria kuwa ifikapo mwaka 2017 idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati kwa nchi zinazoendelea itaongezeka na kufikia Milioni 390.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031