Haki ya kibinadamu Yemeni bado tete

Kusikiliza /

ramani ya Yemen

Kusainiwa kwa mpango wa amani uliokaribisha kipindi cha mpito nchini Yemen kumefungua njia ya kukaribisha huduma za utoaji wa misaada ya kibinadamu ambayo hapo kwanzo ilizorota kutokana na hali mbaya ya kisiasa.

Jarida la masuala ya kibinadamu la Umoja wa Matalifa linasema kuwa mapema mwaka uliopita kulisainiwa makubaliano ya kuwepo kwa kipindi cha mpito kuelekea mwaka 2014 baada ya kuanzishwa majadiliano yalikuwa na shabaha ya kupunguza mvutano wa kisiasa mvutano ambao ulisababisha mamia ya wananchi kwenda kuishi uhamishoni na wengine kukosa makazi.

Hata hivyo pamoja na kuanza kuimarika kwa hali ya amani na utulivu, lakini makadirio yaliyotolewa kuhusiana na hali ya utoaji wa misaada ya kibinadamu katika kipindi cha mwaka 2013 siyo ya kuridhisha.

Umaskini uliokithiri, ukosefu wa chakula na kupanda ovyo kwa bei ya vyakula pamoja na kuwepo kwa ongezeko la gharama za maisha, ni baadhi ya mambo ambayo yanakwamisha ustawi wa wananchi wengi nchini Yemen.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031