Burundi na Uganda zanufaika na msaada wa dharura wa UM

Kusikiliza /

Valerie Amos

Mataifa 12 duniani yakiwemo Sita kutoka Afrika yamepatiwa jumla ya dola Milioni Mia Moja kwa ajili ya misaada ya dharura, taarifa ambazo zimetangazwa leo na Mkuu wa shughuli za usaidizi wa binadamu katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos.

Bi. Amos amesema fedha hizo zimetolewa kuwezesha nchi hizo zikiwemo Burundi, Eritrea, Uganda, Sudan na Liberia kutoa misaada kwa raia wao wenye mahitaji ya dharura. Amesema uteuzi wa nchi hizo ulifanywa na mfuko maalum wa Umoja wa Mataifa unaohusika na dharura, CERF kwa misingi kwamba dharura za nchi hizo zimesahaulika.

Hii ni awamu ya kwanza ay misaada ya dharura kwa maeneo yaliyosahaulika ambapo mathalani Eritrea itapatiwa dola Milioni Tatu kusaidia mipango ya kuokoa maisha huku awamu ya pili ikitarajiwa kutolewa mwezi Julai mwaka huu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031