Bei za vyakula zaendelea kushuka: FAO

Kusikiliza /

vyakula

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema wastani wa bei ya chakula ulishuka kwa asilimia Saba mwezi Disemba mwaka jana na hivyo kufanya bei za vyakula kupungua kwa miezi mitatu mfululizo.

Ripoti ya FAO kuhusu bei ya za chakula inaonyesha bei ya kapu la chakula ilishuka kwa pointi Moja nukta Moja na kuwa pointi 209 kutokana na kushuka kwa bei za nafaka na mafuta katika soko la kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa FAO anayehusika na idara ya uchumi na jamii Jomo Sundaram amesema hali hiyo inabadili mwelekeo wa mwezi Julai ambapo bei za vyakula zilipanda na hata kutia hofu ya uwezekano wa kuwepo kwa uhaba wa chakula.

Amesema uratibu kupitia mabadilishano ya taarifa ya bei za mazao na upatikanaji wa chakula vilisaidia kudhibiti mfumuko wa bei za mazao na kufanya bei za mazao kuwua za chini ikilinganishwa na mwaka 2011.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930