Mashauriano kufanyika kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza /

baraza la usalama

Wakati hali ya usalama ikiendelea kudorora na kutia wasiwasi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baadaye leo litakuwa na mashauriano kuhusu hali ilivyo nchini humo.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA linasema kuwa watu wamekimbia makazi yao ikiwemo mji mkuu Bangui, na kwamba kuna matukio ya uporaji na ghasia.

Halikadhalika inasema watu zaidi ya Laki tatu wanakadiriwa kuishi katika maeneo yenye mzozo nchini humo na Laki Saba wako mjini Bangui.

Ghasia zinazoendelea nchini humo kati ya serikali na waasi wa kikundi cha Seleka zimesababisha vikundi vnavyotoa misaada ya kibinadamu kuondoa kwa muda wafanyakazi wake na hivyo kuathiri mipango ya kusambaza huduma za kibinadamu kwenye maeneo yaliyoathirika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031