Bado tuna wasiwasi mkubwa na hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati: UM

Kusikiliza /

Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali ilivyo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na unaendelea kufanya mawasiliano na mwakilishi maaluma wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa nchini humo Margreth Voght.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo kuwa wakati wanaendelea na mawasiliano hayo umoja wa mataifa unarejelea azimio la Baraza la Usalama la tarehe 27 mwezi uliopita.

"Tunasisitiza azimio la baraza la usalama la terehe 27 mwezi uliopita linalotaka pande zote kujizuia kufanya vitendo vyote vya ghasia dhidi ya raia na kuheshimu haki za binadamu na kutafuta suluhu kwa njia ya amnai. Tunataka serikali na waasi kujikita katika mashauriano yatakayo epusha mzozo na kuwezesha suluhisho la amani na kuheshimuwa pia makubaliano ya kina ya Brazaville."

Halikadhalika amesema kwa nia ya kujihadhari wafanyakazi wa kimataifa wote wamehamishwa kwa muda nchini humo wakati huu ambapo mashaurino ya kuleta amani yakiendelea.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031