Baadhi ya sheria zinasababisha maambukizi mapya ya HIV: Rao

Kusikiliza /

Prasad Rao

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Ukimwi kwa nchi za Asia na Pasifiki, Prasad Rao amesema baadhi ya sheria zinazofuatwa nchini humo zimesababisha kuwepo kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi licha ya mafanikio ya kudhibiti ugonjwa huo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Bwana Rao amesema kitendo cha kutambua uhusiano wa jinsia moja, kubadilisha jinsia kuwa ni uhalifu vinasababisha mambo hayo kufanyika gizani na mikakati ya kinga dhidi ya Ukimwi kushindwa kuwafikia wahusika hao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930