Amani yazidi kusakwa Syria, IOM yaomba msaada zaidi

Kusikiliza /

wakimbizi wa Syria

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakdhar Brahimi, Ijumaa atakuwa na mazungumzo na viongozi wa Urusi na Marekani kwa lengo la kupatia suluhu la kisiasa mzozo unaoendelea nchini Syria.

Habari zinasema kuwa mazungumzo hayo baina ya Brahimi na Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov na yule wa Marekani William Burns yanatarajiwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi.

Wakati huo huo Shirika la uhamiaji duniani, IOM limesema linahitaji dola Milioni 36 kwa ajili ya kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu huko Syria na nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi wa nchi hiyo. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031