Nyumbani » 30/01/2013 Entries posted on “Januari 30th, 2013”

Brahimi ataja vikwazo vya utatuzi wa mgogoro wa Syria

Kusikiliza / Lakdhar Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi amesema kitendo cha pande mbili kwenye mzozo huo kutozungumza kabisa kinafanya utatuzi kuwa mgumu. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani, Brahimi amesema kila upande ina mtazamo wake [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO kuisaidia Mali kukarabati na kuokoa maeneo ya urithi wa dunia

Kusikiliza / Eneo la urithi wa dunia, Timbuktu, Mali

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokova, ametangaza kuwa shirika hilo litaisaidia nchi ya Mali kukarabati na kurejesha maeneo yake ya urithi wa kiasili, ambayo ameyataja kuwa sehemu muhimu ya historia na utamaduni wa nchi hiyo. Bi Bokova ametoa wito kwa wadau wote wa UNESCO kuunga mkono juhudi za ukarabati [...]

30/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kujadili umuhimu wa uongozi wa kisheria

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili umuhimu wa kuimarisha uongozi wa kisheria kama njia ya kuendeleza amani na usalama wa kimataifa. Akilihutubia Baraza hilo wakati wa kufungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amesema kuhakikisha haki na usalama kupitia uongozi wa kisheria ni njia mwafaka ya [...]

30/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu Ulaya wanakata tamaa kufuatia mdororo wa kiuchumi: IFRC

Kusikiliza / nembo ya IFRC

Wakati bara la Ulaya likiwa bado linakumbwa na mdororo wa kiuchumi, Shirikisho la mashirika ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC) limeonya kuwa mamilioni ya watu ambao wameathiriwa na ukosefu wa ajira, ongezeko la umaskini, kupoteza makazi na hali ya sintofahamu kuhusu hatma yao huenda wakakata tamaa. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zaidi [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Athari za kimbunga Msumbiji, mama ajifungulia juu ya paa: OCHA

Kusikiliza / mafuriko Mozambique

Kimbunga Felling kimezidi kusababisha madhara huko Msumbiji wakati huu inapotolewa hadhari kuwa kinasonga kaskazini ambapo licha ya zaidi ya watu 48 kupoteza maisha na nyumba kuharibiwa za wakazi 250,000, mwanamke mmoja mjamzito amejikuta akijifungulia juu ya paa la nyumba. Mama huyo aliyetambulika kwa jina la Hortensia ni mkazi wa wilaya ya Chokwe nchini Msumbiji, moja [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ongezeko la wanaouawa na askari wa Israel latia wasiwasi UM

Kusikiliza / Israel

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa  James W. Rawley ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongeza kwa watu wanaouawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan. Imeripotiwa kuwa tangu mwezi Novemba mwaka jana raia wanane wa kipalestina wakiwemo watoto watatu na mwanamke mmoja wameuawa katika visa tofauti [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumieni mkutano kuonyesha mnawajali raia wa Syria: Amos

Kusikiliza / Syria OCHA

Mkuu wa shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, Valerie Amos amewasihi washiriki wa mkutao wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait kutumia fursa ya mkutano huo kuonyesha kuwa wanajali na kushirikiana kuwasaidia wananchi wa Syria. Bi. Amos amesema mahitaji nchini Syria ni makubwa. Ametoa mfano kuwa nusu ya [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukata wa bajeti usikwamishe mchango kwa Syria: Ban

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa UM.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika mkutano wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait na kusema kuwa mazingira magumu yanayokumba wasyria hayawezi kuachwa yaendelee licha ya kwamba serikali mbali mbali duniani zinakumbwa na ukata. Amesema anatambua hali ngumu ya uchumi lakini ombi la dharura la dola Bilioni Moja na Nusu [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031