Nyumbani » 29/01/2013 Entries posted on “Januari 29th, 2013”

Utata uliopandikizwa kwenye tamko la Geneva juu ya Syria uondolewe: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi amelieza Baraza la Usalama kuwa hali ya Syria ni mbaya na kwamba anaona aibu vile ambavyo kila wakati amekuwa akirejea kauli hiyo bila hatua dhahiri kuchukuliwa. Bwana Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari [...]

29/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaimarisha usaidizi wake kwa watoto huko CAR

Kusikiliza / Watoto Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaimarisha operesheni zake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia maelfu ya watoto wanaohitaji misaada ya dharura baada ya kujikuta katikati ya mzozo unaoendelea hivi sasa nchini humo. Mwakilishi wa UNICEF nchini huko Souleyman Diabate amesema wamebaini maeneo ambako watoto wameathirika zaidi ni pamoja na [...]

29/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM laahidi kuwaunga mkono wananchi wa Haiti

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamewahakikishia wananchi wa Haiti kwamba jamii ya kimataifa imejitolea kuunga mkono jitihada zao za kutafuta amani , uthabiti pamoja na maendeleo. Hii ni kupitia taarifa iliyotolewa na Rais wa baraza hilo Masood Khan inayojiri baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mwakilishi mkuu wa katibu mkuu wa [...]

29/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

29/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNHCR yajiandaa kuwasaidia walio na nia ya kurejea makwao nchini Mali

Kusikiliza / mtoto wa Mali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linajianda kuwasaidia wale waliohama makwao kaskazini mwa nchi na walio na nia ya kurejea kwa hiari wakati hali inapoendelea kubadilika nchini Mali. UNHCR inasema kuwa ina mpango wa kufungua ofisi zake mjini Gao na kwenye miji mingine eneo la kaskazini hivi karibuni hata kama [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Libya bado si nzuri: Mitri

Kusikiliza / Tarek Mitri

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Tarek Mitri amelihutubia Baraza la Usalama hii leo mjini New York, Marekani na kueleza kuwa hali ya usalama nchini Libya bado ni mbaya na jitihada za kuimarisha usalama zinaendelea. Bwana Mitri amesema licha ya kuwepo kwa maendeleo thabiti katika baadhi ya sekta ikiwemo kurejesha [...]

29/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO yaonya uwezekano wa kutokea tena homa ya mafua ya ndege

Kusikiliza / homa ya mafua ya ndege

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya juu ya kitisho cha kuzuka tena ugonjwa wa mafua ya ndege ulioikumba dunia mwaka 2006 na limetaka kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kudhibiti kutojirejea kwa hali hiyo. FAO imesema kuwa wakati dunia ikiendelea kuhangaika na mikwamo ya kiuchumi, kuna kiasi kidogo cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya kushughulikia kutojitokeza [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yarejesha huduma za usambazaji wa chakula mjini Kismayo

Kusikiliza / wfp food sacks

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza tena usambazaji wa msaada wa chakula kwenye mji wa Kismayo ulio kusini mwa Somalia ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita. Mizozo pamoja na ukosefu wa usalama vimekuwa vikiizuia WFP na mashirika kadhaa ya kutoa misaada ya kibinadamu kufanya kazi katika eneo [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lishe bora ya watoto Syria izingatiwe hata wakati huu wa mzozo: UM

Kusikiliza / kunyonyesha watoto Syria

Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali yametaka wote wanaohusika na usaizidi wa wasyria waliopotea makazi yao na kukimbilia nchi jirani za Jordan, Lebanon, Iraq na Uturuki kuepusha magonjwa na vifo vya watoto visivyo vya lazima vinavyotokana na kuwapatia watoto wachanga lishe mbadala badala ya maziwa ya mama. Mashirika [...]

29/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awasili Kuwait, atoa shukrani kwa maandalizi ya mkutano wa Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko nchini Kuwait tayari kushiriki mkutano wa wahisani kwa ajili ya Syria hapo kesho. Tayari Bwana Ban amekuw ana mazungumzo na viongozi wa wa nchi hiyo akiwemo Mfalme wa nchi hiyo, Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Mambo ya Nje. Katika mazungumzo yao pamoja na [...]

29/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka majadiliano ya dhati Misri ili kuepusha maafa zaidi

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navyi Pillay amesema kumekuwa na hali ya wasiwasi kufuatia kuongezeka kwa matukio ya mauaji ya watu na kushamiri kwa vurugu kunakoshuhudiwa sasa nchini Misri na amezita pande zote kuanzisha majadiliano ili kuondokana na hali hiyo. Pia Pillay ameitolea wito serikali ya Misri kutafakari upya njia [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Askari waripotiwa kunyanyasa raia huko Kivu Kaskazini

DRC kivu

Usalama wa raia kwenye jimbo la Kivu Kaskazini huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC bado ni wasiwasi mkubwa ambapo raia wanakumbwa na manyanyaso kutoka kwa askari. Jarida la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa limewakariri wataalamu wa elimu na ulinzi wa mtoto wakitaja manyanyaso hayo kuwa ni pamoja na zaidi ya [...]

29/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jimbo la Equateur, DRC lakumbwa na Surua, 11 wafariki dunia: UNICEF

Kusikiliza / UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Surua kwenye jimbo la Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Limesema ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe Mosi mwezi huu wagonjwa zaidi ya Mia Moja wamebainika ambapo Kumi na Mmoja wamefariki dunia. UNICEF imesema kwa kushirkiana na shirika la afya duniani [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031