Nyumbani » 28/01/2013 Entries posted on “Januari 28th, 2013”

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

  Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule. Maelfu ya watu kwa sasa hawana makazi na wanahitaji msaada ambapo shrika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na idara ya ulinzi wa raia nchini Zimbabwe wameitikia wito wa kutoa [...]

28/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Bado hatujaweza kufikia maeneo yote Syria: OCHA

Kusikiliza / John Ging, Mkuu wa Operesheni- OCHA

Mkuu wa operesheni katika Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu,  OCHA, John Ging amesema hali  ya Syria bado inazidi kudorora kadri siku zinavyosonga na kwamba bado hawajapata kibali cha kuweza kuvuka eneo la mzozo na kuwafikia awle wote wanaohitaji misaada. Bwana Ging amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kuwa wakati [...]

28/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Marais na wanasoka wapaza sauti dhidi ya Malaria

Kusikiliza / CAF- Malaria

Afrika Kusini, mwenyeji wa mwaka huu wa fainali za kombe la mataifa barani AFrika, AFCON. Wakati wachezaji wakipasha misuli yao kulinda nyavu zao, mbu nao wanavinjari kwa lengo la kuwamaliza nguvu.. Malaria na ndio maana Mpango wa kudhibiti Malaria na kampeni ya pamoja dhidi ya Malaria wametoa ujumbe huu mahsusi kwa lengo la kutokomeza Malaria!

28/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wajawazito waona mwanga Somalia

Kusikiliza / akina mama wajawazito

Taifa la Somalia linazidi kuimarika kila uchwao baada ya kuundwa kwa serikali mwaka jana. Huduma za kijamii ikiwemo za kiafya zinazidi kuimarika. Hii imewezesha hata wajawazito ambao awali walikuwa wanajifungulia majumbani, kupata huduma hizo kwenye hospitali chini ya uangalizi wa madaktari, wauguzi na wakunga wenye uzoefu an vifaa. Kitendo hiki kinaokoa siyo tu maisha ya [...]

28/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

28/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa WHO afariki dunia

hiroshi-nakajima

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Dkt. Hiroshi Nakajima amefariki dunia nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa muda mfupi.Alikuwa na umri wa miaka 84. Taarifa za kifo hicho zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa WHO Dr. Margaret Chan ambaye amemwelezea Nakajima kama mtu aliyojitoa kwa dhati na kulitumikia shirika hilo kwa [...]

28/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mafuriko Msumbiji yasababisha wengi kukosa makazi

Kusikiliza / waathiriwa wa mafuriko Mozambique

Serikali ya Msumbiji kwa kushirikiana na mashirika ya misaada imeanzisha juhudi za kuwanusuru mamia ya wananchi ambao wameathiriwa kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba taifa hilo. Kiasi cha watu 150,000 wanahitaji msaada wa dharura baada ya makazi yao kuharibiwa na mafuriko yaliyotokea katika jimbo la Gaza, lililoko kusini mwa nchi hiyo. Mamia ya manusura wa mafuriko [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KASMO FM mkombozi wa wanawake Somalia

Kusikiliza / KASMO

Kwa mara ya kwanza Somalia inapata kituo cha Radio kinachosimamiwa na kuendeshwa na wanawake, KASMO FM. Radio hiyo itazinduliwa rasmi mjini Mogadishu, Somalia tarehe Tatu mwezi Machi mwaka huu ambayo ni siku ya wanawake duniani na kuanzishwa kwake kunatokana na msaada wa UNESCO. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu wa UM asikitishwa na vifo vya vijana kwenye klabu: Brazil

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kuhuzunishwa kwake na vifo vya mamia ya vijana vilivyotokea kwenye klabu moja ya usiku kwenye mji wa Santa Maria, Rio Grande do Sul nchini Brazili. Bwana Ban amekaririwa akieleza kushtushwa zaidi na vifo hivyo kwa kuwa vimehusisha vijana ikiwemo wanafunzi vya vyuo vikuu ambao wamekufa kutokana [...]

28/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu Syria yazidi kudorora

Kusikiliza / baridi, Syria

Umoja wa Mataifa unasema hali ya kibinadamu nchini Syria inazidi kudorora kila uchwao ambapo watu Milioni Nne wanahitaji msaada wa kibinadamu. Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema baridi kali imeongeza madhila ya watu hususan wale waliohama makwao kutokana na mgogoro unaoendelea nchini mwao na sasa wanaishi kwenye makazi ya [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna maendeleo endelevu kama kuna njaa: FAO

Kusikiliza / Graziano Da Silva

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO Graziano Da Silva anasema kuwa hakutakuwepo na maendeleo ya kudumu duniani ikiwa watu wataendela kuhangaishwa na njaa. Akizungumza kwenye mkutano wa jumuia ya nchi za Amerika kusini, Carribean na Ulaya, Da Silva amesema kuwa mataifa sasa yana fursa ya kutoa mapendekezo kuhusu [...]

28/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa yaomba dola milioni 471 kwa ajili ya Afghanistan

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Afghanistan

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa watoto 165 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakufa kila siku huku mama mjamzito mmoja akifariki dunia kila baada ya saa mbili nchini Afhanistan. Taarifa hiyo ya OCHA inalenga kuonyesha jinsi hali ya kibinadamu inavyozidi kuzorota nchini Afghanistan. Inaongeza kuwa [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Somalia, DRC, Madagascar, Zimbabwe zamulikwa huko Addis Ababa

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Afrika ambapo wamefanya mashauriano kuhusu masuala kadhaa ikiwemo yua kiuchumi, kisiasa na kijamii. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. Miongoni mwa viongozi aliokutana nao Bwana Ban ni Paul Kagame wa Rwanda ambapo wamejadili hali ya usalama katika nchi za Maziwa Makuu na amepongeza Rwanda [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bara la Afrika linasonga mbele: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono maendeleo barani Afrika ikiwemo masuala ya utawala bora na haki za binadamu ambapo amesema mtazamo wake ni kwamba bara hilo linaibuka na kusonga mbele. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, Ethiopia, Bwana Ban ametoa mfano wa harakati za Afrika za kupambana na magonjwa [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930