Nyumbani » 24/01/2013 Entries posted on “Januari 24th, 2013”

Ban awapa hongera Wamisri kwa miaka miwili tangu mapinduzi

Kusikiliza / Waandamanaji Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amepeleka salamu za heko kwa raia wa Misri, wakati wakiadhimisha miaka miwili tangu mapinduzi yaloing'oa serikali ya Hosni Mubarak mamlakani.  Bwana Ban ameelezea kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kuwaunga mkono watu wa Misri na serikali yao kujenga mifumo ya kidemokrasia inayowahusisha wote. Amewahimiza waendelee kushabikia kanuni za [...]

24/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Ban huko CAR azungumzia azimio la Baraza la Usalama.

Kusikiliza / Margaret Voght, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM huko CAR na Mkuu wa BINUCA

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Margaret Vogt amezungumza na waandishi wa habari kwa nchi ya video kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bangui na kusifu azimio la Baraza la Usalama ambalo amesema linasisitiza umuhimu wa ofisi yake kutoa usaidizi wa utekelezaji wa makubaliano ya Libreville. [...]

24/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa ofisi yake huko CAR

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa ofisi yake ya ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, BINUCA huku ikitaka serikali na vikundi vya upinzani kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na mengineyo yenye lengo la kurejesha amani nchini humo. BINUCA imeongezewa muda hadi tarehe 31 mwezi Januari mwakani ambapo kupitia [...]

24/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mali na Syria zatawala hotuba ya Ban huko Davos

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Hali ya amani nchini Mali na Syria zinazidi kuzorota na hivyo tuchukue hatua haraka kwa pamoja, na huo ndio ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa viongozi mbali mbali wa dunia wanaohudhuria jukwaa la uchumi huko Davos Uswisi. Katika hotuba yake Ban amesema migogoro hiyo inahatarisha usalama siyo tu wa nchi [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Raila Odinga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi huko Davos, Uswisi. Bwana Ban na Bwana Odinga wamezungumza kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Kenya ujao mwaka huu, pamoja na haja ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IMF yatabiri ukuaji wa uchumi mwaka 2013

Kusikiliza / construction-worker

Shirika la fedha duniani IMF limesema kuwa kutakuwepo na ukuaji wa uchumi duniani mwaka huu wa 2013 wakati vizingiti kwenye masuala ya uchumi vinaporegea mwaka huu. Lakini hata hivyo IMF inasema kuwa ukuaji huo utakuwa wa mwendo wa kinyonga ikiongeza kuwa sera ambazo zitatumika ni lazimea zihakikishe kuwepo ukuaji. Ripoti hiyo inaeleza kuwa sera zilizotumika [...]

24/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yatoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa Global Fund

Kusikiliza / Global-Fund

Jamhuri ya Ujerumani imetoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa kimataifa wa kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria, yaani Global Fund, ili kuwasaidia wahudumu wa afya kuendeleza juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa haya hatari ya kuambukiza. Tangazo la mchango huo limetolewa leo na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban afanya mashauriano na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Bwana Ahmet Davutoğlu mjini Davos, Uswisi, ambako kongamano la kimataifa kuhusu uchumi linaendelea. Bwana Ban na Waziri Davutoğlu wamebadilishana mawazo kuhusu mzozo wa Syria, na uwezekano wa suluhu la kisiasa. Katibu Mkuu ameelezea shukran [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yazindua ukusanyaji maoni kupitia mtandao wa Intaneti

Kusikiliza / UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na UKIMWI, UNAIDS, limefungua ukurasa huru wa mawasiliano ya kimtandao kwa shabaha ya kukusanya maoni toka pande zote za dunia, mawazo ambayo yatatumika kuratibu njia mpya za kukabiliana na tatizo la UKIMWI duniani. Zoezi hili la kukusanya maoni kwenye intaneti litaendeshwa kwa muda wa wiki mbili, na kukamilika mnamo [...]

24/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa ufadhili wa Marekani kwa UNICEF watoa ombi la msaada kwa watoto wa Syria

Kusikiliza / watoto, Syria

Mfuko wa ufadhili wa serikali ya Marekani kwa Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, umetoa ombi la msaada wa dharura kwa watoto wa Syria, ambao wameathiriwa na mapigano na msimu wa baridi. Ripoti za hivi karibuni zimeelezea jinsi watoto wa Syria wanavyoathirika zaidi na mzozo huo. Miongoni mwa takriban watu milioni mbili [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaungana na wadau kuzindua mkakati wa ‘lisha mwili, lisha ubongo”

Kusikiliza / nourishing

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuanzia lile linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la kuhudumia watoto UNICEF, yamekusanya nguvu kwa pamoja ili kuwasaidia mamia ya watoto wanaokabiliwa na hali ngumu. Mpango huo wa miaka mitatu uliotangazwa kwenye kongamano la kitamaifa la uchumi linalofanyika Davos, Uswis [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya fidia ya UM yatoa dola bilioni 1.3 kwa taifa la Kuwait

Kusikiliza / mafuta yaliyochomwa

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya fidia imewasilisha jumla ya dola bilioni 1.3 kwa serikali ya Kuwait. Fedha hizo ambazo ni deni zinafikisha jumla ya dola bilioni 40.1 ambazo zimelipwa na tume hiyo zikiwa ni kati ya dola bilioni 52.4 zilizolipwa kwa zaidi ya serikali 100 na mshirika ya kimataifa na ambazo [...]

24/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031