Nyumbani » 23/01/2013 Entries posted on “Januari 23rd, 2013”

MONUSCO yasifu uamuzi wa Rwanda kukubali matumizi ya ndege zisizo na rubani

Kusikiliza / Madnodje Mounoubai

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC (MONUSCO) umepongeza uamuzi wa Rwanda wa kuungana na Uganda na DRC juu ya matumizi ya ndege zisizo na rubani mpakani mwa nchi hizo tatu. Msemaji wa MONUSCO, Madnodje Mounoubai amesema kufuatia makubaliano hayo anatumai kutakuwepo na maendeleo. Amesema mapendekezo ya [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani kufungwa kwa Mhariri Thailand

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu Navy Pillay amelaani vikali hukumu iliyotolewa kwa mhariri na mwanaharakati wa haki za binadamu Somyot Pruksakasemsuk nchini Thailand, akisema kuwa hukumu hiyo ni ya kuudhi, katili na inakwaza juhudi za utetezi wa haki za binadamu katika nchi hiyo. Mamlaka ya Thailand imemhukumu mhariri huyo [...]

23/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji wa kimataifa kupanda 2013 na 2014: UNCTAD

Kusikiliza / unctad_logo_copy

Uwekazaji wa kimataifa wa moja kwa moja ulishuka kwa asilimia 18 mwaka 2012 sawia na kiwango kilichoshuhudiwa mwaka 2009 hali ambayo inachangiawa zaidi kutokana na kutokuwepo uhakika miongoni mwa wawekezaji. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD. Hata hivyo uwekezaji wa kimataifa unatarajiwa kuongezeka mwaka [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati yaongezeka: ILO

Kusikiliza / wafanyakazi wa kipato cha kati

Shirika la kazi duniani, ILO linasema kuwa idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati kwenye nchi zinazoendelea imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita. Ripoti ya ILO kuhusu mwelekeo wa ajira kwa mwaka 2013 inasema kuwa kitendo hicho kinaweka mazingira yanayohitajika zaidi kwa ukuaji wa uchumi na ongezeko la matumizi kwenye nchi hizo. Takwimu [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sioni mwelekeo wa dhati huko Mashariki ya Kati: Serry

Kusikiliza / Robert Serry

Mratibu maalum wa Umoja wa Taifa katika mchakato wa amani huko Mashariki ya Kati, Robert Serry ameeleza wasiwasi wake juu ya kukosekana kwa mwelekeo wa dhati na bayana wa mchakato wa amani mashariki ya kati baina ya Israeli na Palestina. Bwana Serry ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu amesema hayo katika taarifa yake [...]

23/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wabunge wa nchi za makuu wajadili amani kwenye ukanda wao

Kusikiliza / Baadhi ya maspika wa mabunge ya nchi za Maziwa Makuu

Mkutano wa tatu wa wabunge wa nchi za maziwa makuu umeanza leo huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC ambapo washiriki kutoka nchi 12 za maziwa makuu wanataka kuwepo kwa amani ya kudumu kwenye maeneo ya migogoro ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mashariki mwa DRC, na baina ya Sudan na Sudan Kusini. Katibu [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta ya Kilimo Syria taabani: UM

Kusikiliza / ukulima, Syria

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokwenda Syria kujionea hali halisi umeeleza kuwa mapigano yanayoendelea nchini humo yameathiri uzalishaji wa kilimo na hivyo msaada zaidi unahitajika maeneo ya vijijini. Miongoni mwa waliokuwemo kwenye ujumbe huo ni Mkurugenzi wa idara ya dharura na ukarabati kutoka shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO, Dominique Burgeon [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya chakula Myanmar shwari isipokuwa maeneo yaliyokumbwa na mikasa

Kusikiliza / myanmar map

Umoja wa Mataifa unasema kuwa hali ya chakula nchini Myanmar imeimarika isipokuwa katika maeneo yaliyokumbwa na madhila ya mafuriko na mapigano ya kikabila mwaka jana. Jarida la taarifa za hali ya kibinadamu linasema kuwa maeneo hayo ya Rakhine, Kachin na Shan Kaskazini yana maelfu ya watu waliopoteza makazi kutokana na madhila hayo mwezi Juni na [...]

23/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya ya WHO yaonyesha uhaba wa huduma za afya Syria

Kusikiliza / unhcr-syria

Sita kati ya kila hospitali kumi na tatu, ikiwemo hospitali kuu ya umma katika jimbo la Homs nchini Syria, hazina huduma za matibabu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya hali ya afya katika muktadha wa mzozo nchini humo, ambayo imetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO. Ili kuwezesha huduma za afya, shirika la [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031