Nyumbani » 22/01/2013 Entries posted on “Januari 22nd, 2013”

AFISMA wanahitaji vifaa haraka: Feltman

Kusikiliza / Msimamizi mkuu wa masuala ya siasa ndani ya UM, Jeffrey Feltman

Msimamizi mkuu wa masuala ya kisiasa ndani ya Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amesema kwa kuwa tayari maafisa na askari wanaounda jeshi la Afrika huko Mali, AFISMA  wameanza kuwasili nchini humo, kinachotakiwa hivi sasa ni usaidizi haraka wa vifaa ili waweze kukabiliana na hali halisi. Feltman amesema hayo wakati akitoa taarifa ya  hali ilivyo huko [...]

22/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza lapitisha azimio dhidi ya DPRK, Ban aunga mkono

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio la kushutumu vikali kitendo cha Jamhuri ya kidemokrasia yaWatu wa Korea, DPRK cha kurusha roketi kwa kutumia teknolojia ya makombora ya masafa marefu mwezi Disemba mwaka jana. Azimio hilo namba 2087 limepitishwa Jumanne baada ya mjadala wa wazi ambapo wajumbe wote wamesisitiza msimamo [...]

22/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utupaji na upotevu wa chakula sasa basi: UM

Kusikiliza / food 2

Katika harakati za kuona kuna uhakika wa chakula duniani, kampeni mpya imeanzishwa kuepusha upoteaji au utupaji wa chakula. Kampeni hiyo inayoendeshwa na shirika la chakula na Kilimo duniani, FAO na lile la mazingira, UNEP kwa kushirikiana na wadau wao inazingatia kuwa maelfu ya Tani za chakula hupotea na kusababisha hasara ya dola Trilioni Moja. Je [...]

22/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Marais na wanasoka wapaza sauti dhidi ya Malaria

Kusikiliza / CAF- Malaria

Afrika Kusini, mwenyeji wa mwaka huu wa fainali za kombe la mataifa barani AFrika, AFCON. Wakati wachezaji wakipasha misuli yao kulinda nyavu zao, mbu nao wanavinjari kwa lengo la kuwamaliza nguvu.. Malaria na ndio maana Mpango wa kudhibiti Malaria na kampeni ya pamoja dhidi ya Malaria wametoa ujumbe huu mahsusi kwa lengo la kutokomeza Malaria!

22/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aorodhesha mambo ya kipaumbele katika ajenda ya mwaka 2013

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ameliambia Baraza Kuu la Umoja huo kwamba, masuluhu ya kudumu kwa matatizo ya dunia hayawezi kamwe kuachwa katika mikono ya serikali pekee, na kwamba Umoja wa Mataifa katika karne ya 21 ni lazima uangazie mitandao na ushirikiano. Bwana Ban amesema maamuzi yanayofanyika au kushindwa kufanyika katika [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola Milioni 303 kwa mwaka 2013

Kusikiliza / Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Uhamiaji IOM limetangaza mahitaji ya dola za kimarekani Milioni 303 kwa ajili ya kugharimia miradi ya misaada ya kibinadamu kwa kipindi cha mwaka huu 2013. Miradi hiyo usamaria wema iliyopangwa kutekelezwa na IOM miongoni mwake ni ile iliyoanzishwa mwaka uliopita wa 2012 na inatekelezwa katika nchi 16 ikiwemo [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utupaji chakula umekithiri: UM

Kusikiliza / utupaji chakula umekithiri

Shirika la chakula na Kilimo duniani, FAO na lile la mazingira, UNEP kwa kushirikiana na wadau wao wamezindua kampeni ya kuokoa maelfu ya Tani za chakula kinachopotea na kusababisha hasara ya dola Trilioni Moja, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutokomeza njaa duniani. Kampeni hiyo inaitwa [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za binadamu imesikitishwa na kunyongwa kwa kijana nchini Iran

Kusikiliza / humanrightsoffice

Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imesema kuwa umevunjwa moyo kutokana na ripoti za kunyongwa kwa kijana mmoja wa Ki-iran, aliyenyongwa January 16 mwaka huu baada ya kupatikana na hatia. Kijana huyo Ali Naderi alitiwa hatiana na kuamuliwa kunyongwa hadi kufa kutokana na kosa alilolitenda wakati akiwa na umri wa miaka [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila yanayowakumba wakimbizi wa Syria yaongezeka: OCHA

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Ziara ya siku nne ya ujumbe wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA huko Syria imeibua madhila zaidi yanayowakumba wakimbizi ikiwemo kukosa huduma za msingi kama vile afya, chakula na elimu kwa watoto. Msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema ujumbe huo ukimjumuisha pia Mkuu wa OCHA John Ging, uliweza kutembelea [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapitisha azimio kuimarisha ulinzi wa amani

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio ambalo kwalo operesheni za ulinzi wa amani zitaweka msingi wa amani ya kudumu kwenye mataifa ambayo yanakumbwa na mizozo. Azimio hilo namba 2086 lilipitishwa baada ya mjadala wa siku nzima ambapo linaeleza kuwa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zinastahili kuendeshwa kwa njia ambayo [...]

22/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Mali wakumbwa na uhaba wa chakula: UNHCR

Kusikiliza / Nyakabande

Wakati mashambulizi ya angani na mapigano yanapoendelea nchini Mali, wakimbizi nao wanazidi kuvuka mipaka na kuingia nchi jirani. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa Mauritania imepokea wakimbizi 4,208 kutoka Mali tangu tarehe 11 mwezi huu ambao kwa sasa wanahamishwa kwenda kambi ya wakimbizi ya Mbera ambayo tayari inawahifadhi wakimbizi 55,221. [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

22/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031