Nyumbani » 21/01/2013 Entries posted on “Januari 21st, 2013”

Ukosefu wa sifa zinazotakiwa wakosesha wengi ajira: ILO

Kusikiliza / ILO_logo

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO kuhusu mwelekeo wa ajira inaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu wasio na ajira duniani mwaka jana licha ya kupungua miaka miwili iliyotangulia. Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Rider akizindua ripoti hiyo huko Geneva, Uswisi amesema mwaka jana kulikuwepo na watu wapya Milioni Nne nukta Mbili wasio na [...]

21/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Burundi na Uganda zanufaika na msaada wa dharura wa UM

Kusikiliza / Valerie Amos

Mataifa 12 duniani yakiwemo Sita kutoka Afrika yamepatiwa jumla ya dola Milioni Mia Moja kwa ajili ya misaada ya dharura, taarifa ambazo zimetangazwa leo na Mkuu wa shughuli za usaidizi wa binadamu katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos. Bi. Amos amesema fedha hizo zimetolewa kuwezesha nchi hizo zikiwemo Burundi, Eritrea, Uganda, Sudan na Liberia kutoa [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waonya kuhusu kuajiri watoto katika vita Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na vita vya silaha, Bi Leila Zerrougui, ameelezea kusikitishwa kwake na ripoti za hivi karibuni kuhusu kuajiriwa kwa watoto na makundi yenye silaha yanayojumuisha muungano wa waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Akilihutubia Kundi la kuchukua hatua la Baraza la Usalama la Umoja wa [...]

21/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaoingia Jordan yaongezeka: IOM

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM  limesema kuwa wakimbizi wanaokimbia machafuko Syria kuelekea Jordan wanaendelea kuongezeka.  Jumbe Omar Jumbe, ambae ni msemaji wa IOM, amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo.

21/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha hatua ya Myanmar ya kusitisha mapigano kwenye jimbo la Kachin

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la hivi majuzi la serikali ya Mynamar la kusitisha mapigano kwenye jimbo lililo kakazini la Kachin. Kupitia msemaji wake Ban ametoa wito kwa pande zote kufanya juhudi za kuleta utulivu kwenye jimbo la Kachin hasa kupitia mazungumzo. Ban pia ametoa wito wa kutolewa nafasi ya [...]

21/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa UM kuhusu ubaguzi wa rangi azuru Uhispania

Kusikiliza / Mutuma Ruteere

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi Mutuma Ruteere ameanza ziara ya juma moja nchini Uhispania ambapo anatarajiwa kukutana na waakilishi wa serikali , wabunge , mahakama, Ombudsman, mashirika yasiyokuwa ya serikali pamoja na makundi yanayofanya kazi kwneye nyanja za ubaguzi wa tangi. Ruteere tayari ashakutana na Waziri wa masuala ya kigeni [...]

21/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMID yasambaza misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Darfur

Kusikiliza / UNAMID yasambaza misaada Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Darfur nchini Sudan, UNAMID umesambaza misaada ya dharura kwa mamia ya raia wanaoteseka katika eneo la Kaskazini mwa Darfur na maeneo mengine ya jirani. Katika awamu yake ya kwanza, UNAMID ambayo imetumia njia ya anga na barabara, imesambaza kiasi cha kilo [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Operesheni za ulinzi wa amani kuimarishwa: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu operesheni za kulinda amani za Umoja huo kwenye maeneo mbali mbali duniani ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema watakuwa wanafanya tathmini ya operesheni hizo ili kuhakikisha zina uwezo na stadi za kuwezesha kustahimili mazingira yanayoibuka wakati wa utendaji wao. Katika hotuba [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo vya mateka Algeria yapanda hadi 57

Kusikiliza / Baraza la Usalama lajadili suala la Algeria

Idadi ya watu walio fariki dunia kufuatia tukio la siku nne la utekaji nyara katika kiwanda cha gesi cha Amenas nchini Algeria imepanda na kufika 57. Yapata watu 9 raia wa Japan wameripotiwa kuuawa, huku miili ya watu wengine 25 waliokuwa wametekwa nyara ikigunduliwa na vikosi vya Algeria. Awali mwishoni mwa wiki, Baraza la Usalama [...]

21/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Changamoto za kiafya ni nyingi, lakini zinaweza kukabiliwa: WHO

Kusikiliza / Margaret Chan

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Bi Margaret Chan, amesema kuwa nia ya kuondoa machungu kwa mwanadamu ni thabiti, lakini makali yake huathiriwa na uhaba wa rasilmali, uwezo mdogo na misaada mingi isokuwa na utaratibu mzuri. Akihutubia kikao cha 132 cha halmashauri kuu ya WHO, Bi Chan amesema shirika hilo linahudumu katika mazingira [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la nyuklia Iran, IAEA yazuiwa kuingia Parchin

Kusikiliza / nembo ya IAEA

Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA limesema mazungumzo ya siku mbili kati yake na serikali ya Iran kuhusu mpango wa nyuklia wan chi hiyo hayakuweza kumaliza tofauti kati ya pande mbili hizo. Naibu mkurugenzi Mkuu wa IAEA kuhusu mipango ya ulinzi salama Herman Nackaerts amesema mazungumzo yaliyofanyika Tehran yalikuwa ya kina [...]

21/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Sudan, waasi wa JEM waanza tena mazungumzo Doha

Kusikiliza / Aichatou Mindaoudou

Serikali ya Sudan na waasi wa kundi JEM wameanza tena mazungumzo huko Doha, Qatar ya kumaliza mzozo baina yao huku pande zote zikiahidi kuheshimu majadiliano hayo. Mazungumzo hayo yanafanyika chini ya usimamizi wa Naibu Waziri Mkuu wa Qatar Ahmed Bin Abdullah Al-Mahmoud, na Kaimu Mkuu ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaoingia Jordan yaongezeka

Kusikiliza / kambi iliyoko Jordan

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali ya wakimbizi wa Syria inazidi kuwa mbaya ambapo idadi yao wanaowasili Jordan kwa muda siku imeongezeka maradufu.   UNHCR imesema kwa sasa inapokea wakimbizi 730 kwa siku tofauti na awali ambapo ilikuwa takriban wakimbizi 500 kwa siku wanaingia Jordan.   Shirika la kimataifa [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

21/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031