Nyumbani » 17/01/2013 Entries posted on “Januari 17th, 2013”

Kazi bado kubwa kudhibiti vifo vya wajawazito

Kusikiliza / akina mama wajawazito

Mkutano wa kimataifa kuhusu afya ya wajawazito umemalizika huko Arusha Tanzania ambako imeelezwa kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kupunguza vifo vya wajawazito, bado kuna changamoto ili kuweza kufikia lengo la Milenia la kupunguza vifo hivyo kwa asilimia 75. Katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, Naibu Waziri wa afya wa Tanzania Dkt. Seif [...]

17/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Surua bado tishio baadhi ya maeneo licha ya mafanikio: WHO

Kusikiliza / Muuguzi akimpatia mtoto chanjo dhidi ya Surua

Shirika la afya duniani, WHO limesema licha ya dadi ya vifo vitokanavyo na Surua kupungua kwa asilimia 71 kati ya mwaka 2000 na 2011 duniani, ugonjwa huo bado ni tishio baadhi ya maeneo. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa Alhamisi na WHO ambapo kwa mwaka 2000 kulikuwa na vifo 542,000 ikilinganishwa na [...]

17/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Israel yajiunga na makataba wa kuzuia uchafuzi wa mazingira

Kusikiliza / unece-israel

Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi kwa bara Ulaya UNECE imekaribisha hatua ya Isreal ya kujiunga kwenye mkataba wa uchafuzi wa mazingira na habari kwa umma pamoja na kushirikishwa kwa umma katika utoaji wa maamuzi likiwa ndilo taifa nambari 32 kujiunga na mkataba huo. Mkataba huo ndio wa kwanza wa kimataifa kuhusu uchafuzi wa [...]

17/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya DRC na waasi wa M23 wakubaliana ajenda ya mazungumzo

Kusikiliza / kikundi cha waasi cha M23

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC na waasi wa kikundi cha M23 wanaokutana nchini Uganda wamekubaliana juu ya ajenda ya mazungumzo kati yao yaliyoanza tarehe 10 Desemba mwaka 2012 mjini Kampala. Ajenda ya mazungumzo ilizua vuta nikuvute baina ya pande mbili hizo na kukwamisha mazungumzo kwa siku tano. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na [...]

17/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mapigano kaskazini mwa Darfur yasababisha kuhama kwa watu wengi

Kusikiliza / watu wahama Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID umesema kuwa umejitolea kushirikiana na washikadau wote kwa minajili ya kuwahudumia maelfu ya raia waliokimbia vijiji vilivyo Kaskazini mwa jimbo la Darfur vya Saraf Omra, Kabkabya na El Sereif. Tangazo hilo linajiri baada ya tathmini ya siku mbili ya [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa Rais Rajoelina ni wa busara: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesifu uamuzi wa Rais wa mpito wa Madagascar Andry Rajoelina, wa kutogombea wadhifa huo katika kinyang'anyiro cha Urais mwezi Mei mwaka huu. Bwana Ban amekaririwa akisema kuwa kitendo cha Rais Rajoelina pamoja na ahadi ya awali ya Rais wa zamani Marc Ravalomanana, vitasaidia kuwepo kwa uchaguzi huru [...]

17/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Upanuzi wa kilimo huongeza upotevu wa bayonuai: UNEP

Kusikiliza / mavuno bora

Ripoti moja iliyoangazia ukuaji wa shughuli kilimo pamoja uhifadhi wa mazingira katika nchi za Ki-tropiki, imebainisha namna nchi zinavyopata msukumo wa kuendeleza ardhi kwa ajili ya kupata mavuno zaidi. Ripoti hiyo imesema kuwa, mataifa mengi yanajiingiza katika kile alichokiita maamuzi ya haraka ya kuendeleza ardhi kwa ajili ya kujipatia faida kwenye mazao kama mahindi na [...]

17/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baridi kali ya dhoruba yataabisha wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / baridi kali

Mabadiliko ya hali ya hewa yaliyokumba nchi za Lebanon, Jordan na  Iraq ambazo zimekubwa na mvua kubwa iliyoambatana na theluji kali, imetajwa kuvuruga ustawi wa wakimbizi wengi wa Syria. Kumekuwa na uharibifu mkubwa katika kambi ya Za'atari iliyoko kaskazini mwa Jordan ambako mahema pamoja na mifumo ya upitishaji maji imevurugwa. Mamia ya wakimbizi wengi wao [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa chakula wapungua Afrika Mashariki

Kusikiliza / mazao

Hali ya upatikanaji chakula katika eneo la Afrika Mashariki imeimarika na wasiwasi uliokuwa ulikumba eneo hilo wa umetoweka, kufuatia mavuno mazuri yaliyoanza kupatikana katika msimu wa mwezi Octoba mwaka 2012. Lakini hata hivyo mafanikio hayo hayajaondoa wasiwasi wa moja kwa moja juu ua uwekezakano wa kushudua ukosefu wa chakula katika baadhi ya maeneo. Inakadiriwa kwamba [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya ukata UNHCR yajiandaa na ongezeko la wakimbizi Mali

Kusikiliza / wakimbizi wa Mali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema licha ya ukata unaolikabili limejiandaa kuwahudumia wakimbizi ambao idadi yao inaweza kuongezeka kutokana na kuendelea kwa mapigano huko Kaskazini mwa Mali. Wakimbizi hao wanaongezeka ndani ya Mali na hata wengine wanakimbilia nchi jirani za Niger, Burkina Faso na Mauritania ambapo mwakilishi wa UNHCR nchini Niger [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930