Nyumbani » 16/01/2013 Entries posted on “Januari 16th, 2013”

Nguvu za kijeshi haziwezi kutokomeza ugaidi: UM

Kusikiliza / Balozi Masood Khan, Rais wa sasa wa Baraza la Usalama

Baada ya mjadala wa siku nzima kuhusu vita dhidi ya ugaidi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kamwe nguvu za kijeshi haziwezi kutokomeza ugaidi. Badala yale limesema mkakati wa kina na endelevu ndio njia pekee ya kukabiliana na ugaidi ambapo mkakati huo ushughulikie mazingira yanayochochea vitendo hivyo vya kihalifu. Baraza hilo limekaririwa kupitia [...]

16/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICC sasa yamulika uhalifu wa kivita Mali

Kusikiliza / Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai

Mwendesha mashtaka Mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai yanayohusika na uhalifu wa kivita, ICC, Fatou Bensouda amefungua rasmi uchunguzi dhidi ya vitendo vya  uhalifu vinavyodaiwa kufanyika Mali tangu mwezi Januari mwaka jana. Hatua hiyo inafuatia uchunguzi wa awali uliofanywa na ofisi yake kuhusu hali halisi nchini Mali ambapo sasa amesema ameridhika kuwa [...]

16/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasyria kuweni macho mgogoro unararua Taifa: Ban

Kusikiliza / Mji wa Aleppo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewataka wananchi wa Syria kutafakari upya mgogoro unaondelea nchini mwao ambao amesema unazidi kurarua taifa hilo vipande vipande. Bwana Ban amesema hayo katika taarifa iliyomnukuu kufuatia shambulio dhidi ya Chuo Kikuu Aleppo kwenye mji wa Aleppo nchini Syria ambapo watu zaidi ya 80 wameripotiwa kuuawa na wengi [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamateni wabakaji na si waandishi: Bangura

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya ukatili wa kingono katika maeneo ya migogoro, Hawa Zainab Bangura amezungumzia sakata la kushikiliwa kwa mwandishi wa habari nchini Somalia baada ya kumhoji mwanamke anayedaiwa kubakwa na askari wa jeshi la nchi hiyo ambapo ametaka serikali kumwachia mara moja mwandishi huyo. Katika taarifa yake [...]

16/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

AU yazungumzia Madagascar na Mali

Kusikiliza / mapigano nchini Mali

Umoja wa Afrika umekaribisha hatua ya rais wa Madagascar Andry Rajolina ya kutangaza kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu kukubali sharti lililkotoewa na Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika SADC, iliyotaka kuwepo kwa maelewano ya kisasa ili kuondosha hali ya uhamasama iliyoliandama taifa hilo kwa miaka kadhaa. [...]

16/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaungana na mataifa kadha kupunguza vifo vya watoto

Kusikiliza / watoto

Mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika wanakutana Addis Ababa Ethiopita kuanzia leo kwa lengo la kuweka mikakati mipya ya kudhibiti vifo vya watoto. Ripoti zinasema kuwa idadi ya watoto wanaokufa kwenye nchi za AFrika zilizo kusini mwa jangwa la sahara ilipungua kwa asilimia 39 tangu mwaka 1990. Mataifa mengi ya bara la Afrika kwa [...]

16/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

16/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Viashiria vya uchumi kudorora vyatoweka: Benki ya Dunia

Kusikiliza / uchumi wa nchi zinazoendelea

Ripoti ya benki ya dunia ambayo inaangazia hali ya uchumi wa kimataifa imesema kuwa mkwamo mbaya zaidi wa kiuchumi ulioikumba dunia katika kipindi cha miaka mine iliyopita, sasa unaonekana kutoweka. Ripoti hiyo ambayo imemulika maendeleo ya uchumi wa dunia baada ya mtikisiko wa kiuchumi, imefafanua kuwa, hali iliyosababisha kuyumba kwa uchumi wa dunia haiko tena. [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watoto 1.3 nchini Yemen wameajiriwa: ILO

Kusikiliza / mtoto nchini Yemen

Zaidi ya watoto milioni 1.3 nchini Yemen wanashirikishwa kwenye ajira za watoto ambapo kati yao takribani Laki Tano wana umri wa kati ya miak a469,000 walio umri wa kati ya miaka 5-11, na hiyo ni kwa mujibu wa utafiti mpya wa Shirika la kazi duniani ILO. Hii ina maana kwamba asilimia 17 ya watoto milioni [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

G77 na ushawishi wa agenda ya UM: Ban

Kusikiliza / Mourad Benmehidi na Commodore Josaia V. Bainimarama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kundi la nchi 77 zinazoendelea, G77 pamoja na China zina ushawishi mkubwa wa kusukuma mbele agenda zinazopigamiwa na Umoja wa Mataifa katika miaka ya usoni. Amesema kuwa wakati Umoja huo wa Mataifa ukiweka vipaumbele ambavyo inakusudia kuvitilia mkazo katika miaka inayokuja ikiwemo mpango wa maendeleo endelevu, [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Mali; Umoja wa Afrika wapaza sauti

Kusikiliza / wanachi wa Mali

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Boni Yayi wa Benin ametaka Jumuiya ya kimataifa kuunga mkono jitihada za kuwafurusha vikundi vya wanamgambo vyenye silaha huko Mali, operesheni ambayo kwa sasa inaongozwa na Ufaransa. Rais Yayi amesema hayo mjini Dar Es Salaam baada ya mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete ambapo amesema kitendo cha waasi hao [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Magonjwa yaliyosahaulika kutokomezwa kabisa: WHO

Kusikiliza / who-girl

Shirika la afya duniani, WHO limejivunia maendeleo ya aina yake katika vita dhidi ya magonjwa 17 yaliyosahaulika ambayo yameendelea kuwa mzigo mkubwa kwa nchi maskini duniani. Magonjwa hayo ni kama matende, mabusha, kichocho na usubi. WHO imesema hatua hiyo imetokana na mkakati wa dunia unaotumia mbinu rahisi ya tiba na kinga na ushirika wa kimataifa [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria yaruhusu WFP kusambaza misaada

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Hatimaye serikali ya Syria imeruhusu shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo kusambaza vyakula vya misaada kwa watu Milioni Mbili na Nusu walionaswa katika shida kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo. Mkurugenzi mkuu wa WFP Ertharin Cousin ameaambia waandishi wa habari mjini Geneva leo kuwa wamepata kibali [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031