Nyumbani » 15/01/2013 Entries posted on “Januari 15th, 2013”

Ugaidi ni "zimwi" lisilo na mpaka: Pakistani

Kusikiliza / Hina Rabbani Khar

Mikakati ya kimataifa ndio njia pekee ya kupambana na ugaidi, na hiyo ni kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani, Hina Rabbani Khar aliyoitoa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumane wakati wa mjadala wa wazi kuhusu vita dhidi ya ugaidi. Bi.Khar ambaye aliendesha mjadala huo kwa kuzingatia [...]

15/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauaji ya raia akiwemo mbunge huko Iraq

Kusikiliza / Martin Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler ameshutumu vikali mauaji ya mbunge Ifan Al-Issawi nchini Iraq yaliyotokana na shambulio la kigaidi wakati wa maandamano huko Fallujah ambapo pia watu kadhaa waliuawa na wengine walijeruhiwa. Kobler ambaye anaongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi nchini Iraq UNAMI amesema ni [...]

15/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

CERF yatoa fedha na kupambana na njaa nchini Malawi

Kusikiliza / Malawi

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umeidhinisha kutolewa kwa dola milioni 3.2 zitakazotumiwa kupambana na tatizo la ukosefu wa chakula nchini Malawi nchi ambayo zaidi ya nusu ya wananchi wake wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku huku asilimia 46 ya watoto walio chini ya miaka wakiwa na matatizo ya kukua. Kutokana [...]

15/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu Mali yazidi kuzorota

Kusikiliza / raia wa Mali

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inakadiriwa kuwa takribani. Laki Tatu hadi jana ambapo kabla Ufaransa haijaanza mashambulizi ya kijeshi kwa ridhaa ya serikali ya Mali idadi ya wakimbizi wa ndani ilikuwa takribani Laki Mbili. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA. (SAUTI YA JENS [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waliovuka ghuba ya Aden yavunja rekodi

Kusikiliza / wahamiaji wavuka ghuba ya Aden

Takriban wakimbizi na wahamiaji 107,500 walifanya safari zilizo hatari kutoka pembe ya Afrika kwenda nchini Yemen mwaka 2012 ikiwa ndiyo idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na wahamiji kuwahi kuandikishwa tangu mwaka 2006 wakati shirika la kuhudumia wakimbzi la Umoja wa Mataifa UNHCR lilipoanzisha ukusanyaji wa takwimu hizo. UNHCR inasema kuwa wanane kati watu kumi waliowasili [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna cha kuhalalisha ugaidi: Ban

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kamwe hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha ugaidi duniani. Hata hivyo amesema ni lazima kushungulikia mazingira yanayochochea vitendo hivyo. Bwana Ban amesema hayo leo katika hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama juu ya mikakati ya kukabiliana na ugaidi duniani. Amesema mashauriano baina ya [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mbegu mpya na uhakika wa chakula Sudan Kusini

Kusikiliza / mbegu mpya Sudan Kusini

Wakulima wa hali ya chini katika Jamhuri ya Sudan Kusini wanapatiwa mbegu bora ili waweza kuzalisha mazao muhimu ikiwa ni sehemu ya kuwainua kimaisha . Mpango huo ambao unapigwa jeki na serikali ya Ufaransa kwa kushirikiana na shirika la chakula duniani FAO na Wizara ya Kilimo nchini humo unatekelezwa katika majimbo kadhaa na kwa muhula [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wanaorejea Niger wapatiwa stadi

Kusikiliza / wahamiaji

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua mpango wa kuwasaidia wahamiaji raia wa Niger wanaorejea nyumbani kutoka Libya pamoja na familia zinazowahifadhi. Mradi huo ambao tayari umepokea Euro milioni 2.8 kutoka kwa jumuiya ya Ulaya utasaidia kubuni miradi itakayochangia mapato kwa watu 3,125 moja kwa moja kutoka sehemu za Tahoua, Tillabery, Zinder na mji mkuu [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yasababisha watu zaidi kukimbia Mali

Kusikiliza / wananchi wa Mali

Makabiliano kati ya jeshi la Mali linaloungwa mkono na ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Al-Qaida kwenye maeneo ya Konna, Lere na Gao kaskazini mwa Mali yamesabisha kuhama kwa watu ndani na kwenda nchi majirani zake. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa zaidi ya watu 648 kwa sasa ni wakimbizi wa [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yaanza kurejea Somalia

Kusikiliza / Askari polisi wa Somalia akiwa kwenye doria

Nchini Somalia hususan mji mkuu Mogadishu ambapo awali vikundi vya kigaidi vilitamba, hali ya amani imeanza kutengamaa. Wananchi nyakati za usiku wanafanya shughuli zao hata kucheza mpira wa miguu ambao awali ulipigwa marufuku na Al Shabaab. Je nini imesababisha hali hii? Jiunge na Assumpta Massoi kwa ripoti maalum… Mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu, giza limeingia…..kwa [...]

15/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031