Nyumbani » 14/01/2013 Entries posted on “Januari 14th, 2013”

Jeshi la Afrika kwenda Mali punde

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Baraza la usalama hii leo lilikuwa na kikao  kuhusu hali ilivyo huko Mali ambapo Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud amesema wajumbe wote wa baraza wameunga mkono hatua za kijeshi za Ufaransa kwa ridhaa ya Mali. Bwana Araud amewaambia waandishi wa habari kuwa tayari nchi zingine ikiwemo Marekani, Canada na [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kitabu cha Annan chamulika changamoto na mafanikio

Kusikiliza / Kitabu cha Kofi Annan

Masuala ya amani, ulinzi, usalama, uongozi bora na misaada na maendeleo ni miongoni mwa mambo yaliyochukua nafasi katika kitabu kilichoandikwa na Katibu Mkuu  mstaafu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, A Life in War and Peace. Akizungumza katika hafla ya kuzindua kitabu hicho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani hii [...]

14/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Nafuatilia kwa karibu hali ya Mali: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati  hali ya usalama ikiripotiwa kuendelea kuzorota huko Mali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anafuatilia kwa karibu hali hiyo ambapo tayari amezungumza na Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Rais Alassane Ouattara wa Côte d’Ivoire . Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza kujulishwa [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kurejea kwa Dkt. Mukwege ni ujasiri: Meece

Kusikiliza / Dkt. Denis Mukwege

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC, Roger Meece ameunga mkono kurejea huko Bukavu, Kivu Kusini kwa Dkt. Denis Mukwege, Mganga Mkuu wa hospitali ya Panzi ambaye mchango wake kwa tiba kwa wanawake waliokumbwa na ukatili wa kingono ikiwemo kubakwa unatambulika duniani kote. Bwana Meece ambaye [...]

14/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maelfu wapoteza makazi kufuatia mzozo Mali

Kusikiliza / Wakimbizi Mali

  Takribani watu Elfu Thelathini wanahofiwa kuwa wamepoteza makazi yao kutokana na mapigano huko maeneo ya Kati na kaskazini mwa Mali na inahofiwa kuwa idadi yao inaweza kuwa kubwa kwa kuwa vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kiislamu vinazuia watu kukimbilia maeneo ya Kusini. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo del Buey [...]

14/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa UM kuhusu haki ya kukusanyika kwa amani aitembelea uingereza

Maina Kiai

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki kukusanyika kwa amani na kushauriana Maina Kiai ataitembelea uingereza kuanzia tarehe 14 hadi 23 ziara ambayo itakuwa ndiyo ya kwanza ya ukusanyaji wa habari kufanywa na mtaalamu kama huyo aliyetumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza haki ya kukusanyika kwa amani na [...]

14/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Haki ya kibinadamu Yemeni bado tete

Kusikiliza / ramani ya Yemen

Kusainiwa kwa mpango wa amani uliokaribisha kipindi cha mpito nchini Yemen kumefungua njia ya kukaribisha huduma za utoaji wa misaada ya kibinadamu ambayo hapo kwanzo ilizorota kutokana na hali mbaya ya kisiasa. Jarida la masuala ya kibinadamu la Umoja wa Matalifa linasema kuwa mapema mwaka uliopita kulisainiwa makubaliano ya kuwepo kwa kipindi cha mpito kuelekea [...]

14/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jeshi la kimataifa kuungana na MONUSCO: Gaye

Kusikiliza / Babacar Gaye

Mshauri wa masuala ya kijeshi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jenerali Babacar Gaye, amesema kuunganishwa kwa jeshi la kimataifa linalokwenda mpakani wa Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRCna kikosi cha MONUSCO kutasaidia kupunguza gharama za fedha. Jenerali Gaye amesema hayo alipozungumza na Radio Okapi baada ya kurejea kutoka Addis Ababa, Ethiopia [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

14/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uingereza yaipiga 'jeki' Haiti

Kusikiliza / mabaki ya tetemeko, Haiti

Wito kwa nchi kusaidia Haiti kujijenga baada ya tetemeko kubwa miaka mitatu iliyopita umepata jibu baada ya Uingereza kutangaza mkopo nafuu wa dola Milioni 16 ili iweze kujikwamua haraka na madhila ya sasa. Taarifa iliyotolewa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP imesema fedha hizo pamoja na mambo mengine zitajenga uwezo [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazoibuka kiuchumi zapongezwa kwa kumulikia afya

Kusikiliza / Michel Sidibe

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na HIV na Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé amepongeza hatua za nchi zinazoibukia kiuchumi duniani ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, BRICS ya kuazimia kushirikiana kuboresha sekta ya afya duniani. Mathalani amegusia dhima ya kipekee ya nchi hizo kutumia uzoefu wao wa kupambana na [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tusipuuze ukiukwaji haki za binadamu Korea Kaskazini: Pillay

Kusikiliza / malnutri-dprk

Kamishna mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua kutatua suala la haki za binadamu nchini Korea Kaskazini akisema kuwa wakati umewadia wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu uhalifu ambao umekuwa ukiendelea nchini humo kwa miaka mingi. Pillay amesema kuwa kulikuwa na matumani ya mabadiliko [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunisia iangalie upya usawa wa jinsia: Wataalamu UM

Kusikiliza / Kamala Chandrakirana

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa wanawake kwa misingi ya sheria na vitendo limetaka serikali ya Tunisia kuridhia vipengele vya msingi vya katiba juu ya usawa wa jinsia na kutekeleza hatua maalum za muda zitakazoharakisha ushiriki wa wanawake katika Nyanja zote za maisha. Akizungumza mwishoni mwa ziara ya wataalam hao [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031