Nyumbani » 11/01/2013 Entries posted on “Januari 11th, 2013”

Mzozo CAR, Baraza la usalama lasifu makubaliano ya Libreville

Kusikiliza / Baraza la usalama likipatiwa ripoti kutoka kwa Margaret Vogt kwa njia ya video

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesifu mashauriano yaliyofanyika huko Libreville Gabon, na kuwezesha kutiwa saini kwa makubaliano ya kimsingi ya kusitisha mapigano na kupatia suluhu la kisiasa mzozo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa ya  Baraza hilo iliyotolewa mwishoni mwa kikao maalum kuhusu hali ya usalama nchini humo imesema wajumbe wanataka kuharakishwa [...]

11/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Biashara haramu ya tumbaku yaanza kubanwa

Kusikiliza / Wanawake wakifungasha sigara

Hatimaye itifaki ya kutokomeza biashara haramu ya bidhaa za Tumbaku imeanza kutiwa saini na hivyo kuonyesha utashi wa kisiasa wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku. Hafla hiyo ilifanyika mjini Geneva Uswisi kwa mataifa 12 wanachama wa mkataba huo kutia saini na baadaye shughuli hiyo itahamishiwa New York, Marekani makao [...]

11/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Lahitajika jeshi thabiti CAR: Vogt

Kusikiliza / Margaret Vogt

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limeelezwa jinsi hali  ya usalama ilivyo tete huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako jeshi linashindwa kudhibiti waasi wanaoendelea kushikilia miji kadhaa nchini humo. Taarifa hizo zimetolewa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa nchini humo Margaret Voght wakati akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu [...]

11/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP kutoa msaaada kwa karibu watu 1.6 nchini Zimbabwe

Kusikiliza / Hali ya chakula Zimbabwe

Karibu watu milioni 1.6 nchini Zimabbwe wengi wanaoishi sehemu za vijijini kwa sasa wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula kutokana na sababu ya ukosefu wa mvua na kupungua kwa mazao ya kilimo. Kulingana na msemaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kanda ya mashariki na kusini mwa Afrika Davi Orr ni kuwa WFP [...]

11/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya wakimbizi CAR inatutia wasiwasi: UNHCR

Kusikiliza / Watu wakihama makwao huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linataka kuwafikia wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati bila masharti yoyote kwa kuwa lina wasiwasi kuwa hali zao zitakuwa ni mbaya. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwrds akizungumza mjini Geneva leo amesema maelfu ya watu wamekimbia makazi  yao kutokana na mapigano kaskazini na mashariki mwa nchi [...]

11/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

11/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wazungumzia ghasia zinazoshuhudiwa nchini Kenya

Kusikiliza / tana river

Umoja wa Mataifa umetuma rambi rambi zake kwa serikali ya Kenya pamoja na kwa familia za watu waliothiriwa na ghasia zinazoshuhudiwa kwenye eneo la Mto Tana na sehemu zeningine za nchi. Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya masuala ya kibinadamu nchini Kenya, Umoja wa Mataifa umelaani kile unachokitaja kuwa vitendo viofu ambavyo tangu mwanzo wa [...]

11/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya Geneva bado msingi wa amani Syria: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi, Mjumbe maalum wa pamoja wa UM na nchi za kiarabu kwenye mgogoro wa Syria

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi ametoa muhtasari wa mazungumzo yake na naibu mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani  William Burns na yule wa Urusi Mikhail Bogdanov yaliyofanyika huko Geneva, Uswisi ambapo amesema kwa pamoja wametambua madhila wanayopata wananchi wa Syria na [...]

11/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kunyongwa kwa mfanyakazi wa nyumbani Saudi Arabia kunasikitisha: Pillay

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya UM, Navi Pillay

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kufuatia kitendo cha kunyongwa hadi kufa kwa mfanyakazi wa nyumbani Rizana Nafeek huko Saudi Arabia kwa kosa la kumuua mtoto wa mwajiri wake. Msemaji wa Ofisi hiyo Rupert Colville amemkariri Pillay akisema kuwa adhabu hiyo ni kinyume na haki [...]

11/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNAMID yataka kusitishwa mapigano ya kikabila kwenye eneo la Jebel Amer

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

  Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID unasema kuwa umetiwa wasi wasi na mapigano kati ya kabila za Hussein na Abbala katika eneo la Jebel Amer karibu na Kabkabiya Darfur kaskazini. Mapigano hayo yanayoripotiwa kuanza tarehe tano mwezi Januari mwaka huu yamesabisha mauaji [...]

11/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Burundi waanza maisha mapya

Kusikiliza / wakimbizi wa Burundi warejea nyumbani

Kambi ya Mutabila iliyokuwa imewapokea wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania imefungwa rasmi tarehe 31 Mwezi Desemba mwaka jana na kuwa kambi ya mwisho kabisa kufungwa. Kambi iliyoko magharibi mwa Tanzania ilikuwa imewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 36 Elfu wa Burundi ambao tayari wamerejea nchini mwao Burundi katika shughuli iliyosimamiwa na Shirika la kimataifa la kuwahudumia [...]

11/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930