Nyumbani » 10/01/2013 Entries posted on “Januari 10th, 2013”

Hali ya Mali yatishia usalama wa kikanda na dunia: UM

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Wajumbe wa Baraza la usalama waliokutana katika kikao cha dharura jioni ya leo kuhusu Mali wameeleza kusikitishwa kwao na ripoti ya kwamba vikundi vya kigaidi na vyenye msimamo mkali kaskazini mwa nchi hiyo vinaendelea na mashambulizi, wakigusia zaidi taarifa za kutekwa kwa mji wa Konna. Rais wa Baraza hilo Balozi Masood Khan amewaambia waandishi wa [...]

10/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya Pakistani yanitia wasiwasi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kusikitishwa kwake na mwendelezo wa mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistani akigusia shambulio la jana na la leo. Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban ameshutumu mashambulio hayo katika eneo la Quetta na Swat ambayo yamesababisha vifo vya watu wapatao 100 [...]

10/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ladsous aanza ziara Haiti

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous  na Rais Michel Martelly wa Haiti.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Hervé Ladsous, amesema kazi iliyopo hivi sasa nchini Haiti, miaka mitatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi ni kujikita zaidi katika kujenga jeshi la polisi la kitaifa na kuimarisha wa utawala wa kisheria. Bwana Ladsous amesema hayo alipozungumza na waandishi wa [...]

10/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Upanzi wa miti waokoa wakulima Kenya: UNEP

Kusikiliza / maji nchini Kenya

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa upanzi wa miti kwenye miteremko ya Mlima Kenya umekuwa wa manufaa kwa wakulima waliokuwa wanategemea msimu wa mvua kwenye shughuli zao za kilimo huku pia ukichaangia katika kupunguza umaskini. Kupitia mradi huo unaohusu upanzi wa miche kwenye sehemu za vyanzo vya maji umewanufaisha wakulima hasa sehemu na mashariki mwa [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova alaani mauaji ya waandishi wa habari nchini Syria

Kusikiliza / Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, Irina Bokova ameelezea wasi wasi wake kufuatia kuendelea kuuawa kwa waandishi wa habari nchini Syria , baada ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha runinga Suhail Mahmoud Al-Ali Ijumaa iliyopita. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (SAUTI YA JASON [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zebaki tishio la afya na mazingira: UNEP

Kusikiliza / zebaki

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP limesema kadri siku zinavyosonga, zebaki inazidi kutishia afya ya binadamu na mazingira katika nchi zinazoendelea kutokana na ongezeko la uchafuzi wa mazingira utokanao na madini hayo. UNEP imesema metali hiyo yenye sumu hutumiwa na wachimbaji wadogo katika shughuli zao na pia katika uchomaji wa makaa ya mawe [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malawi isimamie marekebisho ya kiuchumi: IMF

Kusikiliza / Christine Lagarde

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la fedha ulimwenguni IMF, Christine Lagarde amewataka wananchi wa Malawi kuendelea kutekelezwa mageuzi magumu ya kiuchumi yaliyopendekezwa na shirika hilo ambayo yanapigwa na idadi kubwa ya wananchi. Lagarde ametoa wito huo wakati akikamilisha ziara yake ya siku tatu. Taarifa zaidi na George Njogopa: (SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula zaendelea kushuka: FAO

Kusikiliza / vyakula

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema wastani wa bei ya chakula ulishuka kwa asilimia Saba mwezi Disemba mwaka jana na hivyo kufanya bei za vyakula kupungua kwa miezi mitatu mfululizo. Ripoti ya FAO kuhusu bei ya za chakula inaonyesha bei ya kapu la chakula ilishuka kwa pointi Moja nukta Moja [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara haramu ya tumbaku sasa mtegoni: WHO

Kusikiliza / Wajumbe katika hafla ya kutia saini itifaki ya kuzuia biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na tumbaku

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO, Dkt. Margaret Chan amesema itifaki mpya ya kutokomeza biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na tumbaku inaipatia dunia fursa ya kipekee ya kudhibiti njia za kisasa za kitendo hicho cha kihalifu chenye gharama kubwa hususan kwa afya za binadamu. Dkt.Chan amesma hayo leo mjini Geneva, Uswisi wakati wa [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031