Nyumbani » 09/01/2013 Entries posted on “Januari 9th, 2013”

Baada ya tetemeko, Haiti inajikwamua:UM

Kusikiliza / Wananchi wa Haiti wakishiriki ujenzi wa nchi yao.

Miaka mitatu tangu tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti, Umoja wa Mataifa umesema jitihada za kusadia nchi hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida zimetia matumaini ikiwemo ujenzi wa shule, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Hiyo ni kauli ya Afisa Mtendaji Mkuu wa wakfu ya Umoja wa Mataifa Kaithy Calvin aliyoitoa alipozungumza na [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria zitungwe kulinda wafanyakazi wa majumbani: ILO

Kusikiliza / wafanyakazi majumbani

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO imeweka bayana kuwa bado kazi za majumbani zinadharauliwa licha ya mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii. ILO inasema ajira hiyo ni ya manyanyaso, kuanzia muda wa kazi hadi maslahi. Ripoti inaonyesha kuwa kiidadi, wafanyakazi hao wanaongezeka lakini maslahi yao yanazidi kuwa duni hasa katika nchi zinazoendelea. [...]

09/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aunga mkono azma ya Abe ya kuinua uchumi wa Japan

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu mpya wa Japan Shinzo Abe ambapo pamoja na kumpongeza kwa wadhifa huo mpya, amesema anaunga mkono azma ya Abe ya kujenga upya uchumi wa Japan baada ya tetemeko kubwa la ardhi la mwaka 2011 pamoja na Tsunami. [...]

09/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana wakutana Seoul kujadili matatizo yanayokumba eneo la Asia

Kusikiliza / vijana

Nafasi za ajira, kutokuwepo kwa usawa, mazingira, usawa wa kijinsia, amani na usalama huko Kaskazini-mashariki mwa Asia ni miongoni mwa masuala kuu ambayo vijana wa eneo hilo wanataka yazingatiwe katika ajenda ya baadaye ya maendeleo. Washirikishi vijana kutoka nchi kama vile China, Japan na Mongolia wameafikia makubaliano kuhusu maendeleo ya dunia yenye kauli mbiu "Ulimwengu [...]

09/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mapigano Darfur ya kati yanaathiri raia: UNAMID

Kusikiliza / Aichatou Mindaoudou

Kaimu mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID Aichatou Mindaoudou ametembelea mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kati, Zalingei ambapo ameelezea wasiwasi wake juu ya mapigano yanayoendelea kwenye mji wa magharibi wa Jebel Marra. Ameelezea wasiwasi wake huo baada ya mazungumzo na gavana wa jimbo hilo [...]

09/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Canada kufanya mazungumzo ya viongozi wa kitamaduni

Kusikiliza / James Anaya

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya jamii za kiasili James Anaya ametoa wito kwa serikali ya Canada kufanya mazungumzo na viongozi wa kitamaduni nchini humo kufuatia kushuhudiwa kwa maandamano hivi majuzi. Mjumbe huyo amesema amefurahishwa na ripoti kwamba waziri mkuu wa Canada Steven Harper amekubali kukutana na viongozi hao kuzungumzia masuala yakiwemo [...]

09/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yapongeza ripoti mpya ya “Save the Children”

Kusikiliza / save the children

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limepongeza ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali la Uingereza, Save the Children inayomulika mikakati ya kutokomeza umaskini na dira ya watoto baada ya mwaka 2015. UNICEF imesema ripoti hiyo inatoa mwelekeo wa kusimamia haki za msingi za mtoto ikiwemo ile ya kuishi, kulindwa na kuendelezwa [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nitaimarisha mtandao wa posta duniani: Hussein

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa UPU Bishar Hussein

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Umoja wa mashirika ya posta duniani, UPU, Bishar Hussein kutoka Kenya amesema azma yake kubwa ni kuimarisha mtandao wa mashirika ya posta duniani. Akizungumza mjini Berne, Usiwsi leo wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi, ili kuchukua wadhifa huo kwa kipindi cha miaka minne, Bwana Hussein amesema atahakikisha nchi zote kuanzia zilizoendelea, [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani yazidi kusakwa Syria, IOM yaomba msaada zaidi

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakdhar Brahimi, Ijumaa atakuwa na mazungumzo na viongozi wa Urusi na Marekani kwa lengo la kupatia suluhu la kisiasa mzozo unaoendelea nchini Syria. Habari zinasema kuwa mazungumzo hayo baina ya Brahimi na Naibu Waziri wa mambo ya Nje [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa majumbani Tanzania hawajitambui: ILO

Kusikiliza / wafanyakazi wa nyumbani

Ofisi ya ILO nchini Tanzania imesema bado kuna changamoto kubwa ya kuweza kuwakomboa wafanyakazi wa majumbani dhidi ya matatizo yanayowakabili licha ya kwamba sheria za kazi zinawatambua. Mratibu wa mpango wa misaada ya maendeleo katika ofisi ya ILO nchini Tanzania, Anne-Marie Kiaga ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa changamoto hizo ni za pande tatu [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa majumbani waendelea kunyanyasika: ILO

Kusikiliza / mfanyakazi wa nyumbani

Ripoti mpya ya shirika la Kazi duniani, ILO kuhusu hali ya wafanyakazi wa majumbani imeonyesha kupanuka kwa sekta hiyo huku mazingira ya kazi yakiendelea kuwa duni hususan katika nchi zinazoendelea. Mathalani ripoti hiyo imesema kuwa wafanyakazi hao wanaendelea kunyanyaswa ikiwemo kufanya kazi saa nyingi kupindukia kwa ujira mdogo, kufanya kazi kwa saa nyingi ikitolea mfano [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031