Nyumbani » 08/01/2013 Entries posted on “Januari 8th, 2013”

Hali za wakimbizi huko Sudan ni mbaya: Ging

Kusikiliza / Blue-Nile-State-27Sept-UNHCR

Mamia ya maelfu ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali na vikundi vya waasi wenye silaha kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha. Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa OPeresheni wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya [...]

08/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bangura aunga mkono vikwazo dhidi ya waasi DRC

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ukatili wa ngono kwenye maeneo ya migogo Zainab Hawa Bangura amesema anaunga mkono vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama dhidi ya vikundi vya waasi vya FDLR na M23 huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (SAUTI ASSUMPTA) Taarifa [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova asikitishwa na kifo cha Singh

Kusikiliza / Madanjeet Singh

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, ameelezea kusitikitishwa kwake kutokana na kifo cha Balozi mwema wa UNESCO Madanjeet Singh kilichotekea tarehe sita Januari. Amesema marehemu Singh alikuwa na juhudi na alijitolea katika kazi ya kuendeleza maelewano na amani na ni mfano wa kuigwa kwa watu kutoka mataifa, tamaduni na dini mbalimbali. Ameongeza kuwa UNESCO imepoteza [...]

08/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahitaji yazidi kuongezeka Syria

Kusikiliza / watoto nchini Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema mahitaji ya kibinadamu nchini Syria yanaongezeka, likitaja zaidi vyakula ambapo mikate na mafuta vimeadimika zaidi nchini humo. Shirika hilo linasema kuwa kwa sasa linahudumia watu Milioni Moja na Nusu kila mwezi wakati linakadiria kuwa watu Milioni Mbili na Nusu ndio wanaohitaji msaada. WFP imesema inashindwa kutoa msaada [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahrain iwaachie mara moja watetezi wa haki za binadamu: UM

Kusikiliza / maandamano, Bahrain

Ofisi ya Kamishna wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, imetaka kuachiwa mara moja kwa raia 13 wa nchi hiyo waliohukumiwa kifungo jela kwa kufanya maandamano dhidi ya serikali ya nchi hiyo. Ofisi hiyo imeeleza kusikitishwa na kifungo cha wanaharakati hao baada ya miaka miwili ya kesi licha ya matokeo ya tume huru ya [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baadhi ya sheria zinasababisha maambukizi mapya ya HIV: Rao

Kusikiliza / Prasad Rao

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Ukimwi kwa nchi za Asia na Pasifiki, Prasad Rao amesema baadhi ya sheria zinazofuatwa nchini humo zimesababisha kuwepo kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi licha ya mafanikio ya kudhibiti ugonjwa huo. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uswisi yatunisha mfuko wa IOM

Kusikiliza / wahamiaji wa Chad

Shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM pamoja la lile la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) yametia sahihi makubaliano ya mradi utakaowasaidia raia wa Chad waliorejea nyumbani kutoka Libya ambao kwa sasa wanaishi kwenye mikoa mitatu ya kaskazini iliyo jirani na mpaka wa Libya, Niger na Sudan. Msaada huo wa dola Milioni 2.9 kutoka Uswisi [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uvutaji sigara waongezeka nchi maskini: WHO

Kusikiliza / framework

Wakati shirika la afya duniani, WHO likiwa katika maandalizi ya mwisho ya shughuli ya kuanza kutia saini mkataba wa kimataifa wa kutokomeza biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na tumbaku siku ya Alhamisi, shirika hilo limesema kwa sasa kuna taswira tofauti ya kiwango cha uvutaji sigara duniani. Mkuu wa sekretarieti ya mkataba huo Dokta Dr. Haik [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa majumbani bado wametengwa: ILO

Kusikiliza / mfanyakazi wa nyumbani

Shirika la kazi duniani ILO limetoa ripoti yake kuhusu hali za wafanyakazi wa majumbani ambapo takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi hao huku maslahi yao yakiendelea kuwa duni na kuendelea kunyanyaswa ikiwemo kufanya kazi saa nyingi kupindukia kwa ujira mdogo. Ripoti hiyo iliyozinduliwa leo huko Geneva imetolea mfano Tanzania ambako wastani wa saa za [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031