Nyumbani » 04/01/2013
Entries posted on “Januari 4th, 2013”
Kusikiliza /

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Guinea-Bissau Jose Ramos Horta amesema yuko tayari kwenda nchini humo kutekeleza majukumu ya kuwezesha kurejea kwa amani na utulivu. Akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Ramos- Horta amesema anafahamu fika hali halisi ya Guinea-Bisssau kwa kuwa alishakwenda nchini humo, mara ya kwanza akiwa [...]
04/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]
04/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kazi duniani, ILO wiki ijayo itazindua ripoti mpya kuhusu hali za wafanyakazi wa majumbani duniani kote. Ripoti hiyo mpya inajaribu kugusia ukubwa wa sekta hiyo, mazingira ya kazi na mawanda ya ulinzi wa kisheria kwa wafanyakazi hao wa majumbani. Mathalani inajumuisha takwimu za dunia na za kikanda na inalenga kusaidia jitihada za serikali, [...]
04/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kilimo bora kinahitaji pia uwepo wa ardhi yenye rutuba. Nchi Gambia kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika tunaelezwa kuwa ardhi yenye rutuba hutumiwa zaidi na wanaume na wanawake hubakia pembezoni kwenye ardhi iliyochoka na hivyo hata kwa jitihada gani matunda ya kazi ni nadra kuonekana. Lakini kwa sasa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya [...]
04/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Nchi nyingi barani afrika zinalalamikiwa kutokana na kutoweka mazingira mazuri ya kuendelea vipaji vinavyochomoza kwa watoto. Hali hiyo imefanya ndoto za vijana wengi kuishia hewani kutokana na kukosa daraja la kuwaendeleza. Lakini nchini Tanzania nuru imeanza kuchomoza kidogo baada ya kueanzishwa darasa maalumu kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kisanaa. Sanaa hii inaelezwa kuwa kichocheo kikubwa [...]
04/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Wahamiaji Duniani IOM leo limetoa ripoti yake ya kwanza juu ya mwelekeo wa usafirishaji wa binadamu ambapo inaonyesha kuwa nusu ya visa vilivyoletwa mbele ya shirika hilo kwa ajili ya kupata msaada katika mwaka wa 2011 ni kuhusu dhuluma ya kulazimishwa kufanya kazi. Kabla ya hapo biashara ya kusafirisha binadamu iligusa zaidi usafirishaji [...]
04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Jumla ya watu Tisa waliwasilisha majina yao kuwania nafasi ya Ukurenzi Mkuu wa Shirika la biashara duniani, WTO ambapo mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy kipindi chake kinakoma tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu. Taarifa ya WTO inataja nchi wanazotoka watu hao kuwa ni Brazili, Jamhuri ya Korea, Mexico, Jordan, Costa Rica, New Zeland, Ghana, [...]
04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kundi la wachezaji mashuhuri wa ligi ya mpira wa kikapu NBA kutoka Marekani wameitembelea Kenya katika shughuli ya kupambana na ugonjwa wa kupooza. Wakiwa kwenye wilaya ya Turkana wachezaji hao wakiwemo Luc Mbah a Moute, Nick Collison and Dikembe Mutombo waliungana na kampeni ya kutoa chanjo ya nyumba hadi nyumba ya kuwachanja watoto wa eneo [...]
04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekamilisha mpango wake wa kurejesha nyumbani kwa hiari wakimbizi 155,000 wa Liberia waliokuwa wanaishi uhamishoni kwa miaka 23 baada ya kuanza kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao. Kundi la mwisho la wakimbizi 724 waliondoka kutoka Guinea na hivyo kukamilisha mpango huo ulioanza mwaka 2004, [...]
04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaka kusitishwa mara moja kwa vitendo vinavyofanywa na vikundi vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR vya kuandikisha watoto kwenye majeshi. UNICEF imetaka pande zote katika mzozo unaoendelea nchini humo kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote hatari ikiwemo kuhusishwa na mgogoro huo. Tamko la [...]
04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MONUSCO umesema kumekuwa na ongezeko kubwa la ghasia za kikabila katika eneo la Masisi lililoko jimbo la Kivu Kaskazini Taarifa ya kuwepo kwa matukio korofi inakuja baada ya MONUSCO kutuma maafisa wake waliokwenda kutathimini hali jumla ya mambo ikiwemo kuangazia hali ya usalama [...]
04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »