Nyumbani » 03/01/2013 Entries posted on “Januari 3rd, 2013”

Ban apongeza mpango wa mkutano wa Bashir na Kiir

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon

Marais Omar Al Bashir wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan Kusini Ijumaa watakuwa an mazungumzo yanayoratibiwa na Umoja wa Afrika kupitia Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki. Mazungumzo hayo yatafanyika nchini Ethiopia chini ya wenyeji wa Waziri Mkuu uwa nchi hiyo Hailemariam Desalegn ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon [...]

03/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Masuala ya Afrika kuendelea kumulikwa Baraza la Usalama

Kusikiliza / Masood Khan

Harakati za kupatia suluhu migogoro mbali mbali inayoendelea barani Afrika zitaendelea katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Januari, na hiyo ni kwa mujibu wa Rais wa  kipindi hicho Balozi Masood Khan kutoka Pakistani. Akitangaza mpango wa kazi wa Baraza la Usalama mbele ya waandishi wa habari mjini New York, [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unyanyapaa bado wakwamisha udhibiti wa Ukimwi

Kusikiliza / UKIMWI

Shirika lisilo la kiserikali linahusika na HIV na Ukimwi nchini India limetaja changamoto zinazolikabiili katika kazi ya kusaidia waathirika wa ugonjwa huo ikiwemo uhaba wa fedha na unyanyapaa. Loon Gange, ambaye ni Rais na mwanachama mwanzilishi wa DNP+ amesema kuwa ameshuhudia watu wengi wakiaga dunia kwa sababu hawakutibiwa kutokana na uhaba wa fedha na wengine [...]

03/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Utalii wa mazingira hutokomeza umaskini: UM

Kusikiliza / utalii wa mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la utalii, limesema kupitishwa kwa azimio linalotambua utalii wa viumbe na mazingira kama moja ya njia ya kupambana na umaskini na kulinda mazingira ni kitendo cha kupongezwa na kimefanyika wakati muafaka. Kwa mantiki hiyo shirika hilo limetaka nchi wanachama kubuni sera zitakazosaidia kuinua utalii wa mazingira ambao pia husaidia kutokomeza [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Udhibiti wa ajali za barabarani huokoa maisha na fedha: WHO

Kusikiliza / traffic

Utafiti mmoja uliochapishwa na jarida la shirika la afya ulimwenguni WHO, umesema nchi ambazo huchukua njia rahisi kudhibiti ajali za barabarani hunufaika na mambo mengi ikiwemo yale yenye taswira ya kiuchumi. Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la mwezi huu umesema kuwa pamoja na kwamba nchi hizo zinakubalika kwa kufaulu kuokoa maisha ya watu, lakini kwa [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashauriano kufanyika kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / baraza la usalama

Wakati hali ya usalama ikiendelea kudorora na kutia wasiwasi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baadaye leo litakuwa na mashauriano kuhusu hali ilivyo nchini humo. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA linasema kuwa watu wamekimbia makazi yao ikiwemo mji mkuu Bangui, na kwamba kuna [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yasaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii DRC

Kusikiliza / barabara nchini DRC

Kikundi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kimekamilisha ukarabati wa barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 600 kwenye ukanda ulioathiriwa na vita Mashariki mwa nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha amani na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mkuu wa ofisi ya MONUSCO jimbo la [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zambia yawapatia ukaazi wa kudumu wakimbizi wa Angola

Kusikiliza / wakimbizi wa Angola

Serikali ya Zambia imeanza kuwapatia hadhi ya ukaazi wa kudumu baadhi ya wakimbizi wa Angola nchini humo ambao wanakidhi vigezo vya uhamiaji. Mpango huo umeanza kufuatia usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na Umoja wa Afrika kwa kutoa dola Laki Moja kufanikisha mchakato huo wa kujumuisha wakimbizi wa Angola katika [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yatua kwa wakimbizi wa Rwanda huko Pakistani

Kusikiliza / wakimbizi wa Rwanda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza mpango wa kuwarejesha kwa hiari yao makwao kwa wakimbizi wa Rwanda walioko Pakistani. Wakimbizi hao ni wale walioingia nchini humo kwa shughuli mbali mbali ikiwemo masomo kama vilakini walishindwa kurejea nyumbani kutokana na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031