Nyumbani » 02/01/2013 Entries posted on “Januari 2nd, 2013”

Walioachiwa huru baada ya kutekwa na maharamia Somalia, wazungumza!

Kusikiliza / Mateka waliokuwa wanashikiliwa na maharamia wa kisomali

Kwa muda mrefu sasa huduma za usafirishaji wa mizigo katika pwani ya Somalia umekuwa ukikumbwa na visa vya mara kwa mara vya meli kutekwa nyara na maharamia ambapo mara nyingi maharamia hao hudai kulipwa pesa ili waweze kuwaachia wahusika hali inayosababisha hofu kubwa miongoni mwa wasafirishaji. Visa vya namna hiyo viliwakumba wafanyakazi waliokuwemo kwenye Meli [...]

02/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na vifo vya watu 61 huko Cote D'Ivoire

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon ametuma salamu za rambi rambi kwa serikali  ya Cote D'Ivoire na familia, jamaa na ndugu wa watu 61 waliopoteza maisha kufuatia kuibuka kwa kizazaa na msongamano baada ya sherehe za mwaka mpya huko Abidjan, nchini humo. Msemaji wa Ban amemkariri Katibu Mkuu huyo akisema kuwa amesikitishwa [...]

02/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado tuna wasiwasi mkubwa na hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati: UM

Kusikiliza / Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali ilivyo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na unaendelea kufanya mawasiliano na mwakilishi maaluma wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa nchini humo Margreth Voght. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo kuwa wakati wanaendelea na mawasiliano [...]

02/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Takwimu mpya zadokeza idadi ya vifo nchini Syria kuwa zaidi ya Elfu 60

Kusikiliza / Mji wa Homs Syria

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema takwimu mpya zinadokeza idadi ya watu waliokufa nchini Syria kutokana na mapigano yanayoendelea ni zaidi ya Elfu 60. Amesema upembuzi wa awali wa takwimu uliofanywa na wataalamu wa taarifa kwa niaba ya Umoja wa Mataifa umewezesha kukusanywa orodha ya watu [...]

02/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kemikali ya sumu au Aseniki iliyo kwenye maji yaweza kusababisha kansa

Kusikiliza / Maji yenye arseniki

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO, inasema uwepo wa kemikali ya sumu, aseniki katika maji ya kunywa na chakula kwa muda mrefu unaweza kusababisha saratani na vidonda vya ngozi.  WHO inasema aseniki imekuwa ikihusishwa na kuathiri vibaya ukuaji wa binadamu, ugonjwa wa moyo, uharibifu wa mfumo wa mishipa ya fahamu na ugonjwa wa [...]

02/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uturuki yafungua milango kwa wakimbizi wa Syria kujiunga na vyuo vikuu.

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria ambao sasa wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma nchini Uturuki

Uturuki imeanzisha programu ambamo kwayo wakimbizi wa Syria nchini humo wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma bila malipo yoyote ya ada. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema chini ya mpango huo wakimbizi wanaokidhi vigezo wataanza masomo yao kwenye vyuo vikuu saba mwezi Machi mwaka huu. UNHCR inasema hadi sasa wakimbizi [...]

02/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tumesikitishwa na vifo huko Cote d'Ivoire:UNOCI

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa huko Cote D'Ivoire Bert Koenders

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Côte d’Ivoire Bert Koenders ameelezea masikitiko yako kufuatia vifo vya watu 60 vilivyotokea saa chache baada ya kumalizika kwa mkesha wa mwaka mpya kwenye mji mkubwa zaidi nchini humo, Abidjan. Amesema vifo na majeruhi vilivyosababishwa na msongamano kwenye uwanja ambako sherehe za mwaka mpya zilikuwa [...]

02/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Jose Ramos-Horta kuwa mjumbe wake GUINEA –BISSAU

Kusikiliza / José Ramos-Horta na Katibu Mkuu Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Rais wa zamani wa Timor-Letse José Ramos-Horta kuwa mwakilishi wake maalumu nchini Guinea Bissau.Kwa wadhifa huo pia, Ramos-Horta anakuwa Mkuu wa ofisi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Joseph Mutaboba kutoka Rwanda ambapo imeelezwa kuwa Ramos-Horta kwa kushirikiana [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuimarisha amani nchini Somalia ni changamoto kubwa: Balozi Mahiga

Kusikiliza / mahiga-2

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesema bado kuna changamoto kubwa kufanikisha amani ya kudumu nchini Somalia na kwamba ndoto ianyotarajiwa ni nchi hiyo kuwa salama, ustawi na amani ndani yake na kati yake na jirani zaike. Taarifa zaidi na Alice Kariuki: (SAUTI YA ALICE KARIUKI)

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mateka waliookolewa kurejeshwa nyumbani: UNPOS

Kusikiliza / Meli ya MV Iceberg 1

 Umoja wa Mataifa kwa sasa unaongoza shughuli ya kuwarudisha makwao mateka waliookolewa hivi kutoka kwa maharamia wa kisomali baada ya miaka mitatu mikononi mwa maharamia hao. Mateka hao waliokolewa kufuatia oparesheni iliyochukua muda wa siku 15 iliyoongozwa na polisi wa baharini wa eneo la Puntland tarehe 23 mwezi Disemba mwaka uliopita. Mabaharia hao 24 ni wa [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada zaidi yahitajika Afghanistan

Kusikiliza / Afghanistan map

Hali mbaya ya usalama na kudorora kwa hali ya kibinadamu huenda vikaikumba Afghanistan mwaka huu wa 2013, yamesema mashirika ya kutoa misaada.  Mpango mpya wa kibinadamu wa mwaka 2013 uliochapishwa na Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA unasema kuwa kufuatia kuzoroteka kwa hali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wawili wa Jordan waliokuwa wametekwa sasa huru: UNAMID

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

  Walinda amani wawili wa Jordan waliotekwa wakati wakihudumu kwenye kikundi cha pamoja cha kulinda amani Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID wameachiwa huru baada ya kuwa matekani kwa siku 136. Msemaji wa UNAMID, Aicha Elbasri amesema kwa sasa wako salama na wanaelekea mji mkuu wa Sudan, Khartoum na baadaye watakwenda [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yatoa majibu ya uchunguzi dhidi ya FDLR na uvumi mwingine huko Kivu Kaskazini

Kusikiliza / Kivu Kaskazini

 Kundi la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MUNUSCO lililotumwa kubaini uvumi wa kuwasili kwa kundi la FDLR kutokaZambiakwenda mikoa ya Kivu ya Kaskazini wanasema kuwa uvumi huo si ukweli. Kupitia taarifa ya MONUSCO ni kwamba wameshirikina na jeshi la DRC miaka iliyopita kwa minajili ya kupunguza uwezo wa makundi [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930