Nyumbani » 31/01/2013 Entries posted on “Januari, 2013”

Feltman azungumzia uchaguzi mkuu wa Kenya 2013-01-31

Jeffrey Feltman

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa ambaye pia ni msimamizi  mkuu wa masuala ya siasa ndani ya Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amekuwa na mazungumzo na viongozi nchini Kenya ambapo ametaka uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwezi Machi mwaka huu ufanyike kwa uwazi na kwa amani. Feltman ambaye amekutana na viongozi wa tume [...]

31/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya polisi wa kike kwenye Umoja wa Mataifa iongezwe: ORLER

Kusikiliza / Ann-Marie Orler, Mshauri Mkuu wa masuala ya polisi ndani ya UM anayemaliza muda wake

Mshauri mkuu wa masuala ya polisi kwa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake Ann- Marie Orler ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja huo kutuma polisi zaidi wa kike wenye sifa za juu kuhudumu kwenye oparesheni zake. Orler ambaye mtaalamu wa sheria amesema mwaka 2009 Umoja wa Mataifa ulizindua mpango mahsusi wa kuongeza idadi ya [...]

31/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM kuhusu vifungo vinavyokiuka haki wakamilisha ziara Ugiriki

Kusikiliza / HRC

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu vifungo vinavyokiuka haki za binadamu limekamilisha ziara yake nchini Ugiriki, ambayo ilitekelezwa kwa lengo la kukagua hali ya watu kunyimwa haki zao nchini humo. Kundi hilo la wataalam huru lililoteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu, lilizuru vituo kadhaa [...]

31/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Angola yatangaza kuchangia kwenye mfuko wa Africa Solidarity Trust Fund

Kusikiliza / msaada

Taifa la Angola limesema kuwa litatoa mchango wake kwa mfuko wa Africa Solidarity Trust, kwa minajili ya jitihada za kuangamiza njaa barani Afrika. Rais José Eduardo Dos Santos alitoa tangazo hilo kwenye mkutano uliofanyika mjini Luanda, na ambao ulihudhjuria pia na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa FAO, José [...]

31/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay apongeza kampeni ya kutokomeza mila ya kuwanyanyasa wanawake India

Kusikiliza / akina mama wa India

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navi Pillay amekaribisha taarifa za kampeni ya kutokomeza mila ya kuondoa taka hususan kutapisha vyoo kwa mikono, na ambayo inayotumika kuwakandamiza wanawake ambayo pia inatajwa kuwanyanyapaa. Ikijulikana kama "utapishaji vyoo kwa mikono mila hiyo inahusisha kuondoa uchafu wa vyooni na kusafisha mabomba ya kupitisha uchafu [...]

31/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasifu mchango wa wahisani wa dola Bilioni 1.5 kwa Syria

Syria

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, António Guterres amesifu nchi wahisani kwa mchango wao wa zaidi ya dola Bilioni Moja na Nusu kusidia raia wa Syria waliojikuta katika maisha ya ukimbizi baada ya mgogoro kukumba nchi yao. Amesema mchango huo uliotokana na mkutano wa Kuwait ni wa kipekee na [...]

31/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulowezi wa Israeli ni ishara ya ukosefu wa haki kwa Wapalestina: Ripoti

Kusikiliza / Israel

Ripoti mpya ya ujumbe wa kimataifa wa kuhakiki hali katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa imedhihirisha jinsi ulowezi wa Waisraeli unavyoathiri haki za Wapalestina. Ripoti hiyo ambayo imechapishwa leo, inasema kuwa ulowezi huo umechangia ukiukaji wa haki za Wapalestina kwa njia nyingi. Ripoti inasema kuwa ukiukaji huo una uhusiano wa moja kwa moja, na unaonyesha mwenendo [...]

31/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Plumbly atembelea kambi ya Ain El-Hilweh huko Lebanon

Kusikiliza / Mazungumzo kati ya Bwana Plumbly na wawakilishi wa vikundi kwenye kambi ya Ain El-Hilweh

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Lebanon Derek Plumbly leo ametembelea kambi ya Ain El-Hilweh kusini mwa Lebanon ambapo amejionea mazingira magumu ambamo wanaishi wakimbizi wakiwemo wale wa kipalestina waliokimbia mgogoro Syria. Katika ziara hiyo ambapo Bwana Plumbly aliambatana na Ann Dismor, Mkurugenzi wa UNRWA nchini Lebanon, ameshuhudia vile ambavyo wanawake na watoto wanavyoishi [...]

31/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yabuni vyombo vya kuongeza mazingira salama katika hospitali za Afrika

Kusikiliza / WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO), leo limetoa fungu la vyombo vitakavyotumiwa kwa minajili ya kuboresha usalama wa wagonjwa hospitalini katika nchi zinazoendelea. Fungu hilo la vyombo muhimu limebuniwa kwa ushirikiano wa wataalam wa afya kupitia mpango wa WHO wa ushirikiano wa African Partnerships for Patient Safety (APPS), ambao unaweka hospitali kumi na nne kutoka barani [...]

31/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumejizatiti kuisaidia Somalia: UM

Kusikiliza / feltman1

Umoja wa Mataifa umejizatiti kusaidia Somalia kujenga amani ya kudumu, na hiyo ni kauli ya Mkuu wa masuala ya siasa ndani ya Umoja wa Mataifa Jeffery Feltman ambayo aliitoa mara baada ya mazungumzo yake na vinogozi wa nchi hiyo mjini Mogadishu. Feltman licha ya kuonyesha wasiwasi wake juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za [...]

31/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Brahimi ataja vikwazo vya utatuzi wa mgogoro wa Syria

Kusikiliza / Lakdhar Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi amesema kitendo cha pande mbili kwenye mzozo huo kutozungumza kabisa kinafanya utatuzi kuwa mgumu. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani, Brahimi amesema kila upande ina mtazamo wake [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO kuisaidia Mali kukarabati na kuokoa maeneo ya urithi wa dunia

Kusikiliza / Eneo la urithi wa dunia, Timbuktu, Mali

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokova, ametangaza kuwa shirika hilo litaisaidia nchi ya Mali kukarabati na kurejesha maeneo yake ya urithi wa kiasili, ambayo ameyataja kuwa sehemu muhimu ya historia na utamaduni wa nchi hiyo. Bi Bokova ametoa wito kwa wadau wote wa UNESCO kuunga mkono juhudi za ukarabati [...]

30/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kujadili umuhimu wa uongozi wa kisheria

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili umuhimu wa kuimarisha uongozi wa kisheria kama njia ya kuendeleza amani na usalama wa kimataifa. Akilihutubia Baraza hilo wakati wa kufungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amesema kuhakikisha haki na usalama kupitia uongozi wa kisheria ni njia mwafaka ya [...]

30/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu Ulaya wanakata tamaa kufuatia mdororo wa kiuchumi: IFRC

Kusikiliza / nembo ya IFRC

Wakati bara la Ulaya likiwa bado linakumbwa na mdororo wa kiuchumi, Shirikisho la mashirika ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC) limeonya kuwa mamilioni ya watu ambao wameathiriwa na ukosefu wa ajira, ongezeko la umaskini, kupoteza makazi na hali ya sintofahamu kuhusu hatma yao huenda wakakata tamaa. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zaidi [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Athari za kimbunga Msumbiji, mama ajifungulia juu ya paa: OCHA

Kusikiliza / mafuriko Mozambique

Kimbunga Felling kimezidi kusababisha madhara huko Msumbiji wakati huu inapotolewa hadhari kuwa kinasonga kaskazini ambapo licha ya zaidi ya watu 48 kupoteza maisha na nyumba kuharibiwa za wakazi 250,000, mwanamke mmoja mjamzito amejikuta akijifungulia juu ya paa la nyumba. Mama huyo aliyetambulika kwa jina la Hortensia ni mkazi wa wilaya ya Chokwe nchini Msumbiji, moja [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ongezeko la wanaouawa na askari wa Israel latia wasiwasi UM

Kusikiliza / Israel

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa  James W. Rawley ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongeza kwa watu wanaouawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan. Imeripotiwa kuwa tangu mwezi Novemba mwaka jana raia wanane wa kipalestina wakiwemo watoto watatu na mwanamke mmoja wameuawa katika visa tofauti [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumieni mkutano kuonyesha mnawajali raia wa Syria: Amos

Kusikiliza / Syria OCHA

Mkuu wa shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, Valerie Amos amewasihi washiriki wa mkutao wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait kutumia fursa ya mkutano huo kuonyesha kuwa wanajali na kushirikiana kuwasaidia wananchi wa Syria. Bi. Amos amesema mahitaji nchini Syria ni makubwa. Ametoa mfano kuwa nusu ya [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukata wa bajeti usikwamishe mchango kwa Syria: Ban

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa UM.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika mkutano wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait na kusema kuwa mazingira magumu yanayokumba wasyria hayawezi kuachwa yaendelee licha ya kwamba serikali mbali mbali duniani zinakumbwa na ukata. Amesema anatambua hali ngumu ya uchumi lakini ombi la dharura la dola Bilioni Moja na Nusu [...]

30/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utata uliopandikizwa kwenye tamko la Geneva juu ya Syria uondolewe: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi amelieza Baraza la Usalama kuwa hali ya Syria ni mbaya na kwamba anaona aibu vile ambavyo kila wakati amekuwa akirejea kauli hiyo bila hatua dhahiri kuchukuliwa. Bwana Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari [...]

29/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaimarisha usaidizi wake kwa watoto huko CAR

Kusikiliza / Watoto Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaimarisha operesheni zake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia maelfu ya watoto wanaohitaji misaada ya dharura baada ya kujikuta katikati ya mzozo unaoendelea hivi sasa nchini humo. Mwakilishi wa UNICEF nchini huko Souleyman Diabate amesema wamebaini maeneo ambako watoto wameathirika zaidi ni pamoja na [...]

29/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM laahidi kuwaunga mkono wananchi wa Haiti

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamewahakikishia wananchi wa Haiti kwamba jamii ya kimataifa imejitolea kuunga mkono jitihada zao za kutafuta amani , uthabiti pamoja na maendeleo. Hii ni kupitia taarifa iliyotolewa na Rais wa baraza hilo Masood Khan inayojiri baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mwakilishi mkuu wa katibu mkuu wa [...]

29/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

29/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNHCR yajiandaa kuwasaidia walio na nia ya kurejea makwao nchini Mali

Kusikiliza / mtoto wa Mali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linajianda kuwasaidia wale waliohama makwao kaskazini mwa nchi na walio na nia ya kurejea kwa hiari wakati hali inapoendelea kubadilika nchini Mali. UNHCR inasema kuwa ina mpango wa kufungua ofisi zake mjini Gao na kwenye miji mingine eneo la kaskazini hivi karibuni hata kama [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Libya bado si nzuri: Mitri

Kusikiliza / Tarek Mitri

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Tarek Mitri amelihutubia Baraza la Usalama hii leo mjini New York, Marekani na kueleza kuwa hali ya usalama nchini Libya bado ni mbaya na jitihada za kuimarisha usalama zinaendelea. Bwana Mitri amesema licha ya kuwepo kwa maendeleo thabiti katika baadhi ya sekta ikiwemo kurejesha [...]

29/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO yaonya uwezekano wa kutokea tena homa ya mafua ya ndege

Kusikiliza / homa ya mafua ya ndege

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya juu ya kitisho cha kuzuka tena ugonjwa wa mafua ya ndege ulioikumba dunia mwaka 2006 na limetaka kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kudhibiti kutojirejea kwa hali hiyo. FAO imesema kuwa wakati dunia ikiendelea kuhangaika na mikwamo ya kiuchumi, kuna kiasi kidogo cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya kushughulikia kutojitokeza [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yarejesha huduma za usambazaji wa chakula mjini Kismayo

Kusikiliza / wfp food sacks

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza tena usambazaji wa msaada wa chakula kwenye mji wa Kismayo ulio kusini mwa Somalia ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita. Mizozo pamoja na ukosefu wa usalama vimekuwa vikiizuia WFP na mashirika kadhaa ya kutoa misaada ya kibinadamu kufanya kazi katika eneo [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lishe bora ya watoto Syria izingatiwe hata wakati huu wa mzozo: UM

Kusikiliza / kunyonyesha watoto Syria

Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali yametaka wote wanaohusika na usaizidi wa wasyria waliopotea makazi yao na kukimbilia nchi jirani za Jordan, Lebanon, Iraq na Uturuki kuepusha magonjwa na vifo vya watoto visivyo vya lazima vinavyotokana na kuwapatia watoto wachanga lishe mbadala badala ya maziwa ya mama. Mashirika [...]

29/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awasili Kuwait, atoa shukrani kwa maandalizi ya mkutano wa Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko nchini Kuwait tayari kushiriki mkutano wa wahisani kwa ajili ya Syria hapo kesho. Tayari Bwana Ban amekuw ana mazungumzo na viongozi wa wa nchi hiyo akiwemo Mfalme wa nchi hiyo, Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Mambo ya Nje. Katika mazungumzo yao pamoja na [...]

29/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka majadiliano ya dhati Misri ili kuepusha maafa zaidi

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navyi Pillay amesema kumekuwa na hali ya wasiwasi kufuatia kuongezeka kwa matukio ya mauaji ya watu na kushamiri kwa vurugu kunakoshuhudiwa sasa nchini Misri na amezita pande zote kuanzisha majadiliano ili kuondokana na hali hiyo. Pia Pillay ameitolea wito serikali ya Misri kutafakari upya njia [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Askari waripotiwa kunyanyasa raia huko Kivu Kaskazini

DRC kivu

Usalama wa raia kwenye jimbo la Kivu Kaskazini huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC bado ni wasiwasi mkubwa ambapo raia wanakumbwa na manyanyaso kutoka kwa askari. Jarida la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa limewakariri wataalamu wa elimu na ulinzi wa mtoto wakitaja manyanyaso hayo kuwa ni pamoja na zaidi ya [...]

29/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jimbo la Equateur, DRC lakumbwa na Surua, 11 wafariki dunia: UNICEF

Kusikiliza / UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Surua kwenye jimbo la Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Limesema ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe Mosi mwezi huu wagonjwa zaidi ya Mia Moja wamebainika ambapo Kumi na Mmoja wamefariki dunia. UNICEF imesema kwa kushirkiana na shirika la afya duniani [...]

29/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

  Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule. Maelfu ya watu kwa sasa hawana makazi na wanahitaji msaada ambapo shrika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na idara ya ulinzi wa raia nchini Zimbabwe wameitikia wito wa kutoa [...]

28/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Bado hatujaweza kufikia maeneo yote Syria: OCHA

Kusikiliza / John Ging, Mkuu wa Operesheni- OCHA

Mkuu wa operesheni katika Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu,  OCHA, John Ging amesema hali  ya Syria bado inazidi kudorora kadri siku zinavyosonga na kwamba bado hawajapata kibali cha kuweza kuvuka eneo la mzozo na kuwafikia awle wote wanaohitaji misaada. Bwana Ging amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kuwa wakati [...]

28/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Marais na wanasoka wapaza sauti dhidi ya Malaria

Kusikiliza / CAF- Malaria

Afrika Kusini, mwenyeji wa mwaka huu wa fainali za kombe la mataifa barani AFrika, AFCON. Wakati wachezaji wakipasha misuli yao kulinda nyavu zao, mbu nao wanavinjari kwa lengo la kuwamaliza nguvu.. Malaria na ndio maana Mpango wa kudhibiti Malaria na kampeni ya pamoja dhidi ya Malaria wametoa ujumbe huu mahsusi kwa lengo la kutokomeza Malaria!

28/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wajawazito waona mwanga Somalia

Kusikiliza / akina mama wajawazito

Taifa la Somalia linazidi kuimarika kila uchwao baada ya kuundwa kwa serikali mwaka jana. Huduma za kijamii ikiwemo za kiafya zinazidi kuimarika. Hii imewezesha hata wajawazito ambao awali walikuwa wanajifungulia majumbani, kupata huduma hizo kwenye hospitali chini ya uangalizi wa madaktari, wauguzi na wakunga wenye uzoefu an vifaa. Kitendo hiki kinaokoa siyo tu maisha ya [...]

28/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa WHO afariki dunia

hiroshi-nakajima

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Dkt. Hiroshi Nakajima amefariki dunia nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa muda mfupi.Alikuwa na umri wa miaka 84. Taarifa za kifo hicho zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa WHO Dr. Margaret Chan ambaye amemwelezea Nakajima kama mtu aliyojitoa kwa dhati na kulitumikia shirika hilo kwa [...]

28/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mafuriko Msumbiji yasababisha wengi kukosa makazi

Kusikiliza / waathiriwa wa mafuriko Mozambique

Serikali ya Msumbiji kwa kushirikiana na mashirika ya misaada imeanzisha juhudi za kuwanusuru mamia ya wananchi ambao wameathiriwa kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba taifa hilo. Kiasi cha watu 150,000 wanahitaji msaada wa dharura baada ya makazi yao kuharibiwa na mafuriko yaliyotokea katika jimbo la Gaza, lililoko kusini mwa nchi hiyo. Mamia ya manusura wa mafuriko [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KASMO FM mkombozi wa wanawake Somalia

Kusikiliza / KASMO

Kwa mara ya kwanza Somalia inapata kituo cha Radio kinachosimamiwa na kuendeshwa na wanawake, KASMO FM. Radio hiyo itazinduliwa rasmi mjini Mogadishu, Somalia tarehe Tatu mwezi Machi mwaka huu ambayo ni siku ya wanawake duniani na kuanzishwa kwake kunatokana na msaada wa UNESCO. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu wa UM asikitishwa na vifo vya vijana kwenye klabu: Brazil

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kuhuzunishwa kwake na vifo vya mamia ya vijana vilivyotokea kwenye klabu moja ya usiku kwenye mji wa Santa Maria, Rio Grande do Sul nchini Brazili. Bwana Ban amekaririwa akieleza kushtushwa zaidi na vifo hivyo kwa kuwa vimehusisha vijana ikiwemo wanafunzi vya vyuo vikuu ambao wamekufa kutokana [...]

28/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu Syria yazidi kudorora

Kusikiliza / baridi, Syria

Umoja wa Mataifa unasema hali ya kibinadamu nchini Syria inazidi kudorora kila uchwao ambapo watu Milioni Nne wanahitaji msaada wa kibinadamu. Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema baridi kali imeongeza madhila ya watu hususan wale waliohama makwao kutokana na mgogoro unaoendelea nchini mwao na sasa wanaishi kwenye makazi ya [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna maendeleo endelevu kama kuna njaa: FAO

Kusikiliza / Graziano Da Silva

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO Graziano Da Silva anasema kuwa hakutakuwepo na maendeleo ya kudumu duniani ikiwa watu wataendela kuhangaishwa na njaa. Akizungumza kwenye mkutano wa jumuia ya nchi za Amerika kusini, Carribean na Ulaya, Da Silva amesema kuwa mataifa sasa yana fursa ya kutoa mapendekezo kuhusu [...]

28/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa yaomba dola milioni 471 kwa ajili ya Afghanistan

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Afghanistan

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa watoto 165 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakufa kila siku huku mama mjamzito mmoja akifariki dunia kila baada ya saa mbili nchini Afhanistan. Taarifa hiyo ya OCHA inalenga kuonyesha jinsi hali ya kibinadamu inavyozidi kuzorota nchini Afghanistan. Inaongeza kuwa [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Somalia, DRC, Madagascar, Zimbabwe zamulikwa huko Addis Ababa

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Afrika ambapo wamefanya mashauriano kuhusu masuala kadhaa ikiwemo yua kiuchumi, kisiasa na kijamii. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. Miongoni mwa viongozi aliokutana nao Bwana Ban ni Paul Kagame wa Rwanda ambapo wamejadili hali ya usalama katika nchi za Maziwa Makuu na amepongeza Rwanda [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bara la Afrika linasonga mbele: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono maendeleo barani Afrika ikiwemo masuala ya utawala bora na haki za binadamu ambapo amesema mtazamo wake ni kwamba bara hilo linaibuka na kusonga mbele. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, Ethiopia, Bwana Ban ametoa mfano wa harakati za Afrika za kupambana na magonjwa [...]

28/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asisitiza haja ya bara la Afrika kuwajibika kwa siku zake zijazo

Kusikiliza / Ban-ki-moon11

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema bara la Afrika lina uzoefu wa kulitosheleza kupata suluhu kwa changamoto zake, pamoja na kuchangia malengo ya kimataifa ya ukuaji unaowahusisha wote, haki ya kijamii na kulinda mazingira. Bwana Ban amesema hayo katika hotuba yake kwa viongozi wa Afrika, wakati wa mkutano wa kila mwaka wa [...]

27/01/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Ban asifu waliojitolea kuwaokoa wahanga wa mauaji ya kimbari ya wayahudi

Kusikiliza / Holocaust

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amesema siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya waliokufa kwenye mauaji ya kimbari ya kiyahudi inatoa fursa ya kutambua mchango wa wale waliojitolea uhai wao kuokoa wahanga wa mauaji hayo licha ya mazingira magumu. Bwana Ban amesema hayo kwenye ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video wakati [...]

25/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa Mali wazidi kutandaa Afrika Magharibi: Djinnit

Kusikiliza / Said Djinnit

Mgogoro unaoendelea nchini Mali unazidi kutandaa na madhara yake kughubika eneo la Afrika Magharibi na Ukanda wa Sahel. Hiyo ni kauli ya leo Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Afrika Magharibi, UNOWA, Said Djinnit wakati akilipatia Baraza la Usalama hali halisi ya mgogoro huo ambapo amesema hali ilivyo inadhihirisha utete wa eneo hilo. [...]

25/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF yahitaji dola Bilioni 1.4 kusaidia watoto wenye mahitaji

Kusikiliza / mtoto wa Iran

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ombi maalum la dola Milioni Moja nukta Nne kwa ajili ya kuokoa watoto wanaokumbwa na madhila kwenye nchi 45 duniani kote kwa mwaka huu wa 2013. Watoto hao wamejikuta mtegoni kutokana na majanga yanayoendelea kwenye nchi zao ikiwemo migogoro, majanga ya asili na mazingira mengine [...]

25/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya kusaka amani ya Darfur yaanza kupiga hatua

Kusikiliza / Edmond Mulet

Wakati mazungumzo ya kusaka amani baina ya serikali ya Sudan na kundi moja la waasi kuhusiana na mzozo wa Darfur yanaendelea kupiga hatua huko Doha, Umoja wa Mataifa umeitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuendelea kutupia macho kwa karibu ili kusaidia kutanzua mkwamo huo. Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la [...]

25/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Burundi yaitikia wito wa kutokomeza Surua

Kusikiliza / surua, Burundi

Shirika la afya duniani, WHO mapema mwezi huu lilitangaza kupungua kwa idadi ya vifo vitokanavyo na Surua kwa asilimia 71 kati ya mwaka 2000 na 2011 duniani, lakini ugonjwa huo bado ni tishio katika baadhi ya maeneo. WHO ilipendekeza kila mtoto apate vipimo viwili vya chanjo dhidi ya Surua ambapo imesema Jamhuri ya Kidemokrasi ya [...]

25/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay aisifu ripoti ya ukatili dhidi ya wanawake India

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amekaribisha ripoti ya Kamati ya Verma kama msingi wa kuchukua hatua kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake nchini India, na kutoa wito kwa serikali ya India kutekeleza mapendekezo ya ripoti hiyo. Bi Pillay ameipongeza kamati hiyo kwa kuichapisha ripoti hiyo ya kina haraka, [...]

25/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatiwa wasiwasi na visa vya utekaji nyara mashariki mwa Sudan

Kusikiliza / utekaji nyara mashariki mwa sudan

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kumeripotiwa ongezeko kwa visa vya utekaji nyara na kutoweka kwa watu hasa wakimbizi kutoka Eritrea miongoni mwa makabila yaliyo eneo la mpaka mashariki mwa Sudan visa ambavyo vinashuhudiwa ndani ya kambi ya wakimbizi. UNHCR inasemna kuwa kwa muda wa miaka miwili iliyopita wameshuhudi watu [...]

25/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatoa ombi la msaada kwa wakimbizi nchini Mali

Kusikiliza / wakimbizi wa Mali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kwa mara nyingine limetoa ombi la msaada wa kimataifa wa kuwasaidia maelfu ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao kutoka ma mapigano yanayoendelea nchini Mali. Tangu kuanza kwa mapigano kaskazini mwa Mali mwaka mmoja uliopita, zaidi ya wakimbizi 150,000 wamekimbilia mataifa jirani yakiwemo Mauritania, Niger na Burkina [...]

25/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaiomba Kenya ifikirie upya uhamishaji wa wakimbizi kutoka mijini

Kusikiliza / kambi ya wakimbizi nchini Kenya

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limekuwa kwenye mazungumzo na serikali ya Kenya tangu mwezi Disemba baada ya serikali ya Kenya kutangaza kusitisha shughuli ya kuwapokea na kuwaandikisha watafuta hifadhi mjini Nairobi na miji mingine nchini Kenya ikisema kuwa watu hao watapelekwa kwenye kambi za wakimbizi. UNHCR ilielezea wasi wasi wake kutokana na [...]

25/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi yahitaji msaada zaidi kuimarika: UM

Kusikiliza / hali ya umaskini nchini Burundi

Taifa la Burundi linaendelea kupiga hatua katika kuimarisha uongozi na kujikwamua tena kufuatia mizozo ya mara kwa mara, lakini bado linahitaji msaada kutoka jamii ya kimataifa ili kukabiliana na hali tete kisiasa na umaskini. Haya yamesemwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Parfait Onanga-Anyanga, akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Bwana [...]

25/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Kusikiliza / Mafuriko Zimbabwe yaharibu miundombinu

Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule. Maelfu ya watu kwa sasa hawana makazi na wanahitaji msaada ambapo shrika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na idara ya ulinzi wa raia nchini Zimbabwe wameitikia wito wa kutoa misaada [...]

25/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awapa hongera Wamisri kwa miaka miwili tangu mapinduzi

Kusikiliza / Waandamanaji Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amepeleka salamu za heko kwa raia wa Misri, wakati wakiadhimisha miaka miwili tangu mapinduzi yaloing'oa serikali ya Hosni Mubarak mamlakani.  Bwana Ban ameelezea kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kuwaunga mkono watu wa Misri na serikali yao kujenga mifumo ya kidemokrasia inayowahusisha wote. Amewahimiza waendelee kushabikia kanuni za [...]

24/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Ban huko CAR azungumzia azimio la Baraza la Usalama.

Kusikiliza / Margaret Voght, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM huko CAR na Mkuu wa BINUCA

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Margaret Vogt amezungumza na waandishi wa habari kwa nchi ya video kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bangui na kusifu azimio la Baraza la Usalama ambalo amesema linasisitiza umuhimu wa ofisi yake kutoa usaidizi wa utekelezaji wa makubaliano ya Libreville. [...]

24/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa ofisi yake huko CAR

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa ofisi yake ya ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, BINUCA huku ikitaka serikali na vikundi vya upinzani kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na mengineyo yenye lengo la kurejesha amani nchini humo. BINUCA imeongezewa muda hadi tarehe 31 mwezi Januari mwakani ambapo kupitia [...]

24/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mali na Syria zatawala hotuba ya Ban huko Davos

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Hali ya amani nchini Mali na Syria zinazidi kuzorota na hivyo tuchukue hatua haraka kwa pamoja, na huo ndio ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa viongozi mbali mbali wa dunia wanaohudhuria jukwaa la uchumi huko Davos Uswisi. Katika hotuba yake Ban amesema migogoro hiyo inahatarisha usalama siyo tu wa nchi [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Raila Odinga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi huko Davos, Uswisi. Bwana Ban na Bwana Odinga wamezungumza kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Kenya ujao mwaka huu, pamoja na haja ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IMF yatabiri ukuaji wa uchumi mwaka 2013

Kusikiliza / construction-worker

Shirika la fedha duniani IMF limesema kuwa kutakuwepo na ukuaji wa uchumi duniani mwaka huu wa 2013 wakati vizingiti kwenye masuala ya uchumi vinaporegea mwaka huu. Lakini hata hivyo IMF inasema kuwa ukuaji huo utakuwa wa mwendo wa kinyonga ikiongeza kuwa sera ambazo zitatumika ni lazimea zihakikishe kuwepo ukuaji. Ripoti hiyo inaeleza kuwa sera zilizotumika [...]

24/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yatoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa Global Fund

Kusikiliza / Global-Fund

Jamhuri ya Ujerumani imetoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa kimataifa wa kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria, yaani Global Fund, ili kuwasaidia wahudumu wa afya kuendeleza juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa haya hatari ya kuambukiza. Tangazo la mchango huo limetolewa leo na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban afanya mashauriano na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Bwana Ahmet Davutoğlu mjini Davos, Uswisi, ambako kongamano la kimataifa kuhusu uchumi linaendelea. Bwana Ban na Waziri Davutoğlu wamebadilishana mawazo kuhusu mzozo wa Syria, na uwezekano wa suluhu la kisiasa. Katibu Mkuu ameelezea shukran [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yazindua ukusanyaji maoni kupitia mtandao wa Intaneti

Kusikiliza / UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na UKIMWI, UNAIDS, limefungua ukurasa huru wa mawasiliano ya kimtandao kwa shabaha ya kukusanya maoni toka pande zote za dunia, mawazo ambayo yatatumika kuratibu njia mpya za kukabiliana na tatizo la UKIMWI duniani. Zoezi hili la kukusanya maoni kwenye intaneti litaendeshwa kwa muda wa wiki mbili, na kukamilika mnamo [...]

24/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa ufadhili wa Marekani kwa UNICEF watoa ombi la msaada kwa watoto wa Syria

Kusikiliza / watoto, Syria

Mfuko wa ufadhili wa serikali ya Marekani kwa Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, umetoa ombi la msaada wa dharura kwa watoto wa Syria, ambao wameathiriwa na mapigano na msimu wa baridi. Ripoti za hivi karibuni zimeelezea jinsi watoto wa Syria wanavyoathirika zaidi na mzozo huo. Miongoni mwa takriban watu milioni mbili [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaungana na wadau kuzindua mkakati wa ‘lisha mwili, lisha ubongo”

Kusikiliza / nourishing

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuanzia lile linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la kuhudumia watoto UNICEF, yamekusanya nguvu kwa pamoja ili kuwasaidia mamia ya watoto wanaokabiliwa na hali ngumu. Mpango huo wa miaka mitatu uliotangazwa kwenye kongamano la kitamaifa la uchumi linalofanyika Davos, Uswis [...]

24/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya fidia ya UM yatoa dola bilioni 1.3 kwa taifa la Kuwait

Kusikiliza / mafuta yaliyochomwa

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya fidia imewasilisha jumla ya dola bilioni 1.3 kwa serikali ya Kuwait. Fedha hizo ambazo ni deni zinafikisha jumla ya dola bilioni 40.1 ambazo zimelipwa na tume hiyo zikiwa ni kati ya dola bilioni 52.4 zilizolipwa kwa zaidi ya serikali 100 na mshirika ya kimataifa na ambazo [...]

24/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yasifu uamuzi wa Rwanda kukubali matumizi ya ndege zisizo na rubani

Kusikiliza / Madnodje Mounoubai

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC (MONUSCO) umepongeza uamuzi wa Rwanda wa kuungana na Uganda na DRC juu ya matumizi ya ndege zisizo na rubani mpakani mwa nchi hizo tatu. Msemaji wa MONUSCO, Madnodje Mounoubai amesema kufuatia makubaliano hayo anatumai kutakuwepo na maendeleo. Amesema mapendekezo ya [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani kufungwa kwa Mhariri Thailand

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu Navy Pillay amelaani vikali hukumu iliyotolewa kwa mhariri na mwanaharakati wa haki za binadamu Somyot Pruksakasemsuk nchini Thailand, akisema kuwa hukumu hiyo ni ya kuudhi, katili na inakwaza juhudi za utetezi wa haki za binadamu katika nchi hiyo. Mamlaka ya Thailand imemhukumu mhariri huyo [...]

23/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji wa kimataifa kupanda 2013 na 2014: UNCTAD

Kusikiliza / unctad_logo_copy

Uwekazaji wa kimataifa wa moja kwa moja ulishuka kwa asilimia 18 mwaka 2012 sawia na kiwango kilichoshuhudiwa mwaka 2009 hali ambayo inachangiawa zaidi kutokana na kutokuwepo uhakika miongoni mwa wawekezaji. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD. Hata hivyo uwekezaji wa kimataifa unatarajiwa kuongezeka mwaka [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati yaongezeka: ILO

Kusikiliza / wafanyakazi wa kipato cha kati

Shirika la kazi duniani, ILO linasema kuwa idadi ya wafanyakazi wa kipato cha kati kwenye nchi zinazoendelea imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita. Ripoti ya ILO kuhusu mwelekeo wa ajira kwa mwaka 2013 inasema kuwa kitendo hicho kinaweka mazingira yanayohitajika zaidi kwa ukuaji wa uchumi na ongezeko la matumizi kwenye nchi hizo. Takwimu [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sioni mwelekeo wa dhati huko Mashariki ya Kati: Serry

Kusikiliza / Robert Serry

Mratibu maalum wa Umoja wa Taifa katika mchakato wa amani huko Mashariki ya Kati, Robert Serry ameeleza wasiwasi wake juu ya kukosekana kwa mwelekeo wa dhati na bayana wa mchakato wa amani mashariki ya kati baina ya Israeli na Palestina. Bwana Serry ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu amesema hayo katika taarifa yake [...]

23/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wabunge wa nchi za makuu wajadili amani kwenye ukanda wao

Kusikiliza / Baadhi ya maspika wa mabunge ya nchi za Maziwa Makuu

Mkutano wa tatu wa wabunge wa nchi za maziwa makuu umeanza leo huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC ambapo washiriki kutoka nchi 12 za maziwa makuu wanataka kuwepo kwa amani ya kudumu kwenye maeneo ya migogoro ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mashariki mwa DRC, na baina ya Sudan na Sudan Kusini. Katibu [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta ya Kilimo Syria taabani: UM

Kusikiliza / ukulima, Syria

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokwenda Syria kujionea hali halisi umeeleza kuwa mapigano yanayoendelea nchini humo yameathiri uzalishaji wa kilimo na hivyo msaada zaidi unahitajika maeneo ya vijijini. Miongoni mwa waliokuwemo kwenye ujumbe huo ni Mkurugenzi wa idara ya dharura na ukarabati kutoka shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO, Dominique Burgeon [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya chakula Myanmar shwari isipokuwa maeneo yaliyokumbwa na mikasa

Kusikiliza / myanmar map

Umoja wa Mataifa unasema kuwa hali ya chakula nchini Myanmar imeimarika isipokuwa katika maeneo yaliyokumbwa na madhila ya mafuriko na mapigano ya kikabila mwaka jana. Jarida la taarifa za hali ya kibinadamu linasema kuwa maeneo hayo ya Rakhine, Kachin na Shan Kaskazini yana maelfu ya watu waliopoteza makazi kutokana na madhila hayo mwezi Juni na [...]

23/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya ya WHO yaonyesha uhaba wa huduma za afya Syria

Kusikiliza / unhcr-syria

Sita kati ya kila hospitali kumi na tatu, ikiwemo hospitali kuu ya umma katika jimbo la Homs nchini Syria, hazina huduma za matibabu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya hali ya afya katika muktadha wa mzozo nchini humo, ambayo imetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO. Ili kuwezesha huduma za afya, shirika la [...]

23/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AFISMA wanahitaji vifaa haraka: Feltman

Kusikiliza / Msimamizi mkuu wa masuala ya siasa ndani ya UM, Jeffrey Feltman

Msimamizi mkuu wa masuala ya kisiasa ndani ya Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amesema kwa kuwa tayari maafisa na askari wanaounda jeshi la Afrika huko Mali, AFISMA  wameanza kuwasili nchini humo, kinachotakiwa hivi sasa ni usaidizi haraka wa vifaa ili waweze kukabiliana na hali halisi. Feltman amesema hayo wakati akitoa taarifa ya  hali ilivyo huko [...]

22/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza lapitisha azimio dhidi ya DPRK, Ban aunga mkono

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio la kushutumu vikali kitendo cha Jamhuri ya kidemokrasia yaWatu wa Korea, DPRK cha kurusha roketi kwa kutumia teknolojia ya makombora ya masafa marefu mwezi Disemba mwaka jana. Azimio hilo namba 2087 limepitishwa Jumanne baada ya mjadala wa wazi ambapo wajumbe wote wamesisitiza msimamo [...]

22/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utupaji na upotevu wa chakula sasa basi: UM

Kusikiliza / food 2

Katika harakati za kuona kuna uhakika wa chakula duniani, kampeni mpya imeanzishwa kuepusha upoteaji au utupaji wa chakula. Kampeni hiyo inayoendeshwa na shirika la chakula na Kilimo duniani, FAO na lile la mazingira, UNEP kwa kushirikiana na wadau wao inazingatia kuwa maelfu ya Tani za chakula hupotea na kusababisha hasara ya dola Trilioni Moja. Je [...]

22/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban aorodhesha mambo ya kipaumbele katika ajenda ya mwaka 2013

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ameliambia Baraza Kuu la Umoja huo kwamba, masuluhu ya kudumu kwa matatizo ya dunia hayawezi kamwe kuachwa katika mikono ya serikali pekee, na kwamba Umoja wa Mataifa katika karne ya 21 ni lazima uangazie mitandao na ushirikiano. Bwana Ban amesema maamuzi yanayofanyika au kushindwa kufanyika katika [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola Milioni 303 kwa mwaka 2013

Kusikiliza / Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Uhamiaji IOM limetangaza mahitaji ya dola za kimarekani Milioni 303 kwa ajili ya kugharimia miradi ya misaada ya kibinadamu kwa kipindi cha mwaka huu 2013. Miradi hiyo usamaria wema iliyopangwa kutekelezwa na IOM miongoni mwake ni ile iliyoanzishwa mwaka uliopita wa 2012 na inatekelezwa katika nchi 16 ikiwemo [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utupaji chakula umekithiri: UM

Kusikiliza / utupaji chakula umekithiri

Shirika la chakula na Kilimo duniani, FAO na lile la mazingira, UNEP kwa kushirikiana na wadau wao wamezindua kampeni ya kuokoa maelfu ya Tani za chakula kinachopotea na kusababisha hasara ya dola Trilioni Moja, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutokomeza njaa duniani. Kampeni hiyo inaitwa [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za binadamu imesikitishwa na kunyongwa kwa kijana nchini Iran

Kusikiliza / humanrightsoffice

Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imesema kuwa umevunjwa moyo kutokana na ripoti za kunyongwa kwa kijana mmoja wa Ki-iran, aliyenyongwa January 16 mwaka huu baada ya kupatikana na hatia. Kijana huyo Ali Naderi alitiwa hatiana na kuamuliwa kunyongwa hadi kufa kutokana na kosa alilolitenda wakati akiwa na umri wa miaka [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila yanayowakumba wakimbizi wa Syria yaongezeka: OCHA

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Ziara ya siku nne ya ujumbe wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA huko Syria imeibua madhila zaidi yanayowakumba wakimbizi ikiwemo kukosa huduma za msingi kama vile afya, chakula na elimu kwa watoto. Msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema ujumbe huo ukimjumuisha pia Mkuu wa OCHA John Ging, uliweza kutembelea [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapitisha azimio kuimarisha ulinzi wa amani

Kusikiliza / baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio ambalo kwalo operesheni za ulinzi wa amani zitaweka msingi wa amani ya kudumu kwenye mataifa ambayo yanakumbwa na mizozo. Azimio hilo namba 2086 lilipitishwa baada ya mjadala wa siku nzima ambapo linaeleza kuwa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zinastahili kuendeshwa kwa njia ambayo [...]

22/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Mali wakumbwa na uhaba wa chakula: UNHCR

Kusikiliza / Nyakabande

Wakati mashambulizi ya angani na mapigano yanapoendelea nchini Mali, wakimbizi nao wanazidi kuvuka mipaka na kuingia nchi jirani. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa Mauritania imepokea wakimbizi 4,208 kutoka Mali tangu tarehe 11 mwezi huu ambao kwa sasa wanahamishwa kwenda kambi ya wakimbizi ya Mbera ambayo tayari inawahifadhi wakimbizi 55,221. [...]

22/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa sifa zinazotakiwa wakosesha wengi ajira: ILO

Kusikiliza / ILO_logo

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO kuhusu mwelekeo wa ajira inaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu wasio na ajira duniani mwaka jana licha ya kupungua miaka miwili iliyotangulia. Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Rider akizindua ripoti hiyo huko Geneva, Uswisi amesema mwaka jana kulikuwepo na watu wapya Milioni Nne nukta Mbili wasio na [...]

21/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Burundi na Uganda zanufaika na msaada wa dharura wa UM

Kusikiliza / Valerie Amos

Mataifa 12 duniani yakiwemo Sita kutoka Afrika yamepatiwa jumla ya dola Milioni Mia Moja kwa ajili ya misaada ya dharura, taarifa ambazo zimetangazwa leo na Mkuu wa shughuli za usaidizi wa binadamu katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos. Bi. Amos amesema fedha hizo zimetolewa kuwezesha nchi hizo zikiwemo Burundi, Eritrea, Uganda, Sudan na Liberia kutoa [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waonya kuhusu kuajiri watoto katika vita Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na vita vya silaha, Bi Leila Zerrougui, ameelezea kusikitishwa kwake na ripoti za hivi karibuni kuhusu kuajiriwa kwa watoto na makundi yenye silaha yanayojumuisha muungano wa waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Akilihutubia Kundi la kuchukua hatua la Baraza la Usalama la Umoja wa [...]

21/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaoingia Jordan yaongezeka: IOM

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM  limesema kuwa wakimbizi wanaokimbia machafuko Syria kuelekea Jordan wanaendelea kuongezeka.  Jumbe Omar Jumbe, ambae ni msemaji wa IOM, amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo.

21/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha hatua ya Myanmar ya kusitisha mapigano kwenye jimbo la Kachin

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la hivi majuzi la serikali ya Mynamar la kusitisha mapigano kwenye jimbo lililo kakazini la Kachin. Kupitia msemaji wake Ban ametoa wito kwa pande zote kufanya juhudi za kuleta utulivu kwenye jimbo la Kachin hasa kupitia mazungumzo. Ban pia ametoa wito wa kutolewa nafasi ya [...]

21/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa UM kuhusu ubaguzi wa rangi azuru Uhispania

Kusikiliza / Mutuma Ruteere

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi Mutuma Ruteere ameanza ziara ya juma moja nchini Uhispania ambapo anatarajiwa kukutana na waakilishi wa serikali , wabunge , mahakama, Ombudsman, mashirika yasiyokuwa ya serikali pamoja na makundi yanayofanya kazi kwneye nyanja za ubaguzi wa tangi. Ruteere tayari ashakutana na Waziri wa masuala ya kigeni [...]

21/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMID yasambaza misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Darfur

Kusikiliza / UNAMID yasambaza misaada Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Darfur nchini Sudan, UNAMID umesambaza misaada ya dharura kwa mamia ya raia wanaoteseka katika eneo la Kaskazini mwa Darfur na maeneo mengine ya jirani. Katika awamu yake ya kwanza, UNAMID ambayo imetumia njia ya anga na barabara, imesambaza kiasi cha kilo [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Operesheni za ulinzi wa amani kuimarishwa: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu operesheni za kulinda amani za Umoja huo kwenye maeneo mbali mbali duniani ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema watakuwa wanafanya tathmini ya operesheni hizo ili kuhakikisha zina uwezo na stadi za kuwezesha kustahimili mazingira yanayoibuka wakati wa utendaji wao. Katika hotuba [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo vya mateka Algeria yapanda hadi 57

Kusikiliza / Baraza la Usalama lajadili suala la Algeria

Idadi ya watu walio fariki dunia kufuatia tukio la siku nne la utekaji nyara katika kiwanda cha gesi cha Amenas nchini Algeria imepanda na kufika 57. Yapata watu 9 raia wa Japan wameripotiwa kuuawa, huku miili ya watu wengine 25 waliokuwa wametekwa nyara ikigunduliwa na vikosi vya Algeria. Awali mwishoni mwa wiki, Baraza la Usalama [...]

21/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Changamoto za kiafya ni nyingi, lakini zinaweza kukabiliwa: WHO

Kusikiliza / Margaret Chan

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Bi Margaret Chan, amesema kuwa nia ya kuondoa machungu kwa mwanadamu ni thabiti, lakini makali yake huathiriwa na uhaba wa rasilmali, uwezo mdogo na misaada mingi isokuwa na utaratibu mzuri. Akihutubia kikao cha 132 cha halmashauri kuu ya WHO, Bi Chan amesema shirika hilo linahudumu katika mazingira [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la nyuklia Iran, IAEA yazuiwa kuingia Parchin

Kusikiliza / nembo ya IAEA

Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA limesema mazungumzo ya siku mbili kati yake na serikali ya Iran kuhusu mpango wa nyuklia wan chi hiyo hayakuweza kumaliza tofauti kati ya pande mbili hizo. Naibu mkurugenzi Mkuu wa IAEA kuhusu mipango ya ulinzi salama Herman Nackaerts amesema mazungumzo yaliyofanyika Tehran yalikuwa ya kina [...]

21/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Sudan, waasi wa JEM waanza tena mazungumzo Doha

Kusikiliza / Aichatou Mindaoudou

Serikali ya Sudan na waasi wa kundi JEM wameanza tena mazungumzo huko Doha, Qatar ya kumaliza mzozo baina yao huku pande zote zikiahidi kuheshimu majadiliano hayo. Mazungumzo hayo yanafanyika chini ya usimamizi wa Naibu Waziri Mkuu wa Qatar Ahmed Bin Abdullah Al-Mahmoud, na Kaimu Mkuu ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaoingia Jordan yaongezeka

Kusikiliza / kambi iliyoko Jordan

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali ya wakimbizi wa Syria inazidi kuwa mbaya ambapo idadi yao wanaowasili Jordan kwa muda siku imeongezeka maradufu.   UNHCR imesema kwa sasa inapokea wakimbizi 730 kwa siku tofauti na awali ambapo ilikuwa takriban wakimbizi 500 kwa siku wanaingia Jordan.   Shirika la kimataifa [...]

21/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zerrougui asikitishwa na mauaji ya watoto yaliyofanywa na AMISOM

Kusikiliza / Kikosi cha AMISOM

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya kivita Leila Zerrougui amesema anasikitishwa sana na taarifa kuwa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM limeua watoto kadhaa wakati wa operesheni zake huko Shabelle siku ya Jumanne. Ameeleza masikitiko yake wakati huu ambapo Kaimu Mkuu wa [...]

19/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za Burundi kutokomeza umaskini zatiwa shime

Kusikiliza / wananchi wa Burundi

Umoja wa Mataifa umeitolea Burundi msaada wa milioni 600 za dola katika mpango wa nchi hiyo wa kupambana dhidi ya umasikini baada ya taifa hilo kukumbwa na vita vya zaidi ya muongo mzima. Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Mataifa ya kudumisha amani Burundi Balozi Paul SEGER amepongeza hatua iliopigwa na nchi hiyo akiwa katika [...]

19/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa waenda Mali

Kusikiliza / Joao Honwana

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unawasili Mali hii leo kusaidia serikali ya nchi hiyo kurejesha utulivu na utangamano. Msemaji wa Umoja huo Martin Nesirky amesema ujumbe huo wa awali unaongozwa na Joao Honwana kutoka Idara ya masuala ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa na jukumu lao ni kushirikiana na serikali ya Mali katika kutekeleza azimio [...]

19/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama wasilisha suala la Syria ICC: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay, Kamishna mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay kwa mara nyingine tena amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo kuwasilisha suala la Syria kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko The Hague kwa uchunguzi. Bi. Pillay amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, [...]

18/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahiga alaani mauaji ya mwandishi habari mjini Mogadishu

Kusikiliza / Abdihared

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Radio Shabelle, Abdihared Osman Adan, ambaye alipigwa risasi na kuuawa na wanamgambo wasiojulikana mapema hii leo mjini Mogadishu. Huku akisema mauaji hayo ni moja ya mfululizo wa mauaji yanayolenga waandishi wa habari, Balozi Mahiga [...]

18/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zebaki ni tishio kwa afya ya binadamu

Kusikiliza / madini ya zebaki yanavyoathiri afya ya binadamu

Madini ya zebaki yana umuhimu mkubwa kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu, lakini madini haya pia yametajwa kuwa na athari nyingi za afya ya mwanadamu kwa miaka mingi pasipo wengi kufahamu athari zake. Utafiti unaonyesha kuwa viwango vya zebaki duniani vinaendelea kuongezeka vikichochewa kila siku za shughuli za mwanadamu zikiwemo uchomaji wa makaa ya [...]

18/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa mwelekeo wa dunia kusonga katika mpito

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema dunia kwa sasa inapitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kimaendeleo na kisiasa na hivyo kuna mambo makuu matatu ya kufuatia ili kuweza kupita kipindi hicho cha mpito. Ban amesema hayo katika mhadhara alioutoa kwenye Chuo kikuu cha Stanford huko Palo Alto, California. Taarifa zaidi na George Njogopa. [...]

18/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zimbabwe yalaumiwa kwa kukandamiza haki za binadamu

Kusikiliza / wakimbizi wa Zimbabwe

Umoja wa Mataifa umelaani hatua ya serikali ya Zimbabwe ya kuyaandama mashirika yasiyo ya kiserikali na mengine ikiyafungua katika wakati taifa hilo likielekea kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu. Ofisi ya Haki za binadamu ya umoja huo imemtaka Rais Robert Mugabe na utawala wake kuondosha vitisho dhidi ya mashirika hayo ya kiraia na kumtaka kuheshimu [...]

18/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kupeleka wahudumu zaidi Mali

Kusikiliza / Mali, UNHCR

Huku operesheni za kijeshi zikiendelea kaskazini mwa Mali Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaongeza wafanyakazi wake katika eneo hilo kuwasaidia wale waliokimbia makwao. UNHCR inasema kuwa tangu Alhamisi idadi ya wale wanaohama makwao imekuwa ikiongezeka wakati raia 2,744 wakiwa wamewasili kwenye nchi jirani tangu kuanza kwa mapigano na mashambulizi ya angani [...]

18/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitendo vya ubakaji huko Mali sasa ni waziwazi: UM

Kusikiliza / hali ya kibinadamu nchini Mali

Kamishna Mkuu wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Mali sasa ni dhahiri akitaja mauaji, ubakaji na mateso. Amesema vitendo hivyo vimeelezwa kwenye ripoti ya uchunguzi itakayowasilishwa kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, kufuatia uchunguzi uliofanywa na [...]

18/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2013 ni muhimu sana kwa Cote d'Ivoire: UNOCI

Kusikiliza / Bert Koenders

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote D'Ivoire, UNOCI Bert Koenders amesema nchi hiyo inahitaji usaidizi kutoka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Akihutubia baraza hilo Bwana Koenders amesema kuwa serikali ya Cote D'Ivoire itahitaji ushirikiano wakati inapojindaa kutatua masuala yaliyopo yakiwemo umiliki wa ardhi na utambulisho. (SAUTI YA BERT KOENDERS) Mwaka [...]

18/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jitihada za Burundi kutokomeza umaskini zatiwa shime

Kusikiliza / kutokomeza umaskini nchini Burundi

Jitihada za Burundi kutokomeza umaskini zatiwa shime   Umoja wa Mataifa umeipatia Burundi dola Milioni 600 kwa ajili kusaidia mpango wa nchi hiyo kupambana na umasikini baada ya taifa hilo kukumbwa na vita vya zaidi ya muongo mzima. Fedha hizo pamoja na mambo mengine zitasaidia kuimarisha maandalizi ya uchaguzi mkuu na utawala bora nchini humo.Ramadhani [...]

18/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 30.5 zahitajika kuwatia nuru wakazi wa Kivu Kaskazini

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Umoja wa Mataifa na washirka wake wa utoaji wa misaada unaomba dola Milioni 30 na Nusu kwa ajiliya watu Elfu 59 walioathirika na mapigano ya hivi karibuni kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi (SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI) Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa [...]

18/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kazi bado kubwa kudhibiti vifo vya wajawazito

Kusikiliza / akina mama wajawazito

Mkutano wa kimataifa kuhusu afya ya wajawazito umemalizika huko Arusha Tanzania ambako imeelezwa kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kupunguza vifo vya wajawazito, bado kuna changamoto ili kuweza kufikia lengo la Milenia la kupunguza vifo hivyo kwa asilimia 75. Katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, Naibu Waziri wa afya wa Tanzania Dkt. Seif [...]

17/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Surua bado tishio baadhi ya maeneo licha ya mafanikio: WHO

Kusikiliza / Muuguzi akimpatia mtoto chanjo dhidi ya Surua

Shirika la afya duniani, WHO limesema licha ya dadi ya vifo vitokanavyo na Surua kupungua kwa asilimia 71 kati ya mwaka 2000 na 2011 duniani, ugonjwa huo bado ni tishio baadhi ya maeneo. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa Alhamisi na WHO ambapo kwa mwaka 2000 kulikuwa na vifo 542,000 ikilinganishwa na [...]

17/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Israel yajiunga na makataba wa kuzuia uchafuzi wa mazingira

Kusikiliza / unece-israel

Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi kwa bara Ulaya UNECE imekaribisha hatua ya Isreal ya kujiunga kwenye mkataba wa uchafuzi wa mazingira na habari kwa umma pamoja na kushirikishwa kwa umma katika utoaji wa maamuzi likiwa ndilo taifa nambari 32 kujiunga na mkataba huo. Mkataba huo ndio wa kwanza wa kimataifa kuhusu uchafuzi wa [...]

17/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya DRC na waasi wa M23 wakubaliana ajenda ya mazungumzo

Kusikiliza / kikundi cha waasi cha M23

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC na waasi wa kikundi cha M23 wanaokutana nchini Uganda wamekubaliana juu ya ajenda ya mazungumzo kati yao yaliyoanza tarehe 10 Desemba mwaka 2012 mjini Kampala. Ajenda ya mazungumzo ilizua vuta nikuvute baina ya pande mbili hizo na kukwamisha mazungumzo kwa siku tano. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na [...]

17/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mapigano kaskazini mwa Darfur yasababisha kuhama kwa watu wengi

Kusikiliza / watu wahama Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID umesema kuwa umejitolea kushirikiana na washikadau wote kwa minajili ya kuwahudumia maelfu ya raia waliokimbia vijiji vilivyo Kaskazini mwa jimbo la Darfur vya Saraf Omra, Kabkabya na El Sereif. Tangazo hilo linajiri baada ya tathmini ya siku mbili ya [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa Rais Rajoelina ni wa busara: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesifu uamuzi wa Rais wa mpito wa Madagascar Andry Rajoelina, wa kutogombea wadhifa huo katika kinyang'anyiro cha Urais mwezi Mei mwaka huu. Bwana Ban amekaririwa akisema kuwa kitendo cha Rais Rajoelina pamoja na ahadi ya awali ya Rais wa zamani Marc Ravalomanana, vitasaidia kuwepo kwa uchaguzi huru [...]

17/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Upanuzi wa kilimo huongeza upotevu wa bayonuai: UNEP

Kusikiliza / mavuno bora

Ripoti moja iliyoangazia ukuaji wa shughuli kilimo pamoja uhifadhi wa mazingira katika nchi za Ki-tropiki, imebainisha namna nchi zinavyopata msukumo wa kuendeleza ardhi kwa ajili ya kupata mavuno zaidi. Ripoti hiyo imesema kuwa, mataifa mengi yanajiingiza katika kile alichokiita maamuzi ya haraka ya kuendeleza ardhi kwa ajili ya kujipatia faida kwenye mazao kama mahindi na [...]

17/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baridi kali ya dhoruba yataabisha wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / baridi kali

Mabadiliko ya hali ya hewa yaliyokumba nchi za Lebanon, Jordan na  Iraq ambazo zimekubwa na mvua kubwa iliyoambatana na theluji kali, imetajwa kuvuruga ustawi wa wakimbizi wengi wa Syria. Kumekuwa na uharibifu mkubwa katika kambi ya Za'atari iliyoko kaskazini mwa Jordan ambako mahema pamoja na mifumo ya upitishaji maji imevurugwa. Mamia ya wakimbizi wengi wao [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa chakula wapungua Afrika Mashariki

Kusikiliza / mazao

Hali ya upatikanaji chakula katika eneo la Afrika Mashariki imeimarika na wasiwasi uliokuwa ulikumba eneo hilo wa umetoweka, kufuatia mavuno mazuri yaliyoanza kupatikana katika msimu wa mwezi Octoba mwaka 2012. Lakini hata hivyo mafanikio hayo hayajaondoa wasiwasi wa moja kwa moja juu ua uwekezakano wa kushudua ukosefu wa chakula katika baadhi ya maeneo. Inakadiriwa kwamba [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya ukata UNHCR yajiandaa na ongezeko la wakimbizi Mali

Kusikiliza / wakimbizi wa Mali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema licha ya ukata unaolikabili limejiandaa kuwahudumia wakimbizi ambao idadi yao inaweza kuongezeka kutokana na kuendelea kwa mapigano huko Kaskazini mwa Mali. Wakimbizi hao wanaongezeka ndani ya Mali na hata wengine wanakimbilia nchi jirani za Niger, Burkina Faso na Mauritania ambapo mwakilishi wa UNHCR nchini Niger [...]

17/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nguvu za kijeshi haziwezi kutokomeza ugaidi: UM

Kusikiliza / Balozi Masood Khan, Rais wa sasa wa Baraza la Usalama

Baada ya mjadala wa siku nzima kuhusu vita dhidi ya ugaidi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kamwe nguvu za kijeshi haziwezi kutokomeza ugaidi. Badala yale limesema mkakati wa kina na endelevu ndio njia pekee ya kukabiliana na ugaidi ambapo mkakati huo ushughulikie mazingira yanayochochea vitendo hivyo vya kihalifu. Baraza hilo limekaririwa kupitia [...]

16/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICC sasa yamulika uhalifu wa kivita Mali

Kusikiliza / Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai

Mwendesha mashtaka Mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai yanayohusika na uhalifu wa kivita, ICC, Fatou Bensouda amefungua rasmi uchunguzi dhidi ya vitendo vya  uhalifu vinavyodaiwa kufanyika Mali tangu mwezi Januari mwaka jana. Hatua hiyo inafuatia uchunguzi wa awali uliofanywa na ofisi yake kuhusu hali halisi nchini Mali ambapo sasa amesema ameridhika kuwa [...]

16/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasyria kuweni macho mgogoro unararua Taifa: Ban

Kusikiliza / Mji wa Aleppo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewataka wananchi wa Syria kutafakari upya mgogoro unaondelea nchini mwao ambao amesema unazidi kurarua taifa hilo vipande vipande. Bwana Ban amesema hayo katika taarifa iliyomnukuu kufuatia shambulio dhidi ya Chuo Kikuu Aleppo kwenye mji wa Aleppo nchini Syria ambapo watu zaidi ya 80 wameripotiwa kuuawa na wengi [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamateni wabakaji na si waandishi: Bangura

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya ukatili wa kingono katika maeneo ya migogoro, Hawa Zainab Bangura amezungumzia sakata la kushikiliwa kwa mwandishi wa habari nchini Somalia baada ya kumhoji mwanamke anayedaiwa kubakwa na askari wa jeshi la nchi hiyo ambapo ametaka serikali kumwachia mara moja mwandishi huyo. Katika taarifa yake [...]

16/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

AU yazungumzia Madagascar na Mali

Kusikiliza / mapigano nchini Mali

Umoja wa Afrika umekaribisha hatua ya rais wa Madagascar Andry Rajolina ya kutangaza kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu kukubali sharti lililkotoewa na Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika SADC, iliyotaka kuwepo kwa maelewano ya kisasa ili kuondosha hali ya uhamasama iliyoliandama taifa hilo kwa miaka kadhaa. [...]

16/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaungana na mataifa kadha kupunguza vifo vya watoto

Kusikiliza / watoto

Mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika wanakutana Addis Ababa Ethiopita kuanzia leo kwa lengo la kuweka mikakati mipya ya kudhibiti vifo vya watoto. Ripoti zinasema kuwa idadi ya watoto wanaokufa kwenye nchi za AFrika zilizo kusini mwa jangwa la sahara ilipungua kwa asilimia 39 tangu mwaka 1990. Mataifa mengi ya bara la Afrika kwa [...]

16/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viashiria vya uchumi kudorora vyatoweka: Benki ya Dunia

Kusikiliza / uchumi wa nchi zinazoendelea

Ripoti ya benki ya dunia ambayo inaangazia hali ya uchumi wa kimataifa imesema kuwa mkwamo mbaya zaidi wa kiuchumi ulioikumba dunia katika kipindi cha miaka mine iliyopita, sasa unaonekana kutoweka. Ripoti hiyo ambayo imemulika maendeleo ya uchumi wa dunia baada ya mtikisiko wa kiuchumi, imefafanua kuwa, hali iliyosababisha kuyumba kwa uchumi wa dunia haiko tena. [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watoto 1.3 nchini Yemen wameajiriwa: ILO

Kusikiliza / mtoto nchini Yemen

Zaidi ya watoto milioni 1.3 nchini Yemen wanashirikishwa kwenye ajira za watoto ambapo kati yao takribani Laki Tano wana umri wa kati ya miak a469,000 walio umri wa kati ya miaka 5-11, na hiyo ni kwa mujibu wa utafiti mpya wa Shirika la kazi duniani ILO. Hii ina maana kwamba asilimia 17 ya watoto milioni [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

G77 na ushawishi wa agenda ya UM: Ban

Kusikiliza / Mourad Benmehidi na Commodore Josaia V. Bainimarama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kundi la nchi 77 zinazoendelea, G77 pamoja na China zina ushawishi mkubwa wa kusukuma mbele agenda zinazopigamiwa na Umoja wa Mataifa katika miaka ya usoni. Amesema kuwa wakati Umoja huo wa Mataifa ukiweka vipaumbele ambavyo inakusudia kuvitilia mkazo katika miaka inayokuja ikiwemo mpango wa maendeleo endelevu, [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Mali; Umoja wa Afrika wapaza sauti

Kusikiliza / wanachi wa Mali

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Boni Yayi wa Benin ametaka Jumuiya ya kimataifa kuunga mkono jitihada za kuwafurusha vikundi vya wanamgambo vyenye silaha huko Mali, operesheni ambayo kwa sasa inaongozwa na Ufaransa. Rais Yayi amesema hayo mjini Dar Es Salaam baada ya mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete ambapo amesema kitendo cha waasi hao [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Magonjwa yaliyosahaulika kutokomezwa kabisa: WHO

Kusikiliza / who-girl

Shirika la afya duniani, WHO limejivunia maendeleo ya aina yake katika vita dhidi ya magonjwa 17 yaliyosahaulika ambayo yameendelea kuwa mzigo mkubwa kwa nchi maskini duniani. Magonjwa hayo ni kama matende, mabusha, kichocho na usubi. WHO imesema hatua hiyo imetokana na mkakati wa dunia unaotumia mbinu rahisi ya tiba na kinga na ushirika wa kimataifa [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria yaruhusu WFP kusambaza misaada

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Hatimaye serikali ya Syria imeruhusu shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo kusambaza vyakula vya misaada kwa watu Milioni Mbili na Nusu walionaswa katika shida kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo. Mkurugenzi mkuu wa WFP Ertharin Cousin ameaambia waandishi wa habari mjini Geneva leo kuwa wamepata kibali [...]

16/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugaidi ni "zimwi" lisilo na mpaka: Pakistani

Kusikiliza / Hina Rabbani Khar

Mikakati ya kimataifa ndio njia pekee ya kupambana na ugaidi, na hiyo ni kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani, Hina Rabbani Khar aliyoitoa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumane wakati wa mjadala wa wazi kuhusu vita dhidi ya ugaidi. Bi.Khar ambaye aliendesha mjadala huo kwa kuzingatia [...]

15/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauaji ya raia akiwemo mbunge huko Iraq

Kusikiliza / Martin Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler ameshutumu vikali mauaji ya mbunge Ifan Al-Issawi nchini Iraq yaliyotokana na shambulio la kigaidi wakati wa maandamano huko Fallujah ambapo pia watu kadhaa waliuawa na wengine walijeruhiwa. Kobler ambaye anaongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi nchini Iraq UNAMI amesema ni [...]

15/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

CERF yatoa fedha na kupambana na njaa nchini Malawi

Kusikiliza / Malawi

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umeidhinisha kutolewa kwa dola milioni 3.2 zitakazotumiwa kupambana na tatizo la ukosefu wa chakula nchini Malawi nchi ambayo zaidi ya nusu ya wananchi wake wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku huku asilimia 46 ya watoto walio chini ya miaka wakiwa na matatizo ya kukua. Kutokana [...]

15/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu Mali yazidi kuzorota

Kusikiliza / raia wa Mali

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inakadiriwa kuwa takribani. Laki Tatu hadi jana ambapo kabla Ufaransa haijaanza mashambulizi ya kijeshi kwa ridhaa ya serikali ya Mali idadi ya wakimbizi wa ndani ilikuwa takribani Laki Mbili. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA. (SAUTI YA JENS [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waliovuka ghuba ya Aden yavunja rekodi

Kusikiliza / wahamiaji wavuka ghuba ya Aden

Takriban wakimbizi na wahamiaji 107,500 walifanya safari zilizo hatari kutoka pembe ya Afrika kwenda nchini Yemen mwaka 2012 ikiwa ndiyo idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na wahamiji kuwahi kuandikishwa tangu mwaka 2006 wakati shirika la kuhudumia wakimbzi la Umoja wa Mataifa UNHCR lilipoanzisha ukusanyaji wa takwimu hizo. UNHCR inasema kuwa wanane kati watu kumi waliowasili [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna cha kuhalalisha ugaidi: Ban

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kamwe hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha ugaidi duniani. Hata hivyo amesema ni lazima kushungulikia mazingira yanayochochea vitendo hivyo. Bwana Ban amesema hayo leo katika hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama juu ya mikakati ya kukabiliana na ugaidi duniani. Amesema mashauriano baina ya [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mbegu mpya na uhakika wa chakula Sudan Kusini

Kusikiliza / mbegu mpya Sudan Kusini

Wakulima wa hali ya chini katika Jamhuri ya Sudan Kusini wanapatiwa mbegu bora ili waweza kuzalisha mazao muhimu ikiwa ni sehemu ya kuwainua kimaisha . Mpango huo ambao unapigwa jeki na serikali ya Ufaransa kwa kushirikiana na shirika la chakula duniani FAO na Wizara ya Kilimo nchini humo unatekelezwa katika majimbo kadhaa na kwa muhula [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wanaorejea Niger wapatiwa stadi

Kusikiliza / wahamiaji

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua mpango wa kuwasaidia wahamiaji raia wa Niger wanaorejea nyumbani kutoka Libya pamoja na familia zinazowahifadhi. Mradi huo ambao tayari umepokea Euro milioni 2.8 kutoka kwa jumuiya ya Ulaya utasaidia kubuni miradi itakayochangia mapato kwa watu 3,125 moja kwa moja kutoka sehemu za Tahoua, Tillabery, Zinder na mji mkuu [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yasababisha watu zaidi kukimbia Mali

Kusikiliza / wananchi wa Mali

Makabiliano kati ya jeshi la Mali linaloungwa mkono na ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Al-Qaida kwenye maeneo ya Konna, Lere na Gao kaskazini mwa Mali yamesabisha kuhama kwa watu ndani na kwenda nchi majirani zake. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa zaidi ya watu 648 kwa sasa ni wakimbizi wa [...]

15/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yaanza kurejea Somalia

Kusikiliza / Askari polisi wa Somalia akiwa kwenye doria

Nchini Somalia hususan mji mkuu Mogadishu ambapo awali vikundi vya kigaidi vilitamba, hali ya amani imeanza kutengamaa. Wananchi nyakati za usiku wanafanya shughuli zao hata kucheza mpira wa miguu ambao awali ulipigwa marufuku na Al Shabaab. Je nini imesababisha hali hii? Jiunge na Assumpta Massoi kwa ripoti maalum… Mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu, giza limeingia…..kwa [...]

15/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Jeshi la Afrika kwenda Mali punde

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Baraza la usalama hii leo lilikuwa na kikao  kuhusu hali ilivyo huko Mali ambapo Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud amesema wajumbe wote wa baraza wameunga mkono hatua za kijeshi za Ufaransa kwa ridhaa ya Mali. Bwana Araud amewaambia waandishi wa habari kuwa tayari nchi zingine ikiwemo Marekani, Canada na [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kitabu cha Annan chamulika changamoto na mafanikio

Kusikiliza / Kitabu cha Kofi Annan

Masuala ya amani, ulinzi, usalama, uongozi bora na misaada na maendeleo ni miongoni mwa mambo yaliyochukua nafasi katika kitabu kilichoandikwa na Katibu Mkuu  mstaafu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, A Life in War and Peace. Akizungumza katika hafla ya kuzindua kitabu hicho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani hii [...]

14/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Nafuatilia kwa karibu hali ya Mali: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati  hali ya usalama ikiripotiwa kuendelea kuzorota huko Mali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anafuatilia kwa karibu hali hiyo ambapo tayari amezungumza na Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Rais Alassane Ouattara wa Côte d’Ivoire . Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza kujulishwa [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kurejea kwa Dkt. Mukwege ni ujasiri: Meece

Kusikiliza / Dkt. Denis Mukwege

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC, Roger Meece ameunga mkono kurejea huko Bukavu, Kivu Kusini kwa Dkt. Denis Mukwege, Mganga Mkuu wa hospitali ya Panzi ambaye mchango wake kwa tiba kwa wanawake waliokumbwa na ukatili wa kingono ikiwemo kubakwa unatambulika duniani kote. Bwana Meece ambaye [...]

14/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maelfu wapoteza makazi kufuatia mzozo Mali

Kusikiliza / Wakimbizi Mali

  Takribani watu Elfu Thelathini wanahofiwa kuwa wamepoteza makazi yao kutokana na mapigano huko maeneo ya Kati na kaskazini mwa Mali na inahofiwa kuwa idadi yao inaweza kuwa kubwa kwa kuwa vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kiislamu vinazuia watu kukimbilia maeneo ya Kusini. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo del Buey [...]

14/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa UM kuhusu haki ya kukusanyika kwa amani aitembelea uingereza

Maina Kiai

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki kukusanyika kwa amani na kushauriana Maina Kiai ataitembelea uingereza kuanzia tarehe 14 hadi 23 ziara ambayo itakuwa ndiyo ya kwanza ya ukusanyaji wa habari kufanywa na mtaalamu kama huyo aliyetumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza haki ya kukusanyika kwa amani na [...]

14/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Haki ya kibinadamu Yemeni bado tete

Kusikiliza / ramani ya Yemen

Kusainiwa kwa mpango wa amani uliokaribisha kipindi cha mpito nchini Yemen kumefungua njia ya kukaribisha huduma za utoaji wa misaada ya kibinadamu ambayo hapo kwanzo ilizorota kutokana na hali mbaya ya kisiasa. Jarida la masuala ya kibinadamu la Umoja wa Matalifa linasema kuwa mapema mwaka uliopita kulisainiwa makubaliano ya kuwepo kwa kipindi cha mpito kuelekea [...]

14/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jeshi la kimataifa kuungana na MONUSCO: Gaye

Kusikiliza / Babacar Gaye

Mshauri wa masuala ya kijeshi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jenerali Babacar Gaye, amesema kuunganishwa kwa jeshi la kimataifa linalokwenda mpakani wa Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRCna kikosi cha MONUSCO kutasaidia kupunguza gharama za fedha. Jenerali Gaye amesema hayo alipozungumza na Radio Okapi baada ya kurejea kutoka Addis Ababa, Ethiopia [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uingereza yaipiga 'jeki' Haiti

Kusikiliza / mabaki ya tetemeko, Haiti

Wito kwa nchi kusaidia Haiti kujijenga baada ya tetemeko kubwa miaka mitatu iliyopita umepata jibu baada ya Uingereza kutangaza mkopo nafuu wa dola Milioni 16 ili iweze kujikwamua haraka na madhila ya sasa. Taarifa iliyotolewa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP imesema fedha hizo pamoja na mambo mengine zitajenga uwezo [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazoibuka kiuchumi zapongezwa kwa kumulikia afya

Kusikiliza / Michel Sidibe

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na HIV na Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé amepongeza hatua za nchi zinazoibukia kiuchumi duniani ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, BRICS ya kuazimia kushirikiana kuboresha sekta ya afya duniani. Mathalani amegusia dhima ya kipekee ya nchi hizo kutumia uzoefu wao wa kupambana na [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tusipuuze ukiukwaji haki za binadamu Korea Kaskazini: Pillay

Kusikiliza / malnutri-dprk

Kamishna mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua kutatua suala la haki za binadamu nchini Korea Kaskazini akisema kuwa wakati umewadia wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu uhalifu ambao umekuwa ukiendelea nchini humo kwa miaka mingi. Pillay amesema kuwa kulikuwa na matumani ya mabadiliko [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunisia iangalie upya usawa wa jinsia: Wataalamu UM

Kusikiliza / Kamala Chandrakirana

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa wanawake kwa misingi ya sheria na vitendo limetaka serikali ya Tunisia kuridhia vipengele vya msingi vya katiba juu ya usawa wa jinsia na kutekeleza hatua maalum za muda zitakazoharakisha ushiriki wa wanawake katika Nyanja zote za maisha. Akizungumza mwishoni mwa ziara ya wataalam hao [...]

14/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chuki za kidini hazina nafasi karne ya 21: Ban

Kusikiliza / Utengamano

Chuki inayojengwa kwa misingi ya imani ya dini haina nafasi karne hii ya 21 ambayo tunaendelea kuijenga. Na hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyoitoa leo mjini New York, Marekani wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya wayahudi yaliyotekelezwa na serikali ya Adolf Hitler. Bwana Ban amesema wakati [...]

12/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado Haiti inahitaji msaada: Ban

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za UM Hervé Ladsous katika kumbukumbu ya waliokufa kwenye tetemeko huko Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameomba jumuiya ya kimataifa kuendelea na moyo wa kusaidia Haiti katika ujenzi wa nchi yao baada ya tetemeko kubwa la ardhi miaka mitatu iliyopita lililosababisha vifo vya zaidi ya watu Laki Mbili. Ban amesema hayo katika ujumbe uliosomwa kwa niaba yake na Mku uwa operesheni za ulinzi [...]

12/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumbukumbu za tetemeko la Haiti bado dhahiri

Kusikiliza / Jean-Philippe-Bernardini

Leo ni miaka mitatu tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti lililosababisha vifo vya watu zaidi ya Laki Tatu na Mamilioni kupoteza makazi ambapo Umoja wa Mataifa umesema kazi ya ujenzi inaendelea vizuri na asilimia 80 ya taka zitokanazo na tetemeko hilo zimeshaondolewa. Miongoni mwa walionusurika katika tetemeko hilo ni Jean BERNARDINI, ambaye [...]

12/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo CAR, Baraza la usalama lasifu makubaliano ya Libreville

Kusikiliza / Baraza la usalama likipatiwa ripoti kutoka kwa Margaret Vogt kwa njia ya video

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesifu mashauriano yaliyofanyika huko Libreville Gabon, na kuwezesha kutiwa saini kwa makubaliano ya kimsingi ya kusitisha mapigano na kupatia suluhu la kisiasa mzozo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa ya  Baraza hilo iliyotolewa mwishoni mwa kikao maalum kuhusu hali ya usalama nchini humo imesema wajumbe wanataka kuharakishwa [...]

11/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Biashara haramu ya tumbaku yaanza kubanwa

Kusikiliza / Wanawake wakifungasha sigara

Hatimaye itifaki ya kutokomeza biashara haramu ya bidhaa za Tumbaku imeanza kutiwa saini na hivyo kuonyesha utashi wa kisiasa wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku. Hafla hiyo ilifanyika mjini Geneva Uswisi kwa mataifa 12 wanachama wa mkataba huo kutia saini na baadaye shughuli hiyo itahamishiwa New York, Marekani makao [...]

11/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Lahitajika jeshi thabiti CAR: Vogt

Kusikiliza / Margaret Vogt

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limeelezwa jinsi hali  ya usalama ilivyo tete huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako jeshi linashindwa kudhibiti waasi wanaoendelea kushikilia miji kadhaa nchini humo. Taarifa hizo zimetolewa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa nchini humo Margaret Voght wakati akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu [...]

11/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP kutoa msaaada kwa karibu watu 1.6 nchini Zimbabwe

Kusikiliza / Hali ya chakula Zimbabwe

Karibu watu milioni 1.6 nchini Zimabbwe wengi wanaoishi sehemu za vijijini kwa sasa wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula kutokana na sababu ya ukosefu wa mvua na kupungua kwa mazao ya kilimo. Kulingana na msemaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kanda ya mashariki na kusini mwa Afrika Davi Orr ni kuwa WFP [...]

11/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya wakimbizi CAR inatutia wasiwasi: UNHCR

Kusikiliza / Watu wakihama makwao huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linataka kuwafikia wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati bila masharti yoyote kwa kuwa lina wasiwasi kuwa hali zao zitakuwa ni mbaya. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwrds akizungumza mjini Geneva leo amesema maelfu ya watu wamekimbia makazi  yao kutokana na mapigano kaskazini na mashariki mwa nchi [...]

11/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wazungumzia ghasia zinazoshuhudiwa nchini Kenya

Kusikiliza / tana river

Umoja wa Mataifa umetuma rambi rambi zake kwa serikali ya Kenya pamoja na kwa familia za watu waliothiriwa na ghasia zinazoshuhudiwa kwenye eneo la Mto Tana na sehemu zeningine za nchi. Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya masuala ya kibinadamu nchini Kenya, Umoja wa Mataifa umelaani kile unachokitaja kuwa vitendo viofu ambavyo tangu mwanzo wa [...]

11/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya Geneva bado msingi wa amani Syria: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi, Mjumbe maalum wa pamoja wa UM na nchi za kiarabu kwenye mgogoro wa Syria

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi ametoa muhtasari wa mazungumzo yake na naibu mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani  William Burns na yule wa Urusi Mikhail Bogdanov yaliyofanyika huko Geneva, Uswisi ambapo amesema kwa pamoja wametambua madhila wanayopata wananchi wa Syria na [...]

11/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kunyongwa kwa mfanyakazi wa nyumbani Saudi Arabia kunasikitisha: Pillay

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya UM, Navi Pillay

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kufuatia kitendo cha kunyongwa hadi kufa kwa mfanyakazi wa nyumbani Rizana Nafeek huko Saudi Arabia kwa kosa la kumuua mtoto wa mwajiri wake. Msemaji wa Ofisi hiyo Rupert Colville amemkariri Pillay akisema kuwa adhabu hiyo ni kinyume na haki [...]

11/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNAMID yataka kusitishwa mapigano ya kikabila kwenye eneo la Jebel Amer

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

  Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID unasema kuwa umetiwa wasi wasi na mapigano kati ya kabila za Hussein na Abbala katika eneo la Jebel Amer karibu na Kabkabiya Darfur kaskazini. Mapigano hayo yanayoripotiwa kuanza tarehe tano mwezi Januari mwaka huu yamesabisha mauaji [...]

11/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Burundi waanza maisha mapya

Kusikiliza / wakimbizi wa Burundi warejea nyumbani

Kambi ya Mutabila iliyokuwa imewapokea wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania imefungwa rasmi tarehe 31 Mwezi Desemba mwaka jana na kuwa kambi ya mwisho kabisa kufungwa. Kambi iliyoko magharibi mwa Tanzania ilikuwa imewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 36 Elfu wa Burundi ambao tayari wamerejea nchini mwao Burundi katika shughuli iliyosimamiwa na Shirika la kimataifa la kuwahudumia [...]

11/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya Mali yatishia usalama wa kikanda na dunia: UM

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Wajumbe wa Baraza la usalama waliokutana katika kikao cha dharura jioni ya leo kuhusu Mali wameeleza kusikitishwa kwao na ripoti ya kwamba vikundi vya kigaidi na vyenye msimamo mkali kaskazini mwa nchi hiyo vinaendelea na mashambulizi, wakigusia zaidi taarifa za kutekwa kwa mji wa Konna. Rais wa Baraza hilo Balozi Masood Khan amewaambia waandishi wa [...]

10/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya Pakistani yanitia wasiwasi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kusikitishwa kwake na mwendelezo wa mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistani akigusia shambulio la jana na la leo. Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban ameshutumu mashambulio hayo katika eneo la Quetta na Swat ambayo yamesababisha vifo vya watu wapatao 100 [...]

10/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ladsous aanza ziara Haiti

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous  na Rais Michel Martelly wa Haiti.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Hervé Ladsous, amesema kazi iliyopo hivi sasa nchini Haiti, miaka mitatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi ni kujikita zaidi katika kujenga jeshi la polisi la kitaifa na kuimarisha wa utawala wa kisheria. Bwana Ladsous amesema hayo alipozungumza na waandishi wa [...]

10/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Upanzi wa miti waokoa wakulima Kenya: UNEP

Kusikiliza / maji nchini Kenya

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa upanzi wa miti kwenye miteremko ya Mlima Kenya umekuwa wa manufaa kwa wakulima waliokuwa wanategemea msimu wa mvua kwenye shughuli zao za kilimo huku pia ukichaangia katika kupunguza umaskini. Kupitia mradi huo unaohusu upanzi wa miche kwenye sehemu za vyanzo vya maji umewanufaisha wakulima hasa sehemu na mashariki mwa [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova alaani mauaji ya waandishi wa habari nchini Syria

Kusikiliza / Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, Irina Bokova ameelezea wasi wasi wake kufuatia kuendelea kuuawa kwa waandishi wa habari nchini Syria , baada ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha runinga Suhail Mahmoud Al-Ali Ijumaa iliyopita. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (SAUTI YA JASON [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zebaki tishio la afya na mazingira: UNEP

Kusikiliza / zebaki

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP limesema kadri siku zinavyosonga, zebaki inazidi kutishia afya ya binadamu na mazingira katika nchi zinazoendelea kutokana na ongezeko la uchafuzi wa mazingira utokanao na madini hayo. UNEP imesema metali hiyo yenye sumu hutumiwa na wachimbaji wadogo katika shughuli zao na pia katika uchomaji wa makaa ya mawe [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malawi isimamie marekebisho ya kiuchumi: IMF

Kusikiliza / Christine Lagarde

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la fedha ulimwenguni IMF, Christine Lagarde amewataka wananchi wa Malawi kuendelea kutekelezwa mageuzi magumu ya kiuchumi yaliyopendekezwa na shirika hilo ambayo yanapigwa na idadi kubwa ya wananchi. Lagarde ametoa wito huo wakati akikamilisha ziara yake ya siku tatu. Taarifa zaidi na George Njogopa: (SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula zaendelea kushuka: FAO

Kusikiliza / vyakula

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema wastani wa bei ya chakula ulishuka kwa asilimia Saba mwezi Disemba mwaka jana na hivyo kufanya bei za vyakula kupungua kwa miezi mitatu mfululizo. Ripoti ya FAO kuhusu bei ya za chakula inaonyesha bei ya kapu la chakula ilishuka kwa pointi Moja nukta Moja [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara haramu ya tumbaku sasa mtegoni: WHO

Kusikiliza / Wajumbe katika hafla ya kutia saini itifaki ya kuzuia biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na tumbaku

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO, Dkt. Margaret Chan amesema itifaki mpya ya kutokomeza biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na tumbaku inaipatia dunia fursa ya kipekee ya kudhibiti njia za kisasa za kitendo hicho cha kihalifu chenye gharama kubwa hususan kwa afya za binadamu. Dkt.Chan amesma hayo leo mjini Geneva, Uswisi wakati wa [...]

10/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baada ya tetemeko, Haiti inajikwamua:UM

Kusikiliza / Wananchi wa Haiti wakishiriki ujenzi wa nchi yao.

Miaka mitatu tangu tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti, Umoja wa Mataifa umesema jitihada za kusadia nchi hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida zimetia matumaini ikiwemo ujenzi wa shule, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Hiyo ni kauli ya Afisa Mtendaji Mkuu wa wakfu ya Umoja wa Mataifa Kaithy Calvin aliyoitoa alipozungumza na [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria zitungwe kulinda wafanyakazi wa majumbani: ILO

Kusikiliza / wafanyakazi majumbani

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO imeweka bayana kuwa bado kazi za majumbani zinadharauliwa licha ya mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii. ILO inasema ajira hiyo ni ya manyanyaso, kuanzia muda wa kazi hadi maslahi. Ripoti inaonyesha kuwa kiidadi, wafanyakazi hao wanaongezeka lakini maslahi yao yanazidi kuwa duni hasa katika nchi zinazoendelea. [...]

09/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aunga mkono azma ya Abe ya kuinua uchumi wa Japan

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu mpya wa Japan Shinzo Abe ambapo pamoja na kumpongeza kwa wadhifa huo mpya, amesema anaunga mkono azma ya Abe ya kujenga upya uchumi wa Japan baada ya tetemeko kubwa la ardhi la mwaka 2011 pamoja na Tsunami. [...]

09/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana wakutana Seoul kujadili matatizo yanayokumba eneo la Asia

Kusikiliza / vijana

Nafasi za ajira, kutokuwepo kwa usawa, mazingira, usawa wa kijinsia, amani na usalama huko Kaskazini-mashariki mwa Asia ni miongoni mwa masuala kuu ambayo vijana wa eneo hilo wanataka yazingatiwe katika ajenda ya baadaye ya maendeleo. Washirikishi vijana kutoka nchi kama vile China, Japan na Mongolia wameafikia makubaliano kuhusu maendeleo ya dunia yenye kauli mbiu "Ulimwengu [...]

09/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mapigano Darfur ya kati yanaathiri raia: UNAMID

Kusikiliza / Aichatou Mindaoudou

Kaimu mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID Aichatou Mindaoudou ametembelea mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kati, Zalingei ambapo ameelezea wasiwasi wake juu ya mapigano yanayoendelea kwenye mji wa magharibi wa Jebel Marra. Ameelezea wasiwasi wake huo baada ya mazungumzo na gavana wa jimbo hilo [...]

09/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Canada kufanya mazungumzo ya viongozi wa kitamaduni

Kusikiliza / James Anaya

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya jamii za kiasili James Anaya ametoa wito kwa serikali ya Canada kufanya mazungumzo na viongozi wa kitamaduni nchini humo kufuatia kushuhudiwa kwa maandamano hivi majuzi. Mjumbe huyo amesema amefurahishwa na ripoti kwamba waziri mkuu wa Canada Steven Harper amekubali kukutana na viongozi hao kuzungumzia masuala yakiwemo [...]

09/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yapongeza ripoti mpya ya “Save the Children”

Kusikiliza / save the children

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limepongeza ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali la Uingereza, Save the Children inayomulika mikakati ya kutokomeza umaskini na dira ya watoto baada ya mwaka 2015. UNICEF imesema ripoti hiyo inatoa mwelekeo wa kusimamia haki za msingi za mtoto ikiwemo ile ya kuishi, kulindwa na kuendelezwa [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nitaimarisha mtandao wa posta duniani: Hussein

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa UPU Bishar Hussein

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Umoja wa mashirika ya posta duniani, UPU, Bishar Hussein kutoka Kenya amesema azma yake kubwa ni kuimarisha mtandao wa mashirika ya posta duniani. Akizungumza mjini Berne, Usiwsi leo wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi, ili kuchukua wadhifa huo kwa kipindi cha miaka minne, Bwana Hussein amesema atahakikisha nchi zote kuanzia zilizoendelea, [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani yazidi kusakwa Syria, IOM yaomba msaada zaidi

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakdhar Brahimi, Ijumaa atakuwa na mazungumzo na viongozi wa Urusi na Marekani kwa lengo la kupatia suluhu la kisiasa mzozo unaoendelea nchini Syria. Habari zinasema kuwa mazungumzo hayo baina ya Brahimi na Naibu Waziri wa mambo ya Nje [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa majumbani Tanzania hawajitambui: ILO

Kusikiliza / wafanyakazi wa nyumbani

Ofisi ya ILO nchini Tanzania imesema bado kuna changamoto kubwa ya kuweza kuwakomboa wafanyakazi wa majumbani dhidi ya matatizo yanayowakabili licha ya kwamba sheria za kazi zinawatambua. Mratibu wa mpango wa misaada ya maendeleo katika ofisi ya ILO nchini Tanzania, Anne-Marie Kiaga ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa changamoto hizo ni za pande tatu [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa majumbani waendelea kunyanyasika: ILO

Kusikiliza / mfanyakazi wa nyumbani

Ripoti mpya ya shirika la Kazi duniani, ILO kuhusu hali ya wafanyakazi wa majumbani imeonyesha kupanuka kwa sekta hiyo huku mazingira ya kazi yakiendelea kuwa duni hususan katika nchi zinazoendelea. Mathalani ripoti hiyo imesema kuwa wafanyakazi hao wanaendelea kunyanyaswa ikiwemo kufanya kazi saa nyingi kupindukia kwa ujira mdogo, kufanya kazi kwa saa nyingi ikitolea mfano [...]

09/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali za wakimbizi huko Sudan ni mbaya: Ging

Kusikiliza / Blue-Nile-State-27Sept-UNHCR

Mamia ya maelfu ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali na vikundi vya waasi wenye silaha kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha. Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa OPeresheni wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya [...]

08/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bangura aunga mkono vikwazo dhidi ya waasi DRC

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ukatili wa ngono kwenye maeneo ya migogo Zainab Hawa Bangura amesema anaunga mkono vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama dhidi ya vikundi vya waasi vya FDLR na M23 huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (SAUTI ASSUMPTA) Taarifa [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova asikitishwa na kifo cha Singh

Kusikiliza / Madanjeet Singh

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, ameelezea kusitikitishwa kwake kutokana na kifo cha Balozi mwema wa UNESCO Madanjeet Singh kilichotekea tarehe sita Januari. Amesema marehemu Singh alikuwa na juhudi na alijitolea katika kazi ya kuendeleza maelewano na amani na ni mfano wa kuigwa kwa watu kutoka mataifa, tamaduni na dini mbalimbali. Ameongeza kuwa UNESCO imepoteza [...]

08/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahitaji yazidi kuongezeka Syria

Kusikiliza / watoto nchini Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema mahitaji ya kibinadamu nchini Syria yanaongezeka, likitaja zaidi vyakula ambapo mikate na mafuta vimeadimika zaidi nchini humo. Shirika hilo linasema kuwa kwa sasa linahudumia watu Milioni Moja na Nusu kila mwezi wakati linakadiria kuwa watu Milioni Mbili na Nusu ndio wanaohitaji msaada. WFP imesema inashindwa kutoa msaada [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahrain iwaachie mara moja watetezi wa haki za binadamu: UM

Kusikiliza / maandamano, Bahrain

Ofisi ya Kamishna wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, imetaka kuachiwa mara moja kwa raia 13 wa nchi hiyo waliohukumiwa kifungo jela kwa kufanya maandamano dhidi ya serikali ya nchi hiyo. Ofisi hiyo imeeleza kusikitishwa na kifungo cha wanaharakati hao baada ya miaka miwili ya kesi licha ya matokeo ya tume huru ya [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baadhi ya sheria zinasababisha maambukizi mapya ya HIV: Rao

Kusikiliza / Prasad Rao

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Ukimwi kwa nchi za Asia na Pasifiki, Prasad Rao amesema baadhi ya sheria zinazofuatwa nchini humo zimesababisha kuwepo kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi licha ya mafanikio ya kudhibiti ugonjwa huo. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uswisi yatunisha mfuko wa IOM

Kusikiliza / wahamiaji wa Chad

Shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM pamoja la lile la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) yametia sahihi makubaliano ya mradi utakaowasaidia raia wa Chad waliorejea nyumbani kutoka Libya ambao kwa sasa wanaishi kwenye mikoa mitatu ya kaskazini iliyo jirani na mpaka wa Libya, Niger na Sudan. Msaada huo wa dola Milioni 2.9 kutoka Uswisi [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uvutaji sigara waongezeka nchi maskini: WHO

Kusikiliza / framework

Wakati shirika la afya duniani, WHO likiwa katika maandalizi ya mwisho ya shughuli ya kuanza kutia saini mkataba wa kimataifa wa kutokomeza biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na tumbaku siku ya Alhamisi, shirika hilo limesema kwa sasa kuna taswira tofauti ya kiwango cha uvutaji sigara duniani. Mkuu wa sekretarieti ya mkataba huo Dokta Dr. Haik [...]

08/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hotuba ya Assad inabomoa wala haijengi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kusikitishwa kwake na hotuba ya jana ya Rais wa Syria Bashar Al Assad kwa wananchi wake ambayo amesema haichangii katika kumaliza machungu yanayokabili raia wa Syria bali inachochea ghasia zaidi. Bwana Ban amekaririwa na Msemaji wake akieleza kuwa hotuba hiyo inakataa kwa kiasi kikubwa vipengele vya [...]

07/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wapatiwa misaada huko Kivu Kaskazini

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Baada ya ghasia kushamiri huko jimbo la Kivu Kaskazini na kusababisah watu kukimbia makwao na hata mashirika ya misaada kushindwa kusambaza huduma za dharura kwa wananchi, hatimaye kazi ya usambazaji imeanza baada ya kuwepo kwa utulivu siku za karibuni. Misaada inayotolewa ni ya kibinadamu. Assumpta Massoi ameandaa ripoti kamili. (SAUTI YA ASSUMPTA) Msururu mrefu wa [...]

07/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kurejea kwa wakimbizi wa Somalia ni vema lakini kuna changamoto

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwezi huu wa januari kumeshuhudiwa kuanza kurejea kwa wakimbizi wa Somalia nchini mwao. Tafsiri mbalimbali zimetolewa juu ya kitendo hicho lakini kubwa zaidi likielezwa kuwa ni kurejea kwa amani nchini Somalia baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo ili kufahamu zaidi Monica Morara wa radio ya Umoja wa Mataifa amefanya [...]

07/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Bachelet kutembelea nchi tatu za Afrika Magharibi

Kusikiliza / Michelle Bachelet

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN Michelle Bachelet, atasisitiza umuhimu wa kuongeza ushiriki wa wanawake kama msingi wa kujenga taifa na maendeleo ya kiuchumi, wakati wa ziara yake Afrika Magharibiki. Wakati wa ziara hiyo inayoanza leo hadi tarehe 11 mwezi huu, Bi Bachelet atatembelea sehemu zilio na miradi [...]

07/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sayansi na Teknolojia yabakia ndoto kwa wanawake: ILO

Kusikiliza / wanawake na teknolojia

Shirika la kazi duniani ILO linasema kuwa hatua zinastahili kuchukuliwa katika kutatua mwanya uliopo kweye uwakilishi wa wanawake kwenye nyanja za sayansi na teknolojia. Claude Akpokavie afisa wa idara ya wafanyikazi ya ILO ACTRAV anasema kuwa hata kama maendeleo ya sayansi na teknolojia ni ya kasi, wanawake bado wanakabiliwa na hatari ya kuachwa nyuma. Akpokavie [...]

07/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kurejea wakimbizi ni dalili nzuri: Balozi Mahiga

Kusikiliza / wakimbizi wa Somalia wanaorudi nyumbani

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga ametolea ufafanuzi kitendo cha kurejea kwa wakimbizi wa Somalia nchini mwao ambapo amesema wakimbizi hao wanarejea kwa hiari yao wenyewe kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama nchini mwao. Balozi Mahiga amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa [...]

07/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya misaada yajipanga kutathmini hali halisi CAR

Kusikiliza / raia wa CAR

Wakati ripoti zikieleza kuwepo kwa mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na waasi, mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini humo Dkt. Zakaria Maiga amesema wanajiandaa kupeleka jopo la kutathmini hali ya mahitaji kwenye maeneo yaliyokumbwa na mzozo nchini humo.Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. Afisa huyo ametoa kauli hiyo wakati huu [...]

07/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada yasambazwa kwa wakimbizi DRC: UNICEF

Kusikiliza / msaada kutoka UNICEF kwa wakimbizi wa DRC

Utulivu siku za hivi karibuni umechangia kuwepo usambazaji wa misaada ni bidhaa zingine muhimu zikiwemo blanketi na nguo kwenye meeneo waliko wakimbizi wa ndani kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC. Hii ndiyo oparesheni kubwa zaidi ya ugavi wa bidhaa za nyumbani kufanyika siku za hivi karibuni mkoani Kivu Kaskazini. [...]

07/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Niko tayari kwenda Guinea-Bissau: Ramos-Horta

Kusikiliza / Mwakilisha maalum wa Katibu Mkuu wa UM Guinea-Bissau Jose Ramos-Horta

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Guinea-Bissau Jose Ramos Horta amesema yuko tayari kwenda nchini humo kutekeleza majukumu ya kuwezesha kurejea kwa amani na utulivu. Akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Ramos- Horta amesema anafahamu fika hali halisi ya Guinea-Bisssau kwa kuwa alishakwenda nchini humo, mara ya kwanza akiwa [...]

04/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ILO kuzindua ripoti kuhusu wafanyakazi wa majumbani

Kusikiliza / Tukio la kuunga mkono wafanyakazi wa majumbani nchini India

Shirika la kazi duniani, ILO wiki ijayo itazindua ripoti mpya kuhusu hali za wafanyakazi wa majumbani duniani kote. Ripoti hiyo mpya inajaribu kugusia ukubwa wa sekta hiyo, mazingira ya kazi na mawanda ya ulinzi wa kisheria kwa wafanyakazi hao wa majumbani. Mathalani inajumuisha takwimu za dunia na za kikanda na inalenga kusaidia jitihada za serikali, [...]

04/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IFAD yakomboa wanawake Gambia

Kusikiliza / wanawake nchini Gambia

Kilimo bora kinahitaji pia uwepo wa ardhi yenye rutuba. Nchi Gambia kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika tunaelezwa kuwa ardhi yenye rutuba hutumiwa zaidi na wanaume na wanawake hubakia pembezoni kwenye ardhi iliyochoka na hivyo hata kwa jitihada gani matunda ya kazi ni nadra kuonekana. Lakini kwa sasa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya [...]

04/01/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uchoraji unavyopanua uelewa wa watoto

Kusikiliza / uchoraji wa watoto

Nchi nyingi barani afrika zinalalamikiwa kutokana na kutoweka mazingira mazuri ya kuendelea vipaji vinavyochomoza kwa watoto. Hali hiyo imefanya ndoto za vijana wengi kuishia hewani kutokana na kukosa daraja la kuwaendeleza. Lakini nchini Tanzania nuru imeanza kuchomoza kidogo baada ya kueanzishwa darasa maalumu kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kisanaa. Sanaa hii inaelezwa kuwa kichocheo kikubwa [...]

04/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yatoa ripoti kuhusu usafirishaji binadamu

Kusikiliza / usafirishaji haramu wa watu

Shirika la Wahamiaji Duniani IOM leo limetoa ripoti yake ya kwanza juu ya mwelekeo wa usafirishaji wa binadamu ambapo inaonyesha kuwa nusu ya visa vilivyoletwa mbele ya shirika hilo kwa ajili ya kupata msaada katika mwaka wa 2011 ni kuhusu dhuluma ya kulazimishwa kufanya kazi. Kabla ya hapo biashara ya kusafirisha binadamu iligusa zaidi usafirishaji [...]

04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tisa wawania wadhifa mkuu WTO

Kusikiliza / nembo ya WTO

Jumla ya watu Tisa waliwasilisha majina yao kuwania nafasi ya Ukurenzi Mkuu wa Shirika la biashara duniani, WTO ambapo mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy kipindi chake kinakoma tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu. Taarifa ya WTO inataja nchi wanazotoka watu hao kuwa ni Brazili, Jamhuri ya Korea, Mexico, Jordan, Costa Rica, New Zeland, Ghana, [...]

04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wachezaji wa NBA watoa chanjo za Polio Kenya

Kusikiliza / wachezaji wa NBA nchini Kenya

Kundi la wachezaji mashuhuri wa ligi ya mpira wa kikapu NBA kutoka Marekani wameitembelea Kenya katika shughuli ya kupambana na ugonjwa wa kupooza. Wakiwa kwenye wilaya ya Turkana wachezaji hao wakiwemo Luc Mbah a Moute, Nick Collison and Dikembe Mutombo waliungana na kampeni ya kutoa chanjo ya nyumba hadi nyumba ya kuwachanja watoto wa eneo [...]

04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahitimisha urejeshaji wakimbizi wa Liberia

Kusikiliza / wakimbizi wa liberia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekamilisha mpango wake wa kurejesha nyumbani kwa hiari wakimbizi 155,000 wa Liberia waliokuwa wanaishi uhamishoni kwa miaka 23 baada ya kuanza kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao. Kundi la mwisho la wakimbizi 724 waliondoka kutoka Guinea na hivyo kukamilisha mpango huo ulioanza mwaka 2004, [...]

04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo CAR, watoto watumikishwa jeshini: UNICEF

Kusikiliza / watoto walio jeshini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaka kusitishwa mara moja kwa vitendo vinavyofanywa na vikundi vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR vya kuandikisha watoto kwenye majeshi. UNICEF imetaka pande zote katika mzozo unaoendelea nchini humo kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote hatari ikiwemo kuhusishwa na mgogoro huo. Tamko la [...]

04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya kibinadamu yashamiri Masisi: MONUSCO

Kusikiliza / MONUSCO, masisi

Ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MONUSCO umesema kumekuwa na ongezeko kubwa la ghasia za kikabila katika eneo la Masisi lililoko jimbo la Kivu Kaskazini Taarifa ya kuwepo kwa matukio korofi inakuja baada ya MONUSCO kutuma maafisa wake waliokwenda kutathimini hali jumla ya mambo ikiwemo kuangazia hali ya usalama [...]

04/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza mpango wa mkutano wa Bashir na Kiir

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon

Marais Omar Al Bashir wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan Kusini Ijumaa watakuwa an mazungumzo yanayoratibiwa na Umoja wa Afrika kupitia Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki. Mazungumzo hayo yatafanyika nchini Ethiopia chini ya wenyeji wa Waziri Mkuu uwa nchi hiyo Hailemariam Desalegn ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon [...]

03/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Masuala ya Afrika kuendelea kumulikwa Baraza la Usalama

Kusikiliza / Masood Khan

Harakati za kupatia suluhu migogoro mbali mbali inayoendelea barani Afrika zitaendelea katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Januari, na hiyo ni kwa mujibu wa Rais wa  kipindi hicho Balozi Masood Khan kutoka Pakistani. Akitangaza mpango wa kazi wa Baraza la Usalama mbele ya waandishi wa habari mjini New York, [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unyanyapaa bado wakwamisha udhibiti wa Ukimwi

Kusikiliza / UKIMWI

Shirika lisilo la kiserikali linahusika na HIV na Ukimwi nchini India limetaja changamoto zinazolikabiili katika kazi ya kusaidia waathirika wa ugonjwa huo ikiwemo uhaba wa fedha na unyanyapaa. Loon Gange, ambaye ni Rais na mwanachama mwanzilishi wa DNP+ amesema kuwa ameshuhudia watu wengi wakiaga dunia kwa sababu hawakutibiwa kutokana na uhaba wa fedha na wengine [...]

03/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Utalii wa mazingira hutokomeza umaskini: UM

Kusikiliza / utalii wa mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la utalii, limesema kupitishwa kwa azimio linalotambua utalii wa viumbe na mazingira kama moja ya njia ya kupambana na umaskini na kulinda mazingira ni kitendo cha kupongezwa na kimefanyika wakati muafaka. Kwa mantiki hiyo shirika hilo limetaka nchi wanachama kubuni sera zitakazosaidia kuinua utalii wa mazingira ambao pia husaidia kutokomeza [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Udhibiti wa ajali za barabarani huokoa maisha na fedha: WHO

Kusikiliza / traffic

Utafiti mmoja uliochapishwa na jarida la shirika la afya ulimwenguni WHO, umesema nchi ambazo huchukua njia rahisi kudhibiti ajali za barabarani hunufaika na mambo mengi ikiwemo yale yenye taswira ya kiuchumi. Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la mwezi huu umesema kuwa pamoja na kwamba nchi hizo zinakubalika kwa kufaulu kuokoa maisha ya watu, lakini kwa [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashauriano kufanyika kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / baraza la usalama

Wakati hali ya usalama ikiendelea kudorora na kutia wasiwasi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baadaye leo litakuwa na mashauriano kuhusu hali ilivyo nchini humo. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA linasema kuwa watu wamekimbia makazi yao ikiwemo mji mkuu Bangui, na kwamba kuna [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yasaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii DRC

Kusikiliza / barabara nchini DRC

Kikundi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kimekamilisha ukarabati wa barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 600 kwenye ukanda ulioathiriwa na vita Mashariki mwa nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha amani na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mkuu wa ofisi ya MONUSCO jimbo la [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zambia yawapatia ukaazi wa kudumu wakimbizi wa Angola

Kusikiliza / wakimbizi wa Angola

Serikali ya Zambia imeanza kuwapatia hadhi ya ukaazi wa kudumu baadhi ya wakimbizi wa Angola nchini humo ambao wanakidhi vigezo vya uhamiaji. Mpango huo umeanza kufuatia usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na Umoja wa Afrika kwa kutoa dola Laki Moja kufanikisha mchakato huo wa kujumuisha wakimbizi wa Angola katika [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yatua kwa wakimbizi wa Rwanda huko Pakistani

Kusikiliza / wakimbizi wa Rwanda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza mpango wa kuwarejesha kwa hiari yao makwao kwa wakimbizi wa Rwanda walioko Pakistani. Wakimbizi hao ni wale walioingia nchini humo kwa shughuli mbali mbali ikiwemo masomo kama vilakini walishindwa kurejea nyumbani kutokana na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI [...]

03/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walioachiwa huru baada ya kutekwa na maharamia Somalia, wazungumza!

Kusikiliza / Mateka waliokuwa wanashikiliwa na maharamia wa kisomali

Kwa muda mrefu sasa huduma za usafirishaji wa mizigo katika pwani ya Somalia umekuwa ukikumbwa na visa vya mara kwa mara vya meli kutekwa nyara na maharamia ambapo mara nyingi maharamia hao hudai kulipwa pesa ili waweze kuwaachia wahusika hali inayosababisha hofu kubwa miongoni mwa wasafirishaji. Visa vya namna hiyo viliwakumba wafanyakazi waliokuwemo kwenye Meli [...]

02/01/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na vifo vya watu 61 huko Cote D'Ivoire

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon ametuma salamu za rambi rambi kwa serikali  ya Cote D'Ivoire na familia, jamaa na ndugu wa watu 61 waliopoteza maisha kufuatia kuibuka kwa kizazaa na msongamano baada ya sherehe za mwaka mpya huko Abidjan, nchini humo. Msemaji wa Ban amemkariri Katibu Mkuu huyo akisema kuwa amesikitishwa [...]

02/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado tuna wasiwasi mkubwa na hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati: UM

Kusikiliza / Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali ilivyo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na unaendelea kufanya mawasiliano na mwakilishi maaluma wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa nchini humo Margreth Voght. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo kuwa wakati wanaendelea na mawasiliano [...]

02/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Takwimu mpya zadokeza idadi ya vifo nchini Syria kuwa zaidi ya Elfu 60

Kusikiliza / Mji wa Homs Syria

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema takwimu mpya zinadokeza idadi ya watu waliokufa nchini Syria kutokana na mapigano yanayoendelea ni zaidi ya Elfu 60. Amesema upembuzi wa awali wa takwimu uliofanywa na wataalamu wa taarifa kwa niaba ya Umoja wa Mataifa umewezesha kukusanywa orodha ya watu [...]

02/01/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kemikali ya sumu au Aseniki iliyo kwenye maji yaweza kusababisha kansa

Kusikiliza / Maji yenye arseniki

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO, inasema uwepo wa kemikali ya sumu, aseniki katika maji ya kunywa na chakula kwa muda mrefu unaweza kusababisha saratani na vidonda vya ngozi.  WHO inasema aseniki imekuwa ikihusishwa na kuathiri vibaya ukuaji wa binadamu, ugonjwa wa moyo, uharibifu wa mfumo wa mishipa ya fahamu na ugonjwa wa [...]

02/01/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uturuki yafungua milango kwa wakimbizi wa Syria kujiunga na vyuo vikuu.

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria ambao sasa wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma nchini Uturuki

Uturuki imeanzisha programu ambamo kwayo wakimbizi wa Syria nchini humo wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma bila malipo yoyote ya ada. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema chini ya mpango huo wakimbizi wanaokidhi vigezo wataanza masomo yao kwenye vyuo vikuu saba mwezi Machi mwaka huu. UNHCR inasema hadi sasa wakimbizi [...]

02/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tumesikitishwa na vifo huko Cote d'Ivoire:UNOCI

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa huko Cote D'Ivoire Bert Koenders

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Côte d’Ivoire Bert Koenders ameelezea masikitiko yako kufuatia vifo vya watu 60 vilivyotokea saa chache baada ya kumalizika kwa mkesha wa mwaka mpya kwenye mji mkubwa zaidi nchini humo, Abidjan. Amesema vifo na majeruhi vilivyosababishwa na msongamano kwenye uwanja ambako sherehe za mwaka mpya zilikuwa [...]

02/01/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Jose Ramos-Horta kuwa mjumbe wake GUINEA –BISSAU

Kusikiliza / José Ramos-Horta na Katibu Mkuu Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Rais wa zamani wa Timor-Letse José Ramos-Horta kuwa mwakilishi wake maalumu nchini Guinea Bissau.Kwa wadhifa huo pia, Ramos-Horta anakuwa Mkuu wa ofisi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Joseph Mutaboba kutoka Rwanda ambapo imeelezwa kuwa Ramos-Horta kwa kushirikiana [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuimarisha amani nchini Somalia ni changamoto kubwa: Balozi Mahiga

Kusikiliza / mahiga-2

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesema bado kuna changamoto kubwa kufanikisha amani ya kudumu nchini Somalia na kwamba ndoto ianyotarajiwa ni nchi hiyo kuwa salama, ustawi na amani ndani yake na kati yake na jirani zaike. Taarifa zaidi na Alice Kariuki: (SAUTI YA ALICE KARIUKI)

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mateka waliookolewa kurejeshwa nyumbani: UNPOS

Kusikiliza / Meli ya MV Iceberg 1

 Umoja wa Mataifa kwa sasa unaongoza shughuli ya kuwarudisha makwao mateka waliookolewa hivi kutoka kwa maharamia wa kisomali baada ya miaka mitatu mikononi mwa maharamia hao. Mateka hao waliokolewa kufuatia oparesheni iliyochukua muda wa siku 15 iliyoongozwa na polisi wa baharini wa eneo la Puntland tarehe 23 mwezi Disemba mwaka uliopita. Mabaharia hao 24 ni wa [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada zaidi yahitajika Afghanistan

Kusikiliza / Afghanistan map

Hali mbaya ya usalama na kudorora kwa hali ya kibinadamu huenda vikaikumba Afghanistan mwaka huu wa 2013, yamesema mashirika ya kutoa misaada.  Mpango mpya wa kibinadamu wa mwaka 2013 uliochapishwa na Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA unasema kuwa kufuatia kuzoroteka kwa hali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wawili wa Jordan waliokuwa wametekwa sasa huru: UNAMID

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

  Walinda amani wawili wa Jordan waliotekwa wakati wakihudumu kwenye kikundi cha pamoja cha kulinda amani Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID wameachiwa huru baada ya kuwa matekani kwa siku 136. Msemaji wa UNAMID, Aicha Elbasri amesema kwa sasa wako salama na wanaelekea mji mkuu wa Sudan, Khartoum na baadaye watakwenda [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yatoa majibu ya uchunguzi dhidi ya FDLR na uvumi mwingine huko Kivu Kaskazini

Kusikiliza / Kivu Kaskazini

 Kundi la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MUNUSCO lililotumwa kubaini uvumi wa kuwasili kwa kundi la FDLR kutokaZambiakwenda mikoa ya Kivu ya Kaskazini wanasema kuwa uvumi huo si ukweli. Kupitia taarifa ya MONUSCO ni kwamba wameshirikina na jeshi la DRC miaka iliyopita kwa minajili ya kupunguza uwezo wa makundi [...]

02/01/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930