Ugonjwa wa Manjano wazidi kusambaa Darfur, chanjo ya dharura kuanza kutolewa: WHO

Kusikiliza /

homa ya manjano

Kampeni ya dharura ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya Manjano inaendelea huko Darfur nchini Sudan kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani, WHO limesema mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo Darfur ni mkubwa kuwahi kutokea sehemu yoyote duniani kwani watu 165 wamefariki dunia hadi sasa tangu mlipuko wa ugonjwa huo utokee mwezi Septemba na zaidi ya 732 wameugua.

Mwakilishi wa WHO nchini Sudan Dkt. Anshu Banerjee amesema kampeni hiyo ya chanjo inalenga watu Milioni Tano na Nusu kwenye maeneo yote yaliyokumbwa na ugonjwa huo huko Darfur.

(SAUTI YA Dkt. Banerjee)

"Wagonjwa wengi ni wafugaji wanaohamahama na ndio maana mlipuko wa ugonjwa huu unaenea Darfur yote. Chanjo ya dharura inalenga watu Milioni Tano na Nusu na itafanyika kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza ililenga watu Milioni Mbili nukta mbili. Ya pili inaanza wiki ijayo. Chanjo zinawasili Sudan jumapili ambapo kampeni itahusisha maeneo yote ya mijini. Hii ni kwa sababu ugonjwa ukiingia mjini kuna uambukizo wa haraka zaidi kutoka kwa mbu anayebeba vijidudu hadi kwa binamu kuliko vijijini ambako maambukizo kutoka kwa nyani anayebeba virusi vya ugonjwa huo kwenda kwa binadamu ni taratibu."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930