Wahamiaji wa Ethiopia waliokuwa wamekwama Yemen warejeshwa makwao: IOM

Kusikiliza /

wakimbizi wa Ethiopia

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limewarejesha makwao kwa ndege raia 210 wa Ethiopia waliokuwa wamekwama huko Yemen baada ya kushindwa kuingia Saudi Arabia kutafuta ajira.

IOM inasema imegharimu dola Milioni Mbili nukta Moja ambazo ni msaada kutoka Uholanzi kusafirisha raia hao ambao wanafikisha idadi ya raia 9,500 wa Ethiopia waliorejeshwa nyumbani kutoka Yemen kwa msaada wa IOM tangu mwaka 2010.

Waethiopia hao wanajumuisha wanawake, watoto, wazee ambapo baadhi yao ni wagonjwa. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031