Wafadhili waahidi dola milioni 384 kwa mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa mwaka 2013

Kusikiliza /

KM Ban Ki-moon na Valerie Amos

Wafadhili wamejitolea kuchanga jumla ya dola milioni 384 ambazo zitafadhili shughuli za dharura kuhudumia mamilioni ya watu wanaoathiriwa na majanga kufuatia ombi lililotolewa na Umoja wa Mataifa CERF. Akihutubia mkutano CERF uliondaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alimshukuru kila mmoja ambaye anajitolea kufadhili kuhakikisha kuwa maisha imeokolewa. Ban amesema kuwa CERF imesaidia wakati wa mafuriko na vita hasa kwenye maeneo ambayo hayapati ufadhili au yana ufadhili mdogo.

Mwaka huu pekee ufadhili wa mfuko wa CERF ambao ni jumla ya dola milioni 465 imesaidia katika utoaji wa huduma za kibinadamu kwenye nchi 49 zikiwemo Syria, Sudan Kusini, Haiti na Pakistan. Hata hivyo Ban amesema kuwa wakati Umoja wa Mataifa unaposhiriki katika mambo yakiwemo utatuzi wa mizozo na shughuli za kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kulinda haki za binadamu kazi yake haiwezi kuzuia kila janga.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930