Waasi wa M23 waripotiwa kukiuka azimio la UM: Waonekana Kivu Kaskazini

Kusikiliza /

M23 Goma

Hali ya usalama katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini imeripotiwa kuwa ni ya wasiwasi baada ya waasi wa kikundi cha M23 kuonekana katika viunga vya mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martini Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo kuwa kutokana na ripoti hizo kikosi cha kulinda amani cha umoja huo huko DRC, MONUSCO, mwishoni mwa wiki kiliimarisha doria zake za ardhini na angani.

"Ijapokuwa ripoti nyingi hazikuweza kuthibitishwa, lakini MONUSCO iliweza kuthibitisha uwepo wa waasi wa M23 kwenye maeneo kadhaa jimbo la Kivu Kaskazini ikiwemo karibu na Rwhindi, Kibati na Masisi karibu na Moja. Kitendo hicho ni kinyume na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2076. MONUSCO inaendelea na doria zake za mara kwa mara mjini Goma na viunga vyake."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031