Ushirikiano wa UNIFIL na LFA umeleta utulivu Kusini mwa Lebanon: Eliasson

Kusikiliza /

Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson aliyeko ziarani nchini Lebanon ametembelea kikosi cha muda cha kulinda amani nchini humoUNIFIL na kusema kuwa ushirikiano kati ya kikosi hicho na majeshi ya Lebanon, LAF umeleta amani ya aina yake Kusini mwa Lebanon.

Bwana Eliasson ametoa kauli hiyo baada ya kupatiwa maelezo ya operesheni za kikosi hicho kutoka kwa mkuu wake Meja Jenerali Paolo Serra.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema ushirikiano kati ya kikosi hicho na jeshi la Lebanon, LAF ni muhimu katika kutekeleza azimio namba 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutatua mzozo kati ya Lebanon na Israel.

"Mmefikia kiwango cha utulivu ambacho ni cha aina yake. Na nina matumaini kuwa itaendelea kuwa hivyo kwa ushirikiano na pande zote bila shaka. Na nafikiri kuwa ushirikiano kati ya UNIFIL na LAF ni muhimu na nina natumaini kuwa utaendelea, na taratibu uwepo wao hapa utaimarika."

Katika ziara hiyo Bwana Eliasson alikuwa ameambatana na Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya ajenda baada ya mwaka 2015 wa malengo ya Milenia, Bi. Amina Mohammed na Mshauri wa Katibu Mkuu na Katibu Mtendaji wa Tume ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia Magharibi, Bi. Rima Khalaf.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930