UNRWA yataka wakimbizi wa kipalestina wapatiwe ulinzi zaidi

Kusikiliza /

wakimbizi, UNRWA

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu na kusimamia ulinzi kwa wakimbizi wa Kipalestina, lUNRWA Filippo Grandi ameiomba Syria na pande zote katika mzozo nchini humo kuhakikisha wakimbizi wa Syria, popote pale walipo nchini humo wanapatiwa ulinzi.

Ombi la Grandi linafuatia picha zilizochapishwa na mashirika mbali mbali ya habari zinazoonyesha hali ya kusikitisha ya wakimbizi wa Syria waliojeruhiwa kwenye kambi ya Yarmouk.

UNRWA imesema picha hizo zinafuatiliwa kwa umakini na zinaibua wasiwasi mkubwa. Ripoti za awali zinaonyesha kufanyika kwa shambulio la anga dhidi ya kambi ya Yarmouk na kwamba hali katika kambi hiyo kwa sasa ni mbaya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031