UNICEF yazungumzia marufuku ya Urusi kwa Marekani kuasili watoto wa kirusi

Kusikiliza /

Anthony Lake

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeitaka serikali ya Urusi kuzingatia maslahi ya watoto katika mapendekezo yake mapya ya kupiga marufuku raia wa Marekani kuasili watoto wa kirusi.

Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake katika taarifa yake amesema mapendekezo yaliyopitishwa na bunge la Urusi la kuweka marufuku hiyo yanapaswa kuongozwa na utetezi wa maslahi ya watoto.

Inaelezwa kuwa bunge la Urusi limepitishwa muswada wa sheria wa kupiga marufuku hiyo ikisubiri Rais kuridhia au la, hatua ambayo inadaiwa kuchukuliwa kama kulipiza kitendo cha Marekani kushutumu Urusi kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Pamoja na kwamba UNICEF imeunga mkono hatua hiyo lakini imetaka madhila yanayokumba watoto wa kirusi katika taasisi mbalimbail yapewe kipaumbele ikiwemo kusaidia kuimarisha familia za kirusi, mipango ya ndani ya nchi ya kuasili watoto pamoja na makazi ya kudumu ya kulea watoto.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29