Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika watafuta fedha zaidi kukabiliana na waasi wa LRA

Kusikiliza /

waasi wa LRA

Katika harakati za kukabiliana na vitendo viovu vinavyofanywa na kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army kwenye maeneo ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zinatafuta fedha zaidi kutekeleza mipango yake ya kudhibiti kikundi hicho.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Kanda ya Afrika Ya kati, UNOCA Abou Moussa amelieleza Baraza la Usalama kuwa jambo la haraka zaidi ni kukamilisha nyaraka ya mpango wa utekelezaji na hatimaye kuchangisha fedha za kutosha kutekeleza mpango huo. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031