UM na mashirika ya kibinadamu yatoa ombi la msaaada kwa taifa la Haiti

Kusikiliza /

Nigel Fisher

Umoja wa Mataifa na washirika wa huduma za kibinadamu wametoa ombi la dola milioni 144 zitakazotumika kusaidia zaidi ya watu milioni moja nchini Haiti mwaka 2013. Ufadhili huo utayawezesha mashirika ya kutoka misaada kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula, ugonjwa wa kipindupindu na hamiaji kwenye taifa hilo la Caribbean.

Mratibu wa huduma za kibinadamu nchini Haiti Nigel Fisher amesema kuwa utawala nchini humo na washirika wa kutoa huduma za kibinadamu wamejitahidi na kupiga hatua tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini humo lakini hata hivyo mengi yanahitajika kufanywa. Fisher amesema kuwa ukame na vimbunga vikiwemo Isaac na Sandy ni baaadhi ya majanga ambayo yamewaacha mamilioni ya watu bila chakula na ajira na kuongeza kuwa ikiwa lolote halitafanyika yote yaliyoafikiwa yatakuwa ni kazi bure.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2014
T N T K J M P
« nov    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031