Ukatili dhidi ya wanawake unatisha: Cameroon matiti ya wasichana yapigwa pasi kuondoa mvuto

Kusikiliza /

 

Michelle Bachelet

Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN mjini New York, Marekani umemalizika kwa mataifa 12 kuitikia wito wa shirika hilo wa kuzitaka nchi dunia kuongeza juhudi za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Kupitia mpango mpya, COMMIT, nchi hizo ikiwemo Togo, Ufaransa, Marekani na Ugiriki, zimetoa ahadi kama vile kuboresha huduma kwa wanawake walioathirika na vitendo vya ukatili, kampeni za kitaifa za utetezi na uelimishaji dhidi ya madhila mbali mbali yanayokumba wanawake ikiwemo udhalilishaji kwenye sehemu za kazi na kuibua mipango bunifu ya kumkomboa mwanamke dhidi ya vitendo hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa UN-WOMEN Michelle Bachellet amesema hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kudai kuwa haina vitendo dhalili dhidi ya wanawake na watoto wa kike hivyo ni bora kushirikiana na kuvitokomeza.

Mkutano wa kujadili masuala ya ukatili kwa wanawake pia ulifanyika Bujumbora, Burundi, ukileta wajumbe kutoka nchi mbali mbali za Afrika ambapo Dokta Samba Kouyate kutoka Cameroon alitaja moja ya kitendo cha ukatili dhidi ya watoto wa kike nchini humo.

(SAUTI YA DKT. KOUYATE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031