Uhaba wa Maji Darfur wapatiwa suluhisho: UNAMID

Kusikiliza /

UNAMID

Tatizo la uhaba wa maji katika jimbo la Darfur huko Sudan limepatiwa ufumbuzi baada ya kikundi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni humo, UNAMID na benki ya Maendeleo ya Afrika, kwa ushirikiano na serikali ya Sudan kuzindua miradi kadhaa ya maji kwenye eneo hilo.

Miradi hiyo yenye lengo la kukidhi mahitaji ya muda mfupi na muda mrefu ya wakazi wapatao Laki Saba Na nusu wakiwemo wakulima na wafugaji ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa amani wa Doha kuhusu Darfur.

Benki ya maendeleo ya Afrika imetoa mkopo nafuu wa Euro Milioni Tatu nukta Tatu ambazo zitatumika kukarabati mitambo ya maji na ujenzi wa baadhi ya visima vya maji kwa lengo pia la kuhamasisha kurejea kwa wakimbizi wa ndani na wakimbizi kutoka maeneo mengine.

Akizungmza kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa UNAMID, Wolfgang Weiszegger ambaye ni mkurugenzi wa kitengo cha usaidizi cha kikundi hicho amesema UNAMID itaendelea kutoa misaada ya kiufundi na vifaa ili wakazi wa Darfur waishi kwa amani na wapate maendeleo ya kudumu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031