Uamuzi wa Baraza Kuu la UM wa kuanzisha siku ya kimataifa ya Radio wapongezwa

Kusikiliza /

Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne tarehe 18 Disemba limeridhia tarehe 13 ya mwezi Februari kila mwaka kuwa siku ya Radio duniani, ikiwa ni kutambua mchango wa Radio katika kurusha matangazo mbali mbali ya kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na vile vile kwa kutambua nafasi ya Radio ya Umoja wa Mataifa iliyoanzishwa tarehe 13 Februari mwaka 1946.

Je nini umuhimu wa siku hiyo na matangazo ya Radio ya Umoja wa mataifa kwa sasa? Bi, Edda Sanga, mmoja wa watangazaji wakongwe wa Radio nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni Meneja wa vyombo vya habari vya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, nchini Tanzania amemweleza Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa uamuzi huo ni wa kupongezwa na umekuja wakati muafaka.

(PKG- Mahojiano)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031