ITU yaelezwa jinsi simu za mkononi zinavyoimarisha huduma za kijamii

Kusikiliza /

simu ya mkono

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameripotiwa kusaidia kuimarisha sekta ya utoaji huduma mbali mbali nchini Tanzania, ikiwemo za afya na kiuchumi, na hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo Profesa John Nkoma ambaye yuko Dubai, Falme za kiarabu akishiriki mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano ya simu, ITU.

Profesa Nkoma ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa mapinduzi katika teknolojia ya mawasiliano ya simu yamekuwa chachu ya maendeleo ambapo kwa sasa baadhi ya huduma kama vile kwenda benki kulipa ada ya matumizi au kwenda hospitali kupata ushauri wa kitabibu inaweza kufanyika kutokea eneo lolote ali mradi kuna mtandao wa simu.

(SAUTI Profesa Nkoma)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031