Raia wasio na hatia kwenye mapigano ya Syria wanatupiwa macho zaidi na Jumuiya ya Kimataifa

Kusikiliza /

wakimbizi nchini Syria

Huku mapigano yakizidi kuchacha nchini Syria, Kamishna msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji UNHCR Erika Feller ametembelea eneo moja nchini Jordan linalohifadhi wakimbizi wa Syria kujionea hali jumla ya mambo.

Akiwa katika kambi ya Za'atri kamishna huyo ameshuhudia namna utoaji wa huduma za kisamaria zinavyowalenga zaidi raia wasio na hatia ambayo wameathiriwa na mapigano hayo na kwenda uhamishoni.

Kiasi cha raia milioni 2.5 wanatajwa kuathiriwa na mapigano hayo ambayo yameendelea kuvuruga ustawi wa kijamii wa taifa la Syria.

Kamishna huyo amesema kuwa wakati machafuko yakiendelea watu wasiokuwa na hatia ndiyo waathirika wakubwa wa mapaigano hayo na akazitaka pande zote kusitisha uhasama.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930